Tathimini ya ufanisi wa CHF na wanaotumia NHIF ifanyike kwa kina kabla ya kuja na bima ya afya kwa wote

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
228
551
Swala la kuwa na bima ya afya ni la msingi sana kwa kila mwananchi. Hata hivyo kwa Tanzania yetu swala la kuwa na kadi ya bima ni moja na swala la kupata huduma kupitia bima hiyo ni lingine

Naamini kabisa CHF ilikuja Kama mta ngulizi wa bima ya afya kwa wote. NHIF wakafuatia kwa kuleta vifurushi vya bima kulingana na uwezo wa mwananchi. Kundi pekee linaloendelea kutumia hivi vifurushi kwa wingi ni wanafunzi wa vyuo pengine kwasababu ni sehemu ya takwa la kanuni za vyuo husika na urahisi wa kuhudumiwa na hospital zilizomo vyuoni au karibu na vyuo

Kwanini hamasa ya kutumia bima kwa wananchi iko chini sana?

Kwanini vituo vingi vya kutolea huduma haviwapi kipaumbele wananchi wenye bima?

Haya ni maswali ambayo serikali lazima ije na masuruhisho kabla ya kuja na bima kwa wote

Lazima yaandaliwe mazingira mazuri ambayo mwananchi mwenyewe atahamasika kutumia bima.

Kusema bila kadi ya bima hutapata lesseni, au passport ni kukosa ubunifu. Mazingira ya kuhudumiwa lazima yamvutie mwananchi mwenyewe kuitafuta bima ilipo.

Siku hizi baadhi ya hospital ukienda na bima unaambiwa dawa fulani ukanunue (zamani ulikuwa unapewa kibali cha NHIF kwenda kuzitafuta pharmacy) lakini bill inayotumwa kwenye msg unakuta iko juu sana ambayo ni dhahiri inakuwa imejumlisha na dawa ulizokosa kwenye dirisha la dawa ukaenda kuzinunua kwa cash sehemu nyingine.

Huku ni kuibia hii mifuko!

Haya yasipotatuliwa Kwanza tutaongeza tatizo juu ya tatizo
 
Back
Top Bottom