Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,906
- 10,390
Taarifa zilizonifikia hivi punde zinasema kuwa msanii wa Bongo movie ameaga dunia.Ila bado habari hizi hazijawa na uhakika.
RIP mzee wetu.
============ Updates ==========
Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi nz chanzo ch kifo cha mzee wetu huyu.
Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.
Chanzo: bongomovies.com
Godfrey David Manento mtoto wa 4 wa marehemu Mzee Manento
Kutoka nyumbani kwa marehemu Mzee Manento ambaye alikuwa akiishi maeneo ya Kigogo,taratibu za mazishi bado zinaandaliwa ingawa mpaka sasa familia bado haijapanga wapi atapumzishwa Mzee Manento.
Godfrey David Manento ambaye ni mtoto wa 4 wa marehemu David Manento kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema ‘Mzee wetu alikuwa akisumbuliwa na Lishe hali hii ilianza baada ya mama yetu kufariki miaka 2 iliyopita.
‘Si kwamba alikuwa hapati chakula vyakula vilikuwepo vya kutosha lakini alikuwa anakosa mtu wa kumpa matunzo ya ndani ya nyumba kama mke kwa hiyo tangu afariki mama mzee alikuwa mpweke.
Matatizo ya mzee mbali na kuwa na umri mkubwa pia alikuwa na presha na alikuwa akisema mimi nina presha jamani baadae presha ikatengeneza kitu kama kisukari ikitokea presha inapanda na sukari inapanda baadae akawa anasema hadi miguu ina ganzi kidogo.
Mpaka mauti yanamfika tulishampeleka mara tatu hospitali na tulikuwa tukirudi,sisi kwenye familia tulikuwa 10 lakini 1 alifariki hivyo tumebaki 9,Mpaka sasa taratibu za mazishi tunaendelea kuzipanga.
Baba yetu sisi alikuwa mwenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Same maeneo ya Mamba Miamba tulikuwa tunafikiria anaweza kuzikwa nyumbani kwenye asili yetu au tumzike hapa hapa Dar es salaam.
Siku za mwisho za Mzee wetu kama alikuwa akikiona kifo kwa sababu siku zake za mwisho mwisho alikuwa akisema jamani mimi naona kama sitopona alikuwa hana wasi wasi na kifo nadhani na ule uzee alikuwa akiuona na kuona siku zake zinakaribia'.
Mzee Manento amefariki akiwa na umri wa miaka 73 na kuacha watoto 9,filamu alizocheza enzi za uhai wake ni pamoja na Hero of the church,Dar To Lagos,Fake Pastor na nyingine nyingine.
Credit: Millard Ayo