TARURA na madeni yake ni upele unaokaribia kuiva

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
9,019
21,913
Ukiachana na songo songo la kariakoo, na jipu uchungu la TRA. Kuna upele wa tarura ambao kuna kipindi uliwasha ukapata wakunaji. Wakunaji wakawai kuuzima kwa kusema mchakato wao wa kukusanya fedha na kutambua madeni kweli una kasoro.

Nazungumzia ulipaji na uvunaji wa malipo kupitia parking za vyombo vya moto/ usafirishaji hasa magari, bajaji.

Ni kweli TARURA wamefanya makubwa katika mageuzi ya barabara. Tunaona maboresho bora na mitaa ikiachwa katika sura nzuri.

Lakini katika namna ya kuhakikisha wanapata pesa za kufanya mageuzi ya barabara wamebuni njia ya kutoza gari ushuru wa kupaki.

Changamoto zinajitokeza,

•Hawaonekani maeneo yao ya kukuza mapato yanapojaa maji,tena misimu ya mvua ata kusogea hawataki, hawafanyi usafi wanajua kukatisha parking tuu

•Tarura wao wanajua kuvuna tu pesa hawataki kuja na ubunifu wa kutengeneza maeneo. Unatafuta eneo lako kwa ajili ya biashara mpya eneo ni tupu ukianza biashara likaanza kupata magari unashangaa mtu anafika kwa ajili ya kukatisha tiketi.

•Wakatisha tiketi ili kuongeza nguvu na kufikia malengo waliyowekewa ya kukasanya zaidi. Wamekuja na mbinu mpya wanapiga picha namba za gari wanashea kwa wakatishaji wenzao kupitia simu zao za kawaida. Hivyo inakua kama vile mtu amescan gari kupitia mashine yao ya parking. Mfano wa kariakoo shimoni anatuma kwa wa karume/ilala

Changamoto mtu unakuta na madeni mengine huna taarifa nayo. Ambapo siku task force ya madeni ya tarura ikiingia barabara kutaleta taharuki na mvurugano.

Nini kifanyike. Tarura waboreshe maeneo wanayochukua pesa kupitia maegesho ya magari. Wabuni pia maeneo yao makubwa kwa ajili kuongeza wigo wa parking

Pia wanaweza kuja na namna kila gari unalipia kiasi fulani kwa mwaka mzima kwa ajili ya parking. Mwenye gari unapewa sticker kuonesha umefanya malipo ya parking kwa chombo chako cha moto. Mfano kwa gari mpya kabla ya kupewa usajili unailipia pia moja kwa moja na parking fee yake ya mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom