Mazingira ya chaguzi ndogo ni tofauti kabisa na mazingira wakati chaguzi kuu zinapofanyika !
Vyama kwa ujumla huwa vinaconcentrate resources zake zote kwenye chaguzi hizi kwani hakuna chaguzi nyingine katika sehemu nyingine. Viongozi wa kitaifa wa vyama na viongozi wengine kama wabunge wanakuwa kwa wingi sana kwenye chaguzi ndogo tofauti na wakati wa chaguzi kuu, kwani wakati wa chaguzi kuu kila mtu anaconcentrate kwenye eneo lake !
Ni kweli mazingira ya chaguzi ndogo ni tofauti na chaguzi kuu lakini zoezi zima la uchaguzi katika chaguzi ndogo kwa kiwango kikubwa linatoa akisi la zoezi zima la uchaguzi mkuu.
Kama kuna maandalizi mazuri yanayochangiwa na mizizi ya chama katika maeneo hayo kuanzia katika kaya, haihitaji kuwa na timu nzima ya chama (viongozi wakuu) kufanya kampeni. Kukosekana kwa mizizi ya chama katika maeneo ya jimbo la uchaguzi lililowazi ndiyo kunasababisha chama kuwa reactive pale chaguzi ndogo zinapojitokeza katika majimbo la uchaguzi.
Imagine kwa mfano kwa upande wa CDM wabunge karibia wote watakuwa Kalenga, pamoja na madiwani wengi tu pamoja na viongozi wengine wa kitaifa. Vile vile wabunge peke yao wamechanga million 98 kwa ajili ya kumpiga tafu Grace kwenye uchaguzi wa Kalenga !. Na ninakuhakikishia CCM resources zao (especially zile za kuhonga) zitakuwa kubwa mno ! Haya yote huwezi kuyakuta kwenye chaguzi kuu !
Tunarudi kwenye hoja ile ile ambayo ndiyo mzizi wa hoja yangu.
Kama hii ndiyo mikakati, watafanyaje wakati wa chaguzi katika majimbo ya uchaguzi zaidi ya 230 yanayofanya kampeni na uchaguzi kwa muda mmoja.
Mzizi wa hoja yangu ndiyo huu kwa sababu kama wananchi wa maeneo mengi hawawezi kuaminiwa na chama na kukabidhiwa kazi katika mchakato mzima wa uchaguzi, chama kitatoa wapi watu inaowaamini kwenda kwenye majimbo yote ya uchaguzi kusimamia zoezi la uchaguzi katika uchaguzi mkuu.
Wale wezi wa kura (either kwa kuiba au kuhonga) inakuwa rahisi kufanya kwenye chaguzi ndogo sababu eneo la concentration ni dogo, na kwa mfano wakitafuta hela kama billion 1 inaweza ikaleta impact kubwa sana tofauti na hata billion 10 kwenye chaguzi kuu !
Hivyo katika mazingira hayo, mbinu zinazotumika kwa kila Chama lazima ziwe tofauti. Kama chama kinahisi kitaibiwa kura au mawakala wake wanaweza wakanunuliwa, then inabidi kitafute watu ambao wana uelewa na uzalendo wa kushinda hayo majaribu !....Na kwa sababu kaeneo ka concentration ni kadogo Chama kinachotaka kuhonga kama kina resources kinaweza kikawahonga mawakala wengi tu kwa hela nyingi ambazo most of them wanaweza kujaribiwa na kununulika....
Chama hakiwezi kikawa na wanachama wanakiamini wakati chama hakiwaamini wanachama wake. Uhai wa chama unategemea sana kujengeka katika imani kati ya wanachama na viongozi kuanzia ngazi za kijiji mpaka taifa. Chama kinapaswa kiweke imani kwa wanachama wake ili wanachama waweze hata kuwashawishi wananchi wengine na kukiamini chama na katika kukiamini chama, ndiyo watakapo kipigia kura katika chaguzi mbali mbali za kitaifa.
Hili la kununua mawakala linatokea sana ndugu yangu na Mbunge mmoja wa CCM alinithibitishia kwamba huwa wanafanya hivyo kunapokuwa na opportunity......Hivyo sioni ubaya wa CDM kufanya hivyo katika mazingira haya na sioni hilo linaweza kuwa problem kwa mwanachadema wa kweli !
Huwa siamini hii dhana ya kusema mawakala wananunuliwa otherwise, chama kitakuwa kinaweka mawakala wa kuokota na siyo wanachama wanaokipenda na kukipigania chama.
Hii hoja yako ina sadifu kile nilichokuwa ninakisema.
Maandalizi yanayofanyika mapema yanaweza kuondoa tatizo kama hili ambalo mzizi wake ni kukosa kuaminiana kati ya wanachama na viongozi wa chama. Kama chama hakifahamu hata wanachama wake ni rahisi sana kupata mamluki ambao wanadai ni wanachama lakini kiuhalisia siyo wanachama.
Chama kinapofahamu wanachama wake hata katika uchaguzi kinakuwa kinafahamu wastani wa kura ambazo kitapata kutoka kwa wanachama wake achilia mbali wananchi wengine.