Tanzia: Muigizaji Rachel Haule afariki dunia

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,613
2,000
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho,' amefariki dunia asubuhi hii. Marehemu amepoteza maisha mara baada ya kujifungua.

Alijifungua kwa operation mtoto akafariki hapohapo,na yeye akalazwa ICU,ila leo asubuhi ndio akafariki..

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
========================================================

Rachel Haule
Akiwa mmoja wa waigizaji wa kike ndani ya bongo movies na mwenye umbo lenye mvuto. Rachel Haule ama "Recho" kama anavyofahamika na mashabiki wake ni mwigizaji aliyekuja kwenye tasnia ya filamu miaka ya karibuni na kuweza kujipatia umaarufu kupitia filamu mbalimabli alