Taratibu za mtu kufukuzwa kazi

-live Wire

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
375
190
Habari za asubuhi wakubwa,

Nimekua nikiskia wafanyakazi wengi walilalamika kusimamishwa kazi na hata wengine kufukuzwa au kukatishwa mikataba yao pasipo kuisha Kwa mda wake na bila kufuata Mtindo wa notisi yaani taarifa kabla

Ningependa kujua ni stahiki Zipi mwajiriwa anaeza kupata endapo kama atakua amefukuzwa kazi au kusimamishwa kazi Kwa muda usio julikana hasa katika Nyanja za utoro na je taratibu zinazo ambatana na mtu kusimamishwa kazi ni zipi?na endapo mfanya kazi atafukuzwa Kwa Nyanja ambaxo hazihusiani na upotevu wa fedha atalipwa mafao?

Naomba kuwasilisha .
 
Wajuvi wa sheria za kazi watakuja kuelezea hili.Ila ni vizuri mfanyakazi kufahamu nadharia rahisi kuwa MSHAHARA WAKO WA MWEZI ulioupata ndiyo pensheni yako,lolote baya laweza kukutokea ukaacha pensheni ya kustaafu.
 
Kabla ya yote kamati maalum inaundwa kuchunguza makosa yako. Hiyo kamati ni lazima iwe na mwakilishi kutoka Chama cha wafanyakazi. Kamati ikishabaini kosa inatoa mapendekezo kamati ya nidhamu. Kamati ya nidhamu itakuandikia barua yenye mashtaka ( charges) yako. Kama ni mtumishi wa serikali, kamati hiyo inakuwa na wajumbe mbali mbali pamoja na mwakilishi kutoka ofisi ya AG. Pia itakuwa na mwakilishi kutoka Chama cha wafanyakazi. Pia unaruhusiwa kuteua mfanyakazi yeyote hususani kutoka Chama cha wafanyakazi akusaidie katika utetezi( hapa unaweza kuteua idadi ya kuanzia 1 hadi 3 kama sikosei). Kamati ya nidhamu itasikiliza shauri lako na ushahidi uliotolewa kisha kutoa mapendekezo ya adhabu.

Iwapo hizi taratibu zitakiukwa, basi adhabu itakuwa batili hata kama mfanyakazi ana makosa kweli. Kinachotakiwa ni kukata rufaa katika mahakama za kazi kwa kuanzia na Arbitration na mediation.
 
Kiufupi ndio hivi labda atueleze yeye ana tatizo gani ndio tutampatia ushauri wa kisheria kulingana na hilo tatizo lake
 
Ainisha tukio moja, ni kufukuzwa kazi, au kusimamishwa kazi, na uanishe na kosa lenyewe
Hapo tayari nime ainisha poa soma tu vizuri ,kusimamishwa stahiki zake na kufukuzwa taratibu zake na stahiki zake ikiwa mtu kafuluzwa cuz of utoro.
 
Tatizo la Jamaa ni kwamba haja kuwepo kazini siku 28....bila taarifa Kwa mwajiri na alipo rudi kazini mshahara ulikua ushafungwa hivo ukafunguliwa na akapata mshahara wa ule mwezi alipo rudi ambapo akienda kazini kama siku tano ndo mshahara ukatoka na akapata but the same month ndo aka pokea sheet charges ya kumsimamisha kazi for unknown period na hakutakiwa kua mbali na kituo chake cha kazi ...Alijibu zile charges na mwezi uliofuata hali pewa chochote japo yupo kazini na sheet charges zinaeleza kua atakua akipokea nusu mshahara ....je hapo kutakua na tatizo gani na endapo kama atafukuzwa itakua ni haki wakati hakuwahi pewa hata onyo au hata wenyewe walio MPA charges na kushindwa kutimiza ahadi yao ya nusu mshahara ndani ya charges haitokua kosa Kwa upande wao?
 
