Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,412
- 283,609
Taarifa zingine zinadai kwamba Ujio wa Tundu Lissu na Godbless Lema, pamoja na kishindo cha Mikutano Kabambe ya hadhara iliyopangwa Kisomi na kuvurumishwa kwenye kanda kadhaa imekifanya chama hicho kujizolea umaarufu mkubwa, si tu Tanzania bali Dunia nzima.
Hata hivyo Taarifa kutoka ndani ya Chama hicho inaeleza kwamba kuanzia mwisho wa mwezi huu ndio kinaanza rasmi kufanya mikutano ya hadhara Nchi nzima na kwamba ile mliokuwa mnaiona huko Kanda ya Nyasa ilikuwa "FAGIA UWANJA TU" Mliokuwa mnaangalia sinema zamani mtanielewa kwamba kabla ya picha yenyewe kuanza , mlionyeshwa vipande fulani vilivyoitwa "Trela" ili kuwashawishi mlipe kiingilio kabla ya picha lenyewe kuanza .
Mungu Ibariki Chadema.
Mwisho, lakini si kwa Umuhimu, Nawashukuru Wana JF wote wa Jukwaa hili kwa kuniamini .