TASAF, nakuja kwenye Usaili wenu wiki ijayo, naamini mtatenda Haki na si kupendelea

nyapinyapileo

Member
Oct 19, 2022
93
215
Wana JF Salaam,

Naenda kwenye Usaili TASAF Dar es Salaam weekend hii. Usaili ni Jumatatu na Jumanne wiki ijayo(nafasi ni Ukurugenzi wa Idara moja pale TASAF). Kwa kuwa nasafiri umbali mrefu kutoka huku Kigoma mwisho wa Reli mpaka Dar, natumia gharama kubwa.

Nimejiandaa vizuri, lakini nina wasiwasi kama hawa jamaa hawana mtu wao wa ndani hivyo sie wengine ni geresha tu kutupotezea muda na pesa. Nawaonya TASAF mtende Haki maana natumia gharama kubwa kuja huko, ole wenu mpendelee NITAWAROGA Menejimenti nzima. Ole wenu
 
Je wewe ungekua ndio meneja wa TASAD alafu kuna nafasi mmetangaza na una mdogo wako hana ajira.

Je utampa nafasi mdogo wako au utaajiri wengine?

(Kuwa mkweli).
 
Kama ni hivyo wala usiende kwa sababu hawajakulazimisha kwenda kwny usaili wao
 
Kwahiyo mkuu unahisi wewe kupata hiyo kazi ndio watakuwa wametenda Haki?
 
Yani nafasi ya ukurugenzj unadhani watakuchkua we fresher kutoka kigoma

Hio wanafanya internally tu

Unapoteza mda kwenda
 
Weka majina yako kamili ili tukufaham kwamba ukija, huitaji kuonewa. Andika majina yako kamili tafadhali.
 
Muache aje then aliwe kichwa. Muhimu ni kubandika hii "nickname" yake ukutani karibu na mlango wa kuingilia. Akiitazama TU mara mbili, anapewa swali gumu na analiwa kichwa😂
Hii mbinu ya kikamanda tena kwa herufi kubwa NYAPI NYAPI LEO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…