Taratibu za Kinyamwezi

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
18,114
Reaction score
28,014
Wadau mwenye kulijua hili anisaidie,kuna dada nilizaa nae kabla sijafunga ndoa sasa mtoto amefikisha umri ambapo tumekubaliana nimchukue baaada ya kufuata taratibu zote za ustawi wa jamii,hatua iliobakia ni kwenda kwa bibi wa mtoto kwani ndio nimeambiwa mwenye ridhaa ya huyo mtoto,ninachoomba hapa mwenye kujua mila hizo za kinyamwezi mambo yanakuwaje pale(utaratibu) au nitahitajika kufanya nini?
 

Mahitaji yote yame base kwenye fedha kama fedha iko watakachosema utawapa na inategemea zaidi na imani yao kama wakristo au waislam na kama hawana dini pia matambiko hakuna kwa sababu huyo ni mwanao na baba ndiyo mwenye nguvu hasa kimila kwa hiyo usihofu nenda kifua mbele na fedha zako mwanao utamchukua tu.
 
Kaunga Ilumbu Lyane,

Ni kweli nina kamwanga kidogo ila si kakubwa.

Kuna kijana alikuwa anataka kuowa kwetu ila akataka kuwahusisha ndugu upande wa Baba wakati yeye alikuzwa kwa upande wa Mama. Maadamu baba yake alikuwa hajawahi kufika kwetu RASMI kuhusu kuhusu watoto zaidi ya kuwapitia na kuwaona tu, ilibidi taratibu zitumike.

Kilichofanyika ni kama walikuja kutoa POSA kwa ajili ya dada yetu ingawa dada mwenyewe alishafariki. Posa ilipokubaliwa na kupokelewa, jamaa akawa kama MUME halali kwenye familia na anatambulika RASMI. Kutoka hapo akawa Baba anayefahamika kwa upande wa mama official na kwenye harusi ya kijana, baba yake Mzazi akasimama kama Baba Mzazi kweli na si wa kusemwa pembeni.

Kijana mwingine na yeye alipotaka kuoa, utaratibu huo ulitumika kwa Baba kuja Rasmi kwa ndugu wa Mama mtu na kutoa POSA ya mtoto na hapo akawa BABA rasmi na kwenye harusi akawekwa High Table kama baba Mzazi maana vinginevyo ni wajomba tu wangelikaa na yeye asingeruhusiwa kuwa pale high table na sana sana kwa huruma kama Mgeni mualikwa.

Hivyo kwa ufupi, nenda na WAZEE nyumbani kwa huyo Mama na ukajitambulishe na kumtolea Posa huyo Mwanao. Ila mjulishe Bibi ya huyo mtoto mapema malengo ya nyie kwenda hapo kwake ili na yeye ajikusanye na ndugu zake/Marafiki na wawajadili kuhusu KULIPA FAINI ya Kum-mimba mtoto wa Kinyamwezi na kumuacha na Mtumbo wake - SHENZI sana shemeji weee....... πŸ™‚

Nategemea itakusaidia hii habari kwa ufupi. Kama vipi uliza zaidi ntajitahidi kukupa maelezo kwa uelewa wangu.
Ngoja nikuitie Sikonge aje, lakini ukiwa mvumilivu jioni nitamuuliza mama na kukuletea majibu.
 
Mtu hujafuata taratibu tangu mwanzo.

Halafu unaendelea kutofuata taratibu kwa kutafuta taratibu kutoka sehemu isiyo na utaratibu wa kuheshimu taratibu.

Akija muhuni na kukuchuuza hapa utajuaje?

Wewe humjui mnyamwezi hata mmoja anayeheshimika?
 
Ndugu yangu mtoa mada fuata ushauri wa Kiranga hapo juu,una kila kitu.
'
Ni vigumu kupata taratibu kwa wasiokua na taratibu wala hawana utaratibu wa kupata taratibu ili wapate utaratibu wa kujua taratibu!
 
Last edited by a moderator:
Kwani mie SIHESHIMIKI? Kaunga , unamuona Kiranga anasema sisi si Wanyamwezi wa heshima?

Halafu Kiranga, tupe heshima yetu Wanyamwezi kwa kutuandika kwa kuanzia herufi kubwa, Mnyamwezi.

Utaratibu nilioandika ndiyo unatumika kwa Wanyamwezi..... Ahhh, Mnyamwezi alishaMJUA mmoja na akampa Mimba.
Mtu hujafuata taratibu tangu mwanzo.

Halafu unaendelea kutofuata taratibu kwa kutafuta taratibu kutoka sehemu isiyo na utaratibu wa kuheshimu taratibu.

Akija muhuni na kukuchuuza hapa utajuaje?

Wewe humjui mnyamwezi hata mmoja anayeheshimika?
 
Asante sana mkuu umenipa mwanga.
 

Mtu mwenyewe ushaanza kwa kujisema hujui kitu kikubwa.

Ni kweli nina kamwanga kidogo ila si kakubwa.

Kwa nini mtu yeyote afuate ushauri wako.

Kisha mie Kiranga ChaNgeda Sakala Kandumbwa bin Pazi Akihito Pope of Unorthodoxy mtemi wa Uzaramo mtani wa jadi wa Unyanyembe Alwatan wa Mzizima tangu Magogoni nyumba ya saa Mchafukoge mpaka Mwembetogwa na kuvuka Msimbazi Magomeni.

Naweza kuandika wanyaMweZiiiiii ninavyotaka.Nawajua wa kuanzia Urambo, Nzega,Sikonge mpaka Kinyasini. Weusi kwa weupe.

Si tuko katika mambo ya utamaduni na mila hapa?

Wanyamwezi watani zangu mie.
 

Mkuu, naunga mkono maelezo yako naamini hayo ndiyo yatakayo msaidia.
 
Kama kweli wee Mzaramo, basi ni RUKSHA kuandika na kutukana utakavyo na sisi tutasubiri tu siku moja tukubane sehemu nzuri na tukuminye kama Mjusi aliyebanwa Mlangoni hadi upige unyende......

Kwa leo ngoja nikuache uwe mshindi maana Mzaramo ukimvamia kichwa kichwa, atakuacha hoi kwa maneno πŸ™‚

Nice to know kumbe wee ni Chakula yangu, heheheheeee....... Nawapenda woote watani Wangu.
 
Ngoja nikuitie Sikonge aje, lakini ukiwa mvumilivu jioni nitamuuliza mama na kukuletea majibu.
Hivi kaunga pale sikonge mtu akiwa anaenda chabutwa bado tu anakutana na yale ma bwawa madogo dogo na mito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…