Tetesi: TARURA MWANZA: Huu ni wizi, mkaliangalie hili haraka sana

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
6,311
10,353
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri,

Kwanza kabisa mimi na raia mwema na sina nia ya kukwepa ushuru wa tarura tena ukizangitia fees zao ni ndogo sana kwa sasa (reasonable).

Niendelee, leo nimeangalia ushuru wa maegesho kwenye website ya TARURA nakukuta nadaiwa nilipoangalia maelezo ya Tiketi nimekuta tiketi ni ya tarehe 10.12.2022 siku ambayo sikutoka nyumbani kabisa na nina ushahidi hakuna mtu aliyetoka na hii gari maana nimefunga GPS na hii siku kwenye database gari haikutembea kabisa!

Kwenu Tarura Mwanza Gari ambayo imepark nyumbani inawezaje kutozwa ushuru wa parking ?

Je, mnacontrol gani kwa watoza ushuru wenu wasiweze kutoza kiholela kwasababu wale ni mawakala mnatumia mfumo gani kuhakikasha hizi claim ni sahihi na mawakala hawachakachui ili kuonekana ushuru ni mkubwa ili hali ni wakubambikia?

Naweza kufikisha malalmiko yangu wapi kwa urahisi na nikasikilizwa? Ni ujinga kutumia mafuta ya ya 6000 kwaajili ya kwenda kulalamikia tozo ya 500, wanahotline ya malalmiko? Inapokelewa na changamoto zinatatulika au watanilipa usumbufu?

Mdau wa JF Karibu kama ulishawahi kukutwa na hili na ulifanya nini kulitatua?

Kama kuna mtu wa Tarura huku na unania ya kufuatilia hili zaidi karibu pm nitakupa maelezo zaidi.
 
Kuna mmoja nishawahi nusurika kumkamua makofi,mtu nimepaki ili nichukue bidhaa Kwa shop Fulani narudi nakuta minyororo kwenye tyre😃😃 ebana ee moto uliwaka
 
Nimesema hapo hawa ni wesiii
Watakupotezea mda wako bureeeee
Wakaliangalie hili, ila kwa sasa lazima niende kufuatilia aliyepiga picha hilo gari ni nani na ana ushahidi upi isikute ameweka number kwenye notebook akiwa Bar anatoza ushuru tu
 
Mimi nimekuta deni la elfu 50 tokea May 2023, halafu gari imemulikwa Uhuru St na Lumumba ambapo kwa mwezi huo hadi leo sijawahi kupaki maeneo hayo.

Kuna siku nlimkuta dada mmoja anagombezwa maeneo ya kirumba kwa upole nkamfata nikamwambia usiwasikilize hao wewe umetumwa kwanini hawajae da kwa viongozi wako wakalalamike? Yule dada alishusha jazba akase.a wangenipiga, mimi kosa langu nini? Ingekua yule mwen,angu ambae ananakili namba za magari yanayotembea akitulia anayaandikia madeni ingekuaje?

Kuna wizi mkubwa sana unaendelea TARURA - MWANZA. wanabambikia watu fine ni kama sales officer wanavyopewa target. Na vidada vya watu maskini ukimpa 500 hakuandikii ng'o.
 
Hukumuuliza anaetoa hayo maagizo ni nani mkuu
 
Back
Top Bottom