Taswira ya uchaguzi Kalenga, CHADEMA hawana mikakati mbadala ya kushinda uchaguzi mkuu.

Ndio maana nakuambia wewe hujui kitu ni mpiga porojo tu wa kwenye keyboard, uchaguzi wa madiwani ufanyika pamoja na wa Rais acha porojo.
Wewe ndiyo unaandika bila kuelewa hata hoja unayoichambua, inawezekana unasoma andiko lingine!.

Wapi nimesema uchaguzi wa Rais pamoja na madiwani unafanyika siku moja?.
 
Mazingira ya chaguzi ndogo ni tofauti kabisa na mazingira wakati chaguzi kuu zinapofanyika !

Vyama kwa ujumla huwa vinaconcentrate resources zake zote kwenye chaguzi hizi kwani hakuna chaguzi nyingine katika sehemu nyingine. Viongozi wa kitaifa wa vyama na viongozi wengine kama wabunge wanakuwa kwa wingi sana kwenye chaguzi ndogo tofauti na wakati wa chaguzi kuu, kwani wakati wa chaguzi kuu kila mtu anaconcentrate kwenye eneo lake !

Imagine kwa mfano kwa upande wa CDM wabunge karibia wote watakuwa Kalenga, pamoja na madiwani wengi tu pamoja na viongozi wengine wa kitaifa. Vile vile wabunge peke yao wamechanga million 98 kwa ajili ya kumpiga tafu Grace kwenye uchaguzi wa Kalenga !. Na ninakuhakikishia CCM resources zao (especially zile za kuhonga) zitakuwa kubwa mno ! Haya yote huwezi kuyakuta kwenye chaguzi kuu !

Wale wezi wa kura (either kwa kuiba au kuhonga) inakuwa rahisi kufanya kwenye chaguzi ndogo sababu eneo la concentration ni dogo, na kwa mfano wakitafuta hela kama billion 1 inaweza ikaleta impact kubwa sana tofauti na hata billion 10 kwenye chaguzi kuu !

Hivyo katika mazingira hayo, mbinu zinazotumika kwa kila Chama lazima ziwe tofauti. Kama chama kinahisi kitaibiwa kura au mawakala wake wanaweza wakanunuliwa, then inabidi kitafute watu ambao wana uelewa na uzalendo wa kushinda hayo majaribu !....Na kwa sababu kaeneo ka concentration ni kadogo Chama kinachotaka kuhonga kama kina resources kinaweza kikawahonga mawakala wengi tu kwa hela nyingi ambazo most of them wanaweza kujaribiwa na kununulika....

Hili la kununua mawakala linatokea sana ndugu yangu na Mbunge mmoja wa CCM alinithibitishia kwamba huwa wanafanya hivyo kunapokuwa na opportunity......Hivyo sioni ubaya wa CDM kufanya hivyo katika mazingira haya na sioni hilo linaweza kuwa problem kwa mwanachadema wa kweli !
 
Kama mimi ni mnafiki, wewe ni nani?.

Ungechambua na kuonyesha unafiki wangu ndani ya hoja angalau ungewasaidia watakao soma andiko lako, kinyume cha hivyo, utaonekana ni debe tupu.

Ngoja nikuchambulie unafiki wako:

Mnafiki kwa sababu tunajua wazi hauko CHADEMA, sasa ni aidha huna Chama au uko CCM.

Kama huna upande sasa kwa nini usiwashauri na CCM kwani na wao wameleta watu vilevile.

Kama uko CCM pilipili usizozila zakuwashiani?
 
Mijitu Kama hii ni mijizi ya demokrasia,,, inamanipulate hoja ili ipate kuwashawishi watoe hela wa lumumba wakate mshiko bila kujali kuwa halijafika field. Huu ni wizi tu Kama wizi mwingine.

Hebu weka data, Chadema imepeleka walinda kura wangapi, wamepangwa kata zipi na wenyeji watakuwa wapi siku hiyo?
 
