Massbizle
Member
- Apr 22, 2013
- 49
- 5
TARURA wamefanya kazi nzuri kukarabati barabara za kiwango cha changarawe lakini wameshindwa kudhibiti watu wanaojiwekea matuta katika maeneo yao. Kila mtu anauwezo wa kiweka tuta sehemu yake kwa kisingizio cha vumbi au kusema wanadhibiti speed za magari na pikipiki. Huu ni uharibifu wa wazi wa barabara ambazo zimegharimu fedha nyingi za walipakodi. Mamlaka husika tazameni hili. TARURA wanafanya kazi nzuri ila hili litawachafua kwa mfano Tarime mjini hiitabia ni kero kila mtu aliye karibu na barabara akiamua anaweka tuta kwake tena anweza kuweka hata matuta mawili mwanzo na mwidho wa nyumba yake. Pia barabara inayoekekea Bunchari kupita Nyandoto TARURA mmeitengeneza vizuri kwa kiwangu kizuri cha changarawe ila imewekwa matuta kibao.