Tathmini yangu ya maaandamano ya CHADEMA

Tathmini yangu ya maaandamano ya CHADEMA

Kila pande ilipata inachotaka..Chadema imejifufua,na chawa wanamsifia mama kwa kukuza 'demokrasia'...mwisho wa siku Tanesco wakafanya yao Saa 12 jioni kama kawaida.
We jamaa una kipaji😂😂
 
Yalifanikiwa sana, na zile videos zinafanyiwa editing na SHIHATA na tunatarajia kuzituma Umoja wa Ulaya, US na UN, kuonyesha tumeifungua nchi kwa demokrasi ili kukamilisha mchakato wa kupewa fungu la kuendesha uchaguzi mwakani.
 
Hayakufanikiwa kwa sababu nadhani lengo la waanzisha maandamano lilikuwa ni kuona jeshi la polisi linayazuia ili wao waingie barabarani kwa nguvu halafu jeshi litumie nguvu kubwa kuyazuia na hatimae watu wapigwe na wengine kupata ulemavu kabisa ili tu wapate nafasi ya kusema na kuandikwa sana kwamba wananyimwa haki yao ya kuandamana

NB:- hayo ni mawazo yangu tu na naomba yaheshimiwe
Mbowe alitweet siku mbili kabla ya maandamano

Futa ujinga kichwani

View: https://x.com/freemanmbowetz/status/1749422409952751768?s=20
 
Yamefanikiwa kwa sababu serikali na polisi waliogopa kuwazuia
 
Kufanikiwa au kutofanikiwa tunaangakia sababu ya maandamano na matokeo ya maandamano. Maandamano yalikua ni kama kujichoresha tu, mie binafsi sijaona Cha maana ni kama maridhiano mbowe aliyofanya. Hamna Cha maana.
 
Hayakufanikiwa kwa sababu nadhani lengo la waanzisha maandamano lilikuwa ni kuona jeshi la polisi linayazuia ili wao waingie barabarani kwa nguvu halafu jeshi litumie nguvu kubwa kuyazuia na hatimae watu wapigwe na wengine kupata ulemavu kabisa ili tu wapate nafasi ya kusema na kuandikwa sana kwamba wananyimwa haki yao ya kuandamana

NB:- hayo ni mawazo yangu tu na naomba yaheshimiwe
"hayakufanikiwa kwa sababu nadhani...."

Punguza kuishi kwa hisia mkuu. Hujaeleweka kabisa.

Jibu lako hujalidhania, lakini sababu umeidhania.

Kama ni mtihani na lecturer wako anajielewa hapo tayari una 00.

Anyway, maoni yako yaheshimiwe kama ulivyotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani moja ya malengo ya kufanya maandamano ni kufikisha ujumbe! Ujumbe umefika kote duniani ambako wanapenda kufuatilia kinachotokea Tanzania.
Mwisho ni ipongeze Serikali kwa kuanza kukua kidemokrasia!
 
Back
Top Bottom