Tapeli amemuibia simu mke wangu na kulaghai watu

Tapeli amemuibia simu mke wangu na kulaghai watu

Hata mimi ishanitokea mwizi aliendelea kutumia majina ya kwenye simu yangu kuwapiga mizinga
Pole ila ulichukua hatua gani au ulimuacha tu aendelee kupiga mizinga
 
mobakha,
Pole sana mkuu,
Hatua ya kuchukua ni kama ingewezekana kupata contacts zote za kwenye simu iliyoibiwa na kuandika sms moja ya kuwaonya kuhusu huyo mwizi na kuiforwad kwa hizo contacts zote
shukran sana, inawezekana japo si asilimia zote kwa sababu contacts zilisaviwa kwenye email, zile za karibuni sana hazikuweza kujisakronize
 
Umesema kweli. Bado narudia tena. Tatizo ni lile lile. Watanzania wengi hawako makini kabisa. Hili ni kwa mambo yote wanayofanya kila siku. Kuanzia kuandika mpaka kufanya kazi. Sim card yoyote inakuwa na pin number. Ukizima simu wakati wa kuwasha ni lazima ikuambia uingize pin number na ukikosea mara tatu ina-block. Vile vile simu zinakuwa na password. Mwizi akiiba simu yako kama ina passcode atapata shida kuona contacts bila kutumia muda na utaalam. Tena simu kama Iphone ndiyo kabisa bila kujua passcode simu ni kama haina kazi.
Ni sawa unavyosema ila mtu huangalia kilichobora kwake maana kwa upande wangu Pin number si user friendly, so huwa na prefer password kuliko. Ilikua ni Samsung, ilikua na password zake tena mbili mbili ila simcard ilikua haina pin namba. nahisi alichofanya yeye si kutumia line ila alitumia contacts za simu na maelezo mengine kwa mfano sms na ndio maana iliibiwa jumatatu kuanzia Ijumaa ndio akaanza utapeli. So inaelekea aliitoa password kwa njia za kitaalam. maana hata nikiingalia kwenye google naikuta iko offline
 
Hivi SIM pin kazi yake nini..?

Au

Phone password/Pattern/Fingerprint kazi yake ni nini..?!

Yaani tuseme hizo features za kiusalama watu hawajui kuzitumia... au ni uvivu tu..!?

Mtu anakuibiaje simu halafu akaweza kutumia 'laini' yako..?!

Yaani hata kuwajulisha mtandao husika waifunge pia nayo ni kazi..?!

Aisee...!!!
Sijasema anatumia line yangu istoshe mimi binafsi nishatumia sana simu, mke wangu nae pia ameshatumia sana simu na ni mtu amemaliza Degree, simu ina password mbili mbili. ila siku hizi password inakua sio ishu tena.
ao mitandao husika ndio hawafai hasa maana niliwauliza nichukue hatua gani wamenipa maelezo nilipoenda ofisini kwao wananiambia vyengine. mpaka nimekata tamaa kumfatilia
 
mobakha,
Pole sana mkuu,
Hatua ya kuchukua ni kama ingewezekana kupata contacts zote za kwenye simu iliyoibiwa na kuandika sms moja ya kuwaonya kuhusu huyo mwizi na kuiforwad kwa hizo contacts zote
Shukrana, asante kwa wazo lako uwezekano upo wakupata contacts maana zimesaviwa kwenye email
 
Mbona ni rahisi kumpata kama utatoa taarifa polisi ili wamtafute
Polisi nimefika mkuu ila ushauri walionipa umenivunja moyo japo kua nina hamu ya kumjua mwizi
 
Nje ya mada Mkuu

Mke wako aliibiwa akiwa nyumban kwake ...una maana IPI kwao kwa wazaz wake au ananyumba yake na wewe unakwako fafanua ndio nikushauri naona kuna kitu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
nyumba ni yangu na tunaishi pamoja, ninavojua mimi nyumba yako ni ya mkeo pia. so nikisema nyumbani kwake kwa utamaduni wetu huwa sijakosea.
 
Back
Top Bottom