Tanzia:Mwanamziki mkongwe Shabani Dede afariki Dunia.

Tanzia:Mwanamziki mkongwe Shabani Dede afariki Dunia.

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
6,001
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_IMG_2301.JPG

MWIMBAJI mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa. Dede, mwanamuziki wa Msondo ambaye pia aling’ara na bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee na OSS, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari pamoja na figo.
Saluti5 imemnukuu Hamad Dede, mtoto wa marehemu, akisema kwamba mpendwa wao huyo amewatoka. “Baada ya kama masaa mawili tutakaa kama familia na kutoa taarifa rasmi ya msiba utakuwa wapi na mazishi ni lini ingawa kuna kuna zaidi ya asilimia 70 kuwa tutazika kesho,” alisema Hamad.

Onyesho la mwisho Dede kushiriki ni lile lililofanyika Travertine Hotel, Magomeni la mpambano wa Msondo na Sikinde Mei 20 mwaka huu.
 
God rest his soul in eternal peace; Shaaban Dede, ulipokuwa nasi ulitumia kipaji chako kutuburudisha, kutufundisha na kutuliwaza kwa sauti yako yenye mwangwi, upumzike kwa amani Dede
 
Pumzika kwa Amani! Ahsante kwa muziki wako!
 
Umekua Ni mwaka wa kuondokewa na hawa wanamziki wakongwe sijui kuna nn!!?maana huyu nadhani ni wa 4 au 5 tangu mwaka huu uanze.
 
Mwenyezi Mungu aipokee roho yake ailaze mahali pema peponi amina.
Nikikutana nae sana K/koo mitaa ya Mafia/Nyamwezi na Swahili ila kitambo kidogo sijamuona nadhani ni kwa7bu ya maradhi.
 
Back
Top Bottom