Hasara zilizosababishwa na Shirika la Ndege (ATCL) kwa miaka 9 mfululizo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,070
Hasara za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa miaka 9 (2014-2022)

2014/2015 - Tsh. Bilioni 94.3
2015/2016 - Tsh. Bilioni 109.2
2016/2017 - Tsh. Bilioni 113.8
2017/2018 - Tsh. Bilioni 26.6
2018/2019 - Tsh. Bilioni 48
2019/2020 - Tsh. Bilioni 60.24
2020/2021 - Tsh. Bilioni 36.2
2021/2022 - Tsh. Bilioni 35.2

Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zimeendelea kuonesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeendelea kupata hasara tangu Serikali ilipoamua kulifufua kwa kununua ndege mpya 12.

ATCL imekodishwa Ndege 11 zilizonunuliwa kwa Tsh. Tril 1.47 zinazotoa huduma ya Usafiri sehemu mbalimbali ndani na nje ya Nchi, baadhi yake zimepata hitilafu za kiufundi na 1 inashikiliwa Nchini Uholanzi.

Una maoni gani kuhusu hali ya Shirika hili la Serikali?
 
Tuliongea kuhusu Mzee kununua ndege bila business plan watu ooh acheni wivu. Waje waone hasara iliyo tengenezwa Toka aingie madarakani.

Wote hai ni vichwa vya wendawazimu. Haiwezekani tushindwe kuturn around toka 2015. Sometimes privatize huduma nyingine. Hakuna ulazima wa kujidai dai wakati tunakulaza uso
 
Na tena hasara halisi zimefichwa kati ya 2015-2021. Hasara halisi ni angalau mara mbili ya hizo!

Nilisema mwanzoni kabisa wakati Magufuli ananunua ndege hizo kama mbuzi kuwa kwa biashara ya ndege tujiandae kupigwa vibaya. Hii biashara ni ngumu hata kwa mataifa yaliyoendelea wanapata hasara sembuse Tanzania na uongozi mmbovu tulionao.
 
Tuliongea kuhusu Mzee kununua ndege bila business plan watu ooh acheni wivu. Waje waone hasara iliyo tengenezwa Toka aingie madarakani.

Wote hai ni vichwa vya wendawazimu. Haiwezekani tushindwe kuturn around toka 2015. Sometimes privatize huduma nyingine. Hakuna ulazima wa kujidai dai wakati tunakulaza uso
Huoni kama hasara imepungua?
 
Back
Top Bottom