Unaitwa mnafiki kwa sababu hoja zako ni propaganda tu za ccm.cdm wanajua wanapambana na jizi la kimataifa wamewaleta watu wenye uzoefu na wezi na kimataifa wa kula.
 
Mleta mada kajiuliza kuwa,Kwa nini kalenga wamemwagwa policcm wengi kutoka mikoa ya jirani? Je 2015 watakuwepo kalenga ili kufanikisha wizi wa kura? Na je,kwa nini kuna greengard kibao toka maeneo ya jirani? Au wao ruksa ila nongwa ni kwa cdm tu? Jipange upya,njaa ya tumbo isikufanye mwe.hu!
 
Mazingira ya chaguzi ndogo ni tofauti kabisa na mazingira wakati chaguzi kuu zinapofanyika !

Vyama kwa ujumla huwa vinaconcentrate resources zake zote kwenye chaguzi hizi kwani hakuna chaguzi nyingine katika sehemu nyingine. Viongozi wa kitaifa wa vyama na viongozi wengine kama wabunge wanakuwa kwa wingi sana kwenye chaguzi ndogo tofauti na wakati wa chaguzi kuu, kwani wakati wa chaguzi kuu kila mtu anaconcentrate kwenye eneo lake !
Ni kweli mazingira ya chaguzi ndogo ni tofauti na chaguzi kuu lakini zoezi zima la uchaguzi katika chaguzi ndogo kwa kiwango kikubwa linatoa akisi la zoezi zima la uchaguzi mkuu.

Kama kuna maandalizi mazuri yanayochangiwa na mizizi ya chama katika maeneo hayo kuanzia katika kaya, haihitaji kuwa na timu nzima ya chama (viongozi wakuu) kufanya kampeni. Kukosekana kwa mizizi ya chama katika maeneo ya jimbo la uchaguzi lililowazi ndiyo kunasababisha chama kuwa reactive pale chaguzi ndogo zinapojitokeza katika majimbo la uchaguzi.
Imagine kwa mfano kwa upande wa CDM wabunge karibia wote watakuwa Kalenga, pamoja na madiwani wengi tu pamoja na viongozi wengine wa kitaifa. Vile vile wabunge peke yao wamechanga million 98 kwa ajili ya kumpiga tafu Grace kwenye uchaguzi wa Kalenga !. Na ninakuhakikishia CCM resources zao (especially zile za kuhonga) zitakuwa kubwa mno ! Haya yote huwezi kuyakuta kwenye chaguzi kuu !
Tunarudi kwenye hoja ile ile ambayo ndiyo mzizi wa hoja yangu.

Kama hii ndiyo mikakati, watafanyaje wakati wa chaguzi katika majimbo ya uchaguzi zaidi ya 230 yanayofanya kampeni na uchaguzi kwa muda mmoja.

Mzizi wa hoja yangu ndiyo huu kwa sababu kama wananchi wa maeneo mengi hawawezi kuaminiwa na chama na kukabidhiwa kazi katika mchakato mzima wa uchaguzi, chama kitatoa wapi watu inaowaamini kwenda kwenye majimbo yote ya uchaguzi kusimamia zoezi la uchaguzi katika uchaguzi mkuu.
Wale wezi wa kura (either kwa kuiba au kuhonga) inakuwa rahisi kufanya kwenye chaguzi ndogo sababu eneo la concentration ni dogo, na kwa mfano wakitafuta hela kama billion 1 inaweza ikaleta impact kubwa sana tofauti na hata billion 10 kwenye chaguzi kuu !

