A B Sefu
Member
- Nov 15, 2021
- 9
- 4
📍Tarime, Mara
Kwa mara ya kwanza katika Historia, Tarime Community Network Cooperative Society Ltd kwa kushirikiana na Tanzania Community Networks Polytechnic College na wadau wengine vilifanikisha Kongamano la Tano la Shule za Mitandao Jamii Tanzania lenye lengo la kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kufanikisha huduma bora za Mawasiliano maeneo ya vijijini.
Kongamano hili limefanikiwa kwa jitihada za Mwenyekiti wetu Bw. Nsiko Gamisi ambaye alisimama imara kuratibu na kupangilia vyema Kongamano hilo ambalo limewakutanisha washiriki zaidi ya 50 kutoka Dar es Salaam, Dodoma, Kondoa, Nyasa, Kasulu, Tarime na kutoka Nchini Kenya. Hakika watu walikula na kucheza ngoma za asili bila wasiwasi wowote kwa sababu ya maandalizi mema.
Tunawashukuru wafadhili wetu Tanzania Community Networks Company Ltd na Universal Communications Service Access Fund kwa namna ambavyo wameendelea kutushika mkono katika kufanikisha Kongamano hili. Tukutane tena Mwakani Mkoani Dodoma.