BAO LA kisigino!!Kuna matatizo 7 ambayo CHADEMA bado hawayafahamu:
1. Hawajui priority ya matatizo ya watanzania
2. M4C imekuwa na propaganda zaidi kuliko kuwa na idiolojia ya kudumu juu ya kile kinacholenga kutatua matatizo ya watanzania. Hivyo imekipaka matope zaidi chama kuliko kukijenga, kwani watanzania wanaona kama mchezo wa kuigiza. Na ndio maana Zitto hakushabikia wala kushiriki katika M4C.
3. CHADEMA wanadhani watanzania ni WAJINGA/MAJINGA ya kudanganya danganya tu. Hili ni kosa kubwa.
4. Ukabila na Udini
5. Kutoelewa DEMOKRASIA. (Hili ni tatizo kubwa sana, halitatuliwa leo wala kesho). Kwa maana hiyo kuwapendekeza wagombea wasionamvuta kwa wananchi. Hii ni pamoja na uchaguzi wa ndani ya chama na nje(udiwani/ubunge) hata uwakilishi mbali mbali.
6. Mgao wa Ruzuku.
7. Kudhani kuwa Fujo, mapigano, vurugu ndio siasa zinazohitajika Tanzania. Wakati mwingine wakisema hadharani kuwa watanzania ni WAOGA.
Na kwa hayo, ndio sababu kubwa ya wananchi kutojitokeza katika kupiga kura. Kwani walikuwa na imani sana na CHADEMA, na imewafikisha pabaya na wala hawanahaja na CCM. Hawa wamechagua kususia uchaguzi.
! Matokeo haya ni taswira tosha juu ya uchaguzi mkuu 2015. Awe Slaa, Mbowe , pindi wataposhindwa wasizingizie kuwa wamepigwa bao, bali hiyo ndio itakuwa hali halisi. Tena mgombea wa urais wa CHADEMA akipata 10% ashukuru Mungu