Tarehe 25-sept-18 siku ya jumanne Polisi walipokea Amri toka kwa Dalali wa madini anayeitwa MZUNGU mwenye ukaribu na Polisi kwa njia za Rushwa, anatumia pesa kupora madini ya wachimbaji wadogo wadogo huko Tarime, huvamia migodi akiwatumia Polisi kuwabambikia kesi wenye migodi kisha huenda kuchimba dhahabu kwa msaada wa Polisi pindi mmliki wa mgodi akiwa jela, Rais magufuli akiwa Huko mkoani mara alipiga marufuku Polisi kutumiwa na wafanyabiashara kuwaonea Raia lakini inaelekea wamepuuza maagizo yake wameendelea kuwanyanyasa wananchi kwa Amri za wenye pesa, kwa kifupi huko wilayani Tarime bado ni kisiwani kisheria kwani kuna idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu waliobambikiwa kesi kwa njia haramu kukomolewa ama kutengeneza mazingira ya kupata Rushwa, tunamuomba IGP awafukuze kazi RPC na OCD ambao wamekuwa wakimtukuza Mzungu ambaye anawatesa wachimbaji wadogo wadogo kila kukicha.