TAS Taifa yakanusha tuhuma dhidi ya wizara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAS Taifa yakanusha tuhuma dhidi ya wizara

Discussion in 'JF Doctor' started by Rutashubanyuma, Jan 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,395
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280
  TAS Taifa yakanusha tuhuma dhidi ya wizara


  Na Anneth Kagenda

  CHAMA cha Albino Tanzania (TAS), kimekanusha shutuma zilizotolewa na Chama cha Albino Mkoa wa Shinyanga kwamba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inawafanyia majaribio walemavu wa ngozi na kwamba majaribio hayo
  yanaweza kuwasababishia madhara makubwa vikiwemo vifo.

  Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Ernest Kimaya ilisema kuwa chama kina msemaji wake mkuu ambaye ni yeye na kwamba taarifa zilizotolewa na viongozi wa Shinyanga sio msimamo wa chama cha Albino Tanzania.

  "Chama kimefanya kazi kubwa kukaa na wizara kujadili upatikanaji wa mafuta ya kulainisha ngozi na kuzuia mionzi ya jua, hatimaye wizara ilikubali na kuanza utaratibu huo mwaka 2010 mwishoni," ilisema.

  Ilieleza kuwa wizara iliwapatia mafuta hayo na chama kuyapeleka kwa mtaalam ambaye ni mshauri juu ya mafuta ya ngozi na kuwambia kwamba yanafaa na kwamba wanaweza kugawa kwa wananchi wote wa Tanzania.

  Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa zoezi hilo limeleza chama hicho kikiwa kinasoma mapungufu yaliyopo katika shughuli na mwisho kikakaa na viongozi wa wizara ili kujadili mapungufu na kujadili maboresho ya shughuli husika.

  "Kwa hiyo viongozi wa mkoa walipaswa kuleta mapendekezo yao Makao Makuu ya Chama cha Albino Tanzania, maelekezo ambayo walipewa wafanye hivyo na Katibu Mkuu na kila jambo linalofanyika katika chama lina hatua zake za kupitia hadi kufikia kuwa tamko la chama," ilieleza taarifa hiyo.

  Iliongeza kuwa matamko ya mikoani yanaweza kutolewa na Mwenyekiti wa Mkoa kwa kupata baraka kutoka Makao Makuu na kusema kuwa Chama kinaiomba serikali kuelewa na kwamba kipo nayo bega kwa bega kushirikiana kwa masuala mbalimbali kwa manufaa ya Albino wa Tanzania.

  kauli hiyo imekuja baada ya Chama cha Walemavu wa Ngozi Albino (TAS) Mkoa wa Shinyanga kusema kuwa baada ya kupokea mafuta aina ya ENAT Natural vitamin E cream kutoka nchini Australia, wamebaini kwamba yana madhara makubwa kwao na hayafai kutumiwa na albino hapa nchini.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,395
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280
  Acheni urasimu chunguzeni tuhuma na kubaini ukweli.......................................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,395
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280
  Albino walia kuathiriwa na mafuta


  na Stella Ibengwe, Shinyanga


  [​IMG] CHAMA cha watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) mkoani Shinyanga kimesema mafuta aina ya ENAT Vitamin "E"Crime wanayopaka kwa ajili ya kujikinga na mionzi ya jua yanawaathiri.
  Hayo yalielezwa jana na mwenyekiti wa chama hicho, Eunice Manumbu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ambapo aliitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iwe inafanya utafiti wa kina kabla ya kuwapatia mafuta ya kupaka.
  Manumbu alisema mafuta hayo wakiyapaka ngozi zinavimba, hivyo serikali kupitia wizara husika ni vema iwe inafanya uchunguzi juu ya mafuta ya ngozi wanayoyatumia kabla ya kuyasambaza.
  "Mafuta ambayo yameshaonyesha madhara ni aina ya ENAT Vitamin "E"Crime yanayotolewa na kampuni ya MEGA Life Services PTY ya nchini Australi; tunaitaka wizara ifanye uchunguzi na suala hili lichunguzwe kwa umakini mkubwa kwani linaweza kutusababishia ugonjwa wa saratani ya ngozi.
  "Madhara ambayo yameanza kuwapata albino wenzetu yametufanya tuanze kujipaka mafuta ya ng'ombe maarufu kama samli ili kuepuka kupatwa na madhara ambayo yanatokana na mafuta hayo," alisema.
  Alisema mafuta wanayopaka ambayo hayana madhara yanauzwa sh 18,000 hadi 45,000 na hufanya kazi hadi miezi mitatu hadi sita.
   
Loading...