Hivyo katika mazingira hayo, mbinu zinazotumika kwa kila Chama lazima ziwe tofauti. Kama chama kinahisi kitaibiwa kura au mawakala wake wanaweza wakanunuliwa, then inabidi kitafute watu ambao wana uelewa na uzalendo wa kushinda hayo majaribu !....Na kwa sababu kaeneo ka concentration ni kadogo Chama kinachotaka kuhonga kama kina resources kinaweza kikawahonga mawakala wengi tu kwa hela nyingi ambazo most of them wanaweza kujaribiwa na kununulika....
Chama hakiwezi kikawa na wanachama wanakiamini wakati chama hakiwaamini wanachama wake. Uhai wa chama unategemea sana kujengeka katika imani kati ya wanachama na viongozi kuanzia ngazi za kijiji mpaka taifa. Chama kinapaswa kiweke imani kwa wanachama wake ili wanachama waweze hata kuwashawishi wananchi wengine na kukiamini chama na katika kukiamini chama, ndiyo watakapo kipigia kura katika chaguzi mbali mbali za kitaifa.
Hili la kununua mawakala linatokea sana ndugu yangu na Mbunge mmoja wa CCM alinithibitishia kwamba huwa wanafanya hivyo kunapokuwa na opportunity......Hivyo sioni ubaya wa CDM kufanya hivyo katika mazingira haya na sioni hilo linaweza kuwa problem kwa mwanachadema wa kweli !
Huwa siamini hii dhana ya kusema mawakala wananunuliwa otherwise, chama kitakuwa kinaweka mawakala wa kuokota na siyo wanachama wanaokipenda na kukipigania chama.

Hii hoja yako ina sadifu kile nilichokuwa ninakisema.

Maandalizi yanayofanyika mapema yanaweza kuondoa tatizo kama hili ambalo mzizi wake ni kukosa kuaminiana kati ya wanachama na viongozi wa chama. Kama chama hakifahamu hata wanachama wake ni rahisi sana kupata mamluki ambao wanadai ni wanachama lakini kiuhalisia siyo wanachama.

Chama kinapofahamu wanachama wake hata katika uchaguzi kinakuwa kinafahamu wastani wa kura ambazo kitapata kutoka kwa wanachama wake achilia mbali wananchi wengine.
 
Mleta mada kajiuliza kuwa,Kwa nini kalenga wamemwagwa policcm wengi kutoka mikoa ya jirani? Je 2015 watakuwepo kalenga ili kufanikisha wizi wa kura? Na je,kwa nini kuna greengard kibao toka maeneo ya jirani? Au wao ruksa ila nongwa ni kwa cdm tu? Jipange upya,njaa ya tumbo isikufanye mwe.hu!
Kwa hiyo CHADEMA wanamwaga watu Kalenga kwa vile CCM pia wamemwaga watu. Kwa hiyo CHADEMA wanachofanya ni copy & Paste ya mikakati ya CCM.

Nini tofauti yao na CCM kimkakati katika chaguzi nchini.
 
hahahahah yaani hapa ukitaka mashiko sifia chadema tuu ! Rubishhhhhhhhhhhhhhhh mmetudharau wanyalu kweli kutuletea bangi toka arusha
 
Hoja unayo lakini inatizama upande mmoja wa kuona upungufu na si mazingira yanayosababisha hayo ni nini. Ukumbuke kwamba uchaguzi huu ni muhimu sn kwa vyama vyote vyenye ushindani wa karibu huko Kalenga. Ukiiangalia CDM kupeleka vijana toka maeneo mbalimbali kwenda Kalenga kulinda kura. Iangalie CCM, Angalia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Vyote kwa pamoja vinatoa watu mikoani na kwenda kulinda sehemu hizo! Je uchaguzi mkuu vitafanyeje? Watu wa kulinda kura Kalenga ni wazi wapo, lakini unapoona kuna umuhimu wa kuongeza nguvu ya ziada ni vyema kufanya hivyo! Hasa pale nguvu hiyo ikiwepo bila kuwa na kazi nyingine kwa wakati huo!
 
Kwa hiyo CHADEMA wanamwaga watu Kalenga kwa vile CCM pia wamemwaga watu. Kwa hiyo CHADEMA wanachofanya ni copy & Paste ya mikakati ya CCM.

Nini tofauti yao na CCM kimkakati katika chaguzi nchini.

unahangaika sana gamba wewe, cdm lazima iongeze nguvu za kuwadhibiti hao janjaweed wa greengurd na policcm waliomwagwa huko!!!
 
Kwa hiyo CHADEMA wanamwaga watu Kalenga kwa vile CCM pia wamemwaga watu. Kwa hiyo CHADEMA wanachofanya ni copy & Paste ya mikakati ya CCM.

Nini tofauti yao na CCM kimkakati katika chaguzi nchini.

ni mwendawazimu tu asiyefahamu mazimgira ya chaguzi za tz,kama kungekuwa na tume huru ya uchaguzi pamoja na jeshi la polis lisilotumika kwa maslahi ya kisiasa basi chaguzi nyingi zingefanyika bila ulazima wa vijana kupelekwa kuongeza ulinzi wa kura!!!!
 
Wewe ndiyo unaandika bila kuelewa hata hoja unayoichambua, inawezekana unasoma andiko lingine!.

Wapi nimesema uchaguzi wa Rais pamoja na madiwani unafanyika siku moja?.
Mkuu Ng'wamapalala

Haujawazoea hawa vijana wa Chadema, hawa karibia wote fikra zao zinafanana ukitaka wakushambulie wewe elezea mapungufu yao.

Chadema wanadhani uchaguzi ni siku ya kupiga kura tu hawajui kama siku hiyo ndiyo uchaguzi unakamilika.

Kila siku nawambia Chadema hawawezi kutwaa dola kwa Chopa tu, wananchi wanaitaji kufahamishwa watafanyiwa nini.
 
Last edited by a moderator:
nimejaribu kiangalia kwa mtazamo wa tanzania na siyo jimbo la kalenga pekee.

Kwa angalizo lako una maana training inafanyika pale kunapokuwa na uchaguzi!.

Kwa sasa kuna miezi tu kabla ya uchaguzi wa madiwani. Nani na muda gani atatoa training kwa zaidi ya kata 3000.

Haya bana, acha hiyo sindano iingie taratibu huku nikipiga kelele kama ilivyo mtazamo wako. Daktali makini akisikia kelele za mgonjwa wakati akimchoma sindano lazima atataka kufahamu kulikoni!.
uchaguzi upi wa madiwani unaousema , madiwani watachaguliwa mwakani wala sio kipindi hiki, mwaka huu kuna uchaguzi wa serikali za mitaa
 
yawn5.jpg
 
Haya unayoongea ni sawa, ila hayo yanaweza yakawa malengo ya muda mrefu lakini si ya muda mfupi. Hili wanalolifanya ni njia mojawapo ya kufikia malengo hayo...

Chama kuwa na watu nchi nzima ambao wameshiba sera za chama na hivyo kutoyumbishwa kwa namna yeyote ni swala la process ya muda mrefu inayohitaji resources za fedha pamoja na watu. Ukirudi miaka ya nyuma kidogo, CDM wasingekuwa na uwezo wa kuwapata hata hao wa kutoka mikoa mingine ! Sasa wanaweza kuwapata hao wa kutoka mikoa mingine kwa idadi ya kutosha na probably wawili watatu kutoka hapo hapo Kalenga !.... With time and hard work hii idadi ya wanachama waliokomaa itaenea Tz nzima !

Lakini kilicho mbele ya CDM sasa hivi ni uchaguzi wa Kalenga. Na kama unachoice cha either kufanya hilo unalotaka wewe na kuhatarisha ushindi au kutumia mawakala ambao wametestiwa na kuaminiwa hivyo kuondoa mwanya huo na probably kusababisha ushindi...inabidi uchague kati ya hayo mawili. Huwezi kuyapata yote kwa sasa hivi. Mimi naona walilolichagua ni bora kwani ushindi kwa Kalenga kwa sasa hivi ni bora zaidi...Wewe probably unaona vinginevyo kwamba ikibidi hata kwa kuhatarisha ushindi watumie hiyo option ya kumwamini kila mtu kwa jukumu zito kama la uwakala eti kwa sababu tu ni mwanachama wa CDM !......Ninaamini hauko sahihi !

