Tanzon CAR

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,530
13,467
Wana JF, hivi ni lini Tanzania itakuwa na uwezo wa kumanufacture its own car? Tatizo ni nini?, Malighafi, Wataalamu, Uwezo wa kifedha, Mipango mibovu, Nia au kutokuwa na ndoto kama wenzetu walivyo na ndoto?
 
We unawaza magari tu, Barabara ziko wapi???

Uliza lini tutaanza kuweka fly overs kwanza na kuboresha infrastructure.

Umeme wenyewe ishu, nani atawekeza kiwanda hapa.!!!!
 
Barabara tatizo lake ni political will tu. Lakini kumamufacture Magari it is more than that, that is what l think. Nilisikia Uganda wana hiyo project! Nyumbu ya TZ tulikwama wapi?
 
Barabara tatizo lake ni political will tu. Lakini kumamufacture Magari it is more than that, that is what l think. Nilisikia Uganda wana hiyo project! Nyumbu ya TZ tulikwama wapi?

Hapo ndio ulitakiwa uanzie swali lako.

Kabla ya kutengeneza hilo gari unatakiwa ujue mambo kadhaa:
1. unalenga soko lipi?
2. kuna nani wengine wanaocheza kwenye soko hhilohilo?
3. wanafanya vizuri kiasi gani au vibaya kwenye hilo soko?
4.gari lako la mwisho kutengenezwa Nyumbu bei yake ilikuwaje ikilinganishwa na magari yenye sifa na uwezo sawa na la kwako kutoka kwa watakaokuwa washindani wako?
5. unaweza vipi kushusha gharama za uzalishaji ili uweze kuuza kwa bei ya kiushindani?

Hayo ni baadhi tu maswali unayotakiwa kuyapatia majibu, lakini utaona kuwa katika gharama za uzalishaji, umeme bado ni kikwazo kikubwa kwani ni ghali mno ukilinganisha na nchi zilizo nyingi na bado sio wa kuaminika. Hii ni moja ya sababu kubwa kiwanda cha karatasi Mgololo kilishindwa kufanya vizuri na hatimaye kukosa hata bei kilipokuwa kinaelekea kufa pamoja na kuwa soko la karatasi hapa nchini ni kubwa sana.

Kimsingi kuna bidhaa nyingi sana ambazo ni mahitaji ya msingi na zenye demand kubwa kama karatasi, nguo, mafuta ya kula, building materials n.k. tunatakiwa tumudu kuzalisha hapa nchini kwa viwango vya kimataifa na bei za kiushindani ndipo tupate jeuri ya kufikiria kutengeneza magari.

Ni swala la kujenga uwezo na uzoefu hatua kwa hatua.
 
Back
Top Bottom