Kwa wale wapenzi wa muziki wa Injili watakuwa wanaifahamu vizuri sana Kwaya ya Lulu ya KKKT Mtoni kule Temeke, hii ni moja ya Kwaya zilizodumu katika huduma hii kwa muda mrefu sana bila kuteteleka, moja ya nyimbo zao ni huu wa " lulu iko mbinguni"
Jana kwaya hii pamoja na wapenzi wote wa muziki wa injili tumepata pigo kwa kufiwa na mmoja wa Waimbaji wao mahiri ndugu George. Msiba uko Tabata Bima nyumbani kwake. George ametangulia, kapumzike kwa amani baada ya kuumaliza mwendo. Poleni kwaya ya Lulu,Washarika wote wa Mtoni na Watanzania wote kwa ujumla.
Ikimpendeza Mungu tuje tuimbe sote HALELUYA KUU huko kwa Baba.
RIP George.