Hivi unajua hata Arumeru walitumia baadhi ya mawakala kutoka nje ya Arumeru ?...Tukifuata msingi wa hoja yako ni kwamba hawakuwaamini watu wa Arumeru. Sasa hebu fikiri, CDM baada ya kuchaguliwa Nassari imekuwa au imesinyaa Arumeru ?. Ninaamini imekuwa sana tu, na probably kati ya hao waliotoka sehemu nyingine baadhi yao wametoka Arumeru.

Ikiwa Grace atashinda Kalenga, CDM watakuwa wameweka misingi thabiti ya kujijenga zaidi hapo Kalenga na upatikanaji wa makada walioiva CDM watapikwa kwa urahisi zaidi na baada ya hapo si kwamba kutakuwa na mawakala ambao wanaweza kuaminiwa kupambana na mikiki mikiki ya CCM hapo Kalenga, bali hata nao wanaweza kupelekwa katika sehemu nyingine kutoa msaada !

Ni kweli mazingira ya chaguzi ndogo ni tofauti na chaguzi kuu lakini zoezi zima la uchaguzi katika chaguzi ndogo kwa kiwango kikubwa linatoa akisi la zoezi zima la uchaguzi mkuu.

Kama kuna maandalizi mazuri yanayochangiwa na mizizi ya chama katika maeneo hayo kuanzia katika kaya, haihitaji kuwa na timu nzima ya chama (viongozi wakuu) kufanya kampeni. Kukosekana kwa mizizi ya chama katika maeneo ya jimbo la uchaguzi lililowazi ndiyo kunasababisha chama kuwa reactive pale chaguzi ndogo zinapojitokeza katika majimbo la uchaguzi.

Tunarudi kwenye hoja ile ile ambayo ndiyo mzizi wa hoja yangu.

Kama hii ndiyo mikakati, watafanyaje wakati wa chaguzi katika majimbo ya uchaguzi zaidi ya 230 yanayofanya kampeni na uchaguzi kwa muda mmoja.

Mzizi wa hoja yangu ndiyo huu kwa sababu kama wananchi wa maeneo mengi hawawezi kuaminiwa na chama na kukabidhiwa kazi katika mchakato mzima wa uchaguzi, chama kitatoa wapi watu inaowaamini kwenda kwenye majimbo yote ya uchaguzi kusimamia zoezi la uchaguzi katika uchaguzi mkuu.

Chama hakiwezi kikawa na wanachama wanakiamini wakati chama hakiwaamini wanachama wake. Uhai wa chama unategemea sana kujengeka katika imani kati ya wanachama na viongozi kuanzia ngazi za kijiji mpaka taifa. Chama kinapaswa kiweke imani kwa wanachama wake ili wanachama waweze hata kuwashawishi wananchi wengine na kukiamini chama na katika kukiamini chama, ndiyo watakapo kipigia kura katika chaguzi mbali mbali za kitaifa.

Huwa siamini hii dhana ya kusema mawakala wananunuliwa otherwise, chama kitakuwa kinaweka mawakala wa kuokota na siyo wanachama wanaokipenda na kukipigania chama.

Hii hoja yako ina sadifu kile nilichokuwa ninakisema.

Maandalizi yanayofanyika mapema yanaweza kuondoa tatizo kama hili ambalo mzizi wake ni kukosa kuaminiana kati ya wanachama na viongozi wa chama. Kama chama hakifahamu hata wanachama wake ni rahisi sana kupata mamluki ambao wanadai ni wanachama lakini kiuhalisia siyo wanachama.

Chama kinapofahamu wanachama wake hata katika uchaguzi kinakuwa kinafahamu wastani wa kura ambazo kitapata kutoka kwa wanachama wake achilia mbali wananchi wengine.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom