TANZIA: Mzee Patrick Qorro (aliyewahi kuwa Mbunge wa Karatu) afariki dunia

Mzee Patrick Qorro. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Tutakukumbuka kwa mengi uliyoyafanya wakati wa Uhami wako. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe. Amina!
 
Asante Kwa Kuniita Pimbi na Unaweza Ukaendelea tu Kunitusi Utakavyo ila Nilichomaanisha Ni Kwamba Alifanyiwa Matibabu Ya Aina Mbili Ya Kwanza ni Kuondoa Damu iliyokuwa Imeingia ktk Ubongo Wake na Baadae Pia Akafanyiwa hiyo Oparesheni Ya Mapafu Yake. Taarifa Kamili Ndiyo Hiyo na Kama Kuna Mahala Nimekuchanganya au Nimekosea Niwie Sana Radhi Kwani Yawezekana Pia Nimechanganyikiwa na Taarifa Za Msiba Wake Kwani Kwangu alikuwa ni Baba Wa Mfano wa Kuigwa na Mwanasiasa Mnyenyekevu, Muungwana, Mwenye Upeo wa Kuona Mbali na Mshauri Mzuri Sana Wa Maisha na Binafsi Nimejifunza na Nimefaidika na Mengi Sana Ya Kiushauri Kutoka Kwa Mzee Patrick Qorro na Nadiriki Kusema Kuwa hata Mafanikio Yangu na Maisha Yangu Kiujumla hadi hapa Nilipofikia ana Asilimia Zake 25. Nitamkumbuka Sana Mzee Qorro Tokea Akiwa Anaishi Kinondoni Karibu na Ubalozi wa India, Kisha Akahamia Chuo Kikuu Mlimani Mtaa wa Kaloleni na Hadi Alipohamia ktk Nyumba Yake hapo Ada Estate. RIP Uncle Patrick Qorro NITAKUKUMBUKA na KUKULILIA DAIMA.

Mtaa unaitwa KILELENI sio KALOLENI. Ny mpe pole sana pandi mdau
 
..r.i.p Mzee Patrick Sylverius Qorro[koro].

..kama sijakosea aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa vijana TANU, na waziri mdogo ktk serikali ya Mwalimu Nyerere.

..baadaye alipata kutumikia kama Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Breweries, na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kiwanda cha Sigara. wakati huo mashirika hayo yalikuwa mali ya umma.

..alikuwa mtu muadilifu sana, mchapakazi, kiongozi mfuatiliaji na results oriented, aliyeheshimu wakubwa na wadogo.

..aliyaacha mashirika ya breweries na sigara yakiwa ktk afya nzuri, kwa maana ya uzalishaji, mafao na nafasi za kujiendeleza kwa wafanyakazi. moja ya miradi ninayoikumbuka kuachwa na Mzee Qorro pale breweries ni zile nyumba za wafanyakazi pale Buguruni.

..Patrick Qorro alikuwa mtu aliyependa kujiendeleza kielimu. alichukua shahada ya MBA pale udsm akiwa tayari ni mwenyekiti mtendaji wa Tanzania Breweries.

..zaidi ya hayo alikuwa kiongozi mpenda MICHEZO. wakati wa uongozi wake timu za mpira wa miguu za Breweries na Sigara zilipanda daraja na kucheza ktk ligi kuu. kama mtakumbuka enzi za akina Jamhuri Kihwelu, Yassin Abuu Napili, etc etc.

..bungeni alikuwa ni mbunge mwenye msimamo usioyumba ktk kutetea maslahi ya nchi. namkumbuka akiwa mbunge aliandika hoja binafsi kupinga uchafuzi wa mazingira ktk mbuga zetu za wanyama.

..nje ya majukumu yake ya kiserikali na kisiasa, Mzee Qorro alikuwa mtu mwuungana, mnyenyekevu, na mwenye msaada kwa wenzake.

NB:

..kama sijakosea Mzee Patrick Qorro aliwahi kuomba radhi kwa wapiga kura wa Karatu kutokana na kauli tata aliyoitoa ktk mkutano wa kampeni ambao ulihudhuriwa na makamu wa raisi Dr.Omar Ali Juma[r.i.p].
 
Namfahamu nawapa pole wafiwa. Huyu alikuwaga kwenye timu ya G55 na akina Njelu Kasaka
 
Nawapa pole sana Mama Qorro na watoto wake

inasikitisha kupoteza wazee wetu hawa,

Pole zaidi Grace maana ni juzijuzi tu ulipoteza mume... hard to take when a woman loses two special men in her life in such a short period of time
na grace alikuwa kipenzi cha babake toka zamaniiiiii, yaani she will be really in pain, rest in peace mzee qorro
 
Mzee alichangia sana ccm kuchukiwa Karatu kwa dharau aliyonayo na kauli mbovu

Yale Yale!!!!!!!!!!!!!!!! Mlikuwa Mnasubiri Afe Ndipo Mfunguke Kwa Maneno Yenu Ya Chuki na Ya Kinafiki? Bila Shaka hata Kifo chake Kwenu Sasa ni Sherehe.
 
Alikuwa mwalimu wangu shule ya msingi Kaloleni, Arusha, pole sana kwa mdogo wake mwanafunzi mwenzetu pamoja na Lowassa, Kinana,& OleNjolay aitwaye Michael Qorro pale Arusha Secondary
 
Ratiba kesho tarehe 11/2 kuanzia saa 5 hadi saa7 ni chakula then misa itasomwa nyumbani na kutoa heshima za mwisho hadi saa 9.30 alasiri, baada ya hapo wataanza safari kuelekea karatu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Habari za kusikitisha-mzee patrick qorro amefariki dunia usiku huu muhimbili. Huyu alikuwa mwanasiasa nguli, lakini alikwaa kisiki cha dk slaa.


Poleni sana, Mola ailaze Roho yake pahala panapo stahikhi.

Pole sana rafiki na classmate wangu Ilboru Bwana Joseph Masinda. Poleni wana Karatu na wana Arusha wote na waTz wapenda amani
.
 
Back
Top Bottom