Kuna makosa ambayo ukiyafanya unapewa summary dismissal papo hapo hamna cha kamati wala nini. Kwa mfano kuiba etc. Hilo la kutokuwepo kazini kwa siku 28 mfululizo ni absconding na pia unafutwa kazi mara moja kisheria.
 
Suala hilo limeegemea katika Sheria ya Ajira na Uhusiano kazini(Employment and Labour Relations Act No.06 of 2004) na pia sheria ya Labour Institutions Act No.07 of 2004 vilevile na sheria ya Employment and Labour Relations( Code of Good practice )Rules GN. No.42 of 2007.Hivyo kwa kuzingatia tatizo hilo kwa mujibu wa sheria hiyo ya kwanza No.06,sababu ambazo zinaweza kufanya muajiriwa afukuzwe kazini ni kufanys kosa ambalo ni kinyume na makubaliano ya kimkataba(misconduct),kosa hilo linaweza kuwa wizi,ama kufanya kazi kinyume na maagizo au kufanya kazi chini ya kiwango(work below the skills/standard), ama kufanya kosa lolote ambalo sheria hizo hapo juu zinamruhusu kumfukuza kazi(lakini kwa kuzingatia utaratibu wa kumfukuza kazi).Vilevile jambo la muhim hapa ni kuwa hatakama muajiriwa amefanya makosa hayo kiasi ambacho sheria insmruhusu kumtengua ajira bado muajiriwa atalazimika kuthibitisha makosa hayo kwa kumpa notisi ya kumuita na ampe haki ya kumsikiliza utetezi wake.Vile vile muajiri anaweza kumfukuza kazi au kumtengua kweny ajira bila hata ya kufanya kosa lakini katika mazingira kama; rudundancy operation(hali ya kupunguza wafanyakazi kenye eneo la kazi kwa kuzingatia cheo na idadi), au endapo mfanyakazi ameugua kwa mda mrefu sana kiasi ambacho kutokuwepo kwake kazini kunapelekea kuyumba kwa ufanisi na mchakato mzima wa uzalishaji mali,ingawaje haya yote laxima muajiri afuate taratibu maalum kwamfano suala la kutaka kupinguza wafanya kazi(redundany) ni lazima afanye haya:
1) kumpa notisi muajiriwa huyo ya kumjulisha kuhusu kuondolewa kazini
2) kumpa sababu za msingi kwanini anamuondoa kazini
3)kumpa nafasi ya kujiandaa kutafuta ajira nyingine kwa kumpa mda maalum na wakutosha.
4) na kuzingatia mkataba unasema nini juu ya matokeo ya kufanya redundancy.
Hivyo ikumbukwe kuwa muajiri akishindwa kufuata utaratibu wa kumuondoa kazini muajiriwa mahakama au bodi yoyote inayohusika na kusuluhisha migogoro ya wafanyakazi inaweza kumuamuru musjiri haya:
1)kumrudisha kaxini muajiriwa na kumlipa fidia ya pesa ya mshahara wa miezi 12,au kumlipa malipo yote aliostahiki kulipwa kwa kuhesabu tangu siku anafukuzwa mpaka amri inatolewa na mahakama/bodi.
2)kumlipa tu fidia ya mshahara wa miezi 12.
Kumlipa fidia ya mshahara wa miezi 12 na kubadilisha vipengele vya mkataba.
 
Nimekupata sana Mkuu shukrani ....
 
Nilitaka nijue maana ya neno" bila taarifa" linapotumika katika mambo ya kiutumishi. Ina maana nikiandika barua na ikafuata taratibu zote, hiyo ni taarifa au siyo taarifa!!! Mfano, nakuandikia barua kuwa muda wowote naweza kutekwa kwangu, na kesho kweli nikatekwa! Then nisionekane miaka mitatu, nikirudi mwajiri utasema huna taarifa?
 
Back
Top Bottom