Tathmini ya hasara shirika la ndege la ATCL ianze katika manunuzi ya ndege

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,601
46,244
Watu watatikisa sana vichwa watakaposikia Shirika hilo limetengeneza hasara ya bilioni 60 kwa mwaka mmoja na limekuwa likitengeneza hasara kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini msiangalie tu hasara ya bilioni 60 kwa mwaka mmoa kutoka shirika la ndege la ATCL angalieni karibia Tirioni moja zilizotumika kununua ndege za shirika hilo na ambazo tija yake haijaonekana mpaka sasa

Ukiangalia historia za mashirika ya ndege ya SA, Kenya na Ethiopia yalivyo taabani miaka yote hakuna kitu cha ajabu ambacho ATCL itaweza kukifanya kutengeneza faida ni wakati sasa wa ATCL kubinafsishwa kwa sekta binafsi na serikali kujiondoa katika biashara ya ndege.
 
Tulishabinafsisha likiwa na ndege za kutosha by the time tunalirudisha lilikua na ndege moja tu choka mbaya.
Kenya airways imebinafsishwa imeshindikana now wanapambana kuirudisha serikalini...
Hakuna namna tuendelee kulilea tu.
 
Kagame ni kiboko hili chaka tuliloingizwa sio la mchezo
Halafu Ndege kwa sasa zinabeba Viongozi we Serikali tu na kuwapeleka kwenye Warsha na Seminaa mbalimbali za kutafuna Kodi kwa kujinafasi huku Wamachinga wanazidi kuahidiwa Wakae na kuyafunga mabarabara
 
Kenya airways inamalikiwa na wanahisa mbalimbali na serikali ndio mwanahisa mkubwa zaidi ila nayo ni tia maji tia maji tu, iko hoi taabani.
Tulishabinafsisha likiwa na ndege za kutosha by the time tunalirudisha lilikua na ndege moja tu choka mbaya.
Kenya airways imebinafsishwa imeshindikana now wanapambana kuirudisha serikalini...
Hakuna namna tuendelee kulilea tu.
 
Watu watatikisa sana vichwa watakaposikia Shirika hilo limetengeneza hasara ya bilioni 60 kwa mwaka mmoja na limekuwa likitengeneza hasara kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini msiangalie tu hasara ya bilioni 60 kwa mwaka MMOJA kutoka shirika la ndege la ATCL angalieni karibia Tirioni moja zilizotumika kununua ndege za shirika hilo na ambazo tija yake haijaonekana mpaka sasa

Ukiangalia historia za mashirika ya ndege ya SA, Kenya na Ethiopia yalivyo taabani miaka yote hakuna kitu cha ajabu ambacho ATCL itaweza kukifanya kutengeneza faida ni wakati sasa wa ATCL kubinafsishwa kwa sekta binafsi na serikali kujiondoa katika biashara ya ndege.
Ngoja wataalam wenye uelewa na uzoefu wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya anga waje kwanza watufumbue macho tatizo ni nini:
a) Gharama za uendeshaji ni kubwa sana kuliko mapato
b) Hakuna wateja wa kutosha kuliendesha shirika kwa faida

Sote tunajua biashara ya usafirishaji ni moja kati ya biashara ngumu sana. Hii ipo hata kwenye mabasi, malori, daladala na hata boda boda. Majirani zetu wa Kenyan Airways (KQ) nao wiki hii hii inayoisha walitangaza hasara kubwa tu kwa shirika lao huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni Uwepo wa ugonjwa Corona.

Hili shirika limepitia mikono yote - ya serikali na kampuni binafsi. Liliwahi kubinafsishwa. Unataka libinafsishwe tena umeona kuna tofauti gani na awali?
 
Biashara ya usafirishaji wa anga ni ngumu sana zinahitaji akili na fitna nyingi lakini Hii biashara ikifanywa na serikali ndio inakuwa kichaa zaidi, inakuwa hasara tupu ndio maana nchi nyingi zimeishia kuuza hisa za hayo mashirika au kuyabinafsisha kabisa.
Ngoja wataalam wenye uelewa na uzoefu wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya anga waje kwanza watufumbue macho tatizo ni nini:
a) Gharama za uendeshaji ni kubwa sana kuliko mapato
b) Hakuna wateja wa kutosha kuliendesha shirika kwa faida

Sote tunajua biashara ya usafirishaji ni moja kati ya biashara ngumu sana. Hii ipo hata kwenye mabasi, malori, daladala na hata boda boda. Majirani zetu wa Kenyan Airways (KQ) nao wiki hii hii inayoisha walitangaza hasara kubwa tu kwa shirika lao huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni Uwepo wa ugonjwa Corona.

Hili shirika limepitia mikono yote - ya serikali na kampuni binafsi. Liliwahi kubinafsishwa. Unataka libinafsishwe tena umeona kuna tofauti gani na awali?
 
Watu watatikisa sana vichwa watakaposikia Shirika hilo limetengeneza hasara ya bilioni 60 kwa mwaka mmoja na limekuwa likitengeneza hasara kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita
Hii ndio vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kiuchumu kati ya serikali na wananchi.🪖
 
Ngoja wataalam wenye uelewa na uzoefu wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya anga waje kwanza watufumbue macho tatizo ni nini:
a) Gharama za uendeshaji ni kubwa sana kuliko mapato
b) Hakuna wateja wa kutosha kuliendesha shirika kwa faida

Sote tunajua biashara ya usafirishaji ni moja kati ya biashara ngumu sana. Hii ipo hata kwenye mabasi, malori, daladala na hata boda boda. Majirani zetu wa Kenyan Airways (KQ) nao wiki hii hii inayoisha walitangaza hasara kubwa tu kwa shirika lao huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni Uwepo wa ugonjwa Corona.

Hili shirika limepitia mikono yote - ya serikali na kampuni binafsi. Liliwahi kubinafsishwa. Unataka libinafsishwe tena umeona kuna tofauti gani na awali?
Kuna mambo yakuzingatia katika hili suala
1. Wakati tunabinafsisha kipindi kile shirika lilikuwa tayari limekufa na uwekezaji ulikuwa sio wa tija maana mwekezaji hakununua ndege bali alitua zake SA na Precision kipindi hicho alipewa route ya SA.

2. Kweli gonjwa na corona na pia tokea kipindi kile cha tikisiko la uchumi mashitika mengi yalitetereka.

3. Ushindani wa kibiashara huwezi tegemea kupata faida kwa route za ndani ATCL ina route cha za nje na pia nazo sio daily ni once or twice a week hivyo unakuta ndege zinafanya route za ndani ambazo ni hasara kwa aina ya ndege zilizonunuliwa.
 
Basi wauze kabisa hayo mandege waachane na hiyo biashara. Hasara ya bilioni 60 inamaanisha gharama zimezidi mapato na hivyo hizo ni pesa za walipa kodi zinazoteketea.
Kuna mambo yakuzingatia katika hili suala
1. Wakati tunabinafsisha kipindi kile shirika lilikuwa tayari limekufa na uwekezaji ulikuwa sio wa tija maana mwekezaji hakununua ndege bali alitua zake SA na Precision kipindi hicho alipewa route ya SA.

2. Kweli gonjwa na corona na pia tokea kipindi kile cha tikisiko la uchumi mashitika mengi yalitetereka.

3. Ushindani wa kibiashara huwezi tegemea kupata faida kwa route za ndani ATCL ina route cha za nje na pia nazo sio daily ni once or twice a week hivyo unakuta ndege zinafanya route za ndani ambazo ni hasara kwa aina ya ndege zilizonunuliwa.
 
Kuna mambo yakuzingatia katika hili suala
1. Wakati tunabinafsisha kipindi kile shirika lilikuwa tayari limekufa na uwekezaji ulikuwa sio wa tija maana mwekezaji hakununua ndege bali alitua zake SA na Precision kipindi hicho alipewa route ya SA.

2. Kweli gonjwa na corona na pia tokea kipindi kile cha tikisiko la uchumi mashitika mengi yalitetereka.

3. Ushindani wa kibiashara huwezi tegemea kupata faida kwa route za ndani ATCL ina route cha za nje na pia nazo sio daily ni once or twice a week hivyo unakuta ndege zinafanya route za ndani ambazo ni hasara kwa aina ya ndege zilizonunuliwa.
Then what is the way forward???
Maana Corona bado ipo na itaendelea kuwepo mpaka mwakani. Tupoteze Billioni 60+ tena mwaka huu?
Nimesoma mahali kuhusu hasara za mashirika ya ndege na kukuta kumbe soko kubwa sana la ndege ni watalii, kwa hiyo njia kubwa sana ya kuongeza mapato ni kuongeza idadi ya watalii wanaokuja kwako na kuwashawishi watumie shirika lako.

Sasa sisi tunajikwamuaje katika hili? Vivutio vingi vya utalii tayari tunavyo na watalii wanakuja kiasi. Ila wengi wanakuja kwa madege ya nchi zao au mashirika ya nchi nyingine mbali na Air Tanzania. Labda watue Arusha kwenda Mbuga za wanyama au Mlima Kilimanjaro, then wakitaka kwenda Zanzibar ndio wanapanda Air Tanzania. Otherwise wanatoka na madege yao direct hadi Zanzibar, then Flight Link au Chartered Flights kwenda Mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro, Magoroto na kadhalika
 
Tulishabinafsisha likiwa na ndege za kutosha by the time tunalirudisha lilikua na ndege moja tu choka mbaya.
Kenya airways imebinafsishwa imeshindikana now wanapambana kuirudisha serikalini...
Hakuna namna tuendelee kulilea tu.
Mkuu naomba elimu kidogo NI LAZIMA NCHI KUWA NA SHIRIKA LA NDEGE linalotoa huduma ya usafirishaji???? Kama ni LAZIMA ni kwanini?
Kama SIYO LAZIMA kwanini sisi tunang'ang'ani kuwa nalo???

Asante!!
 
Back
Top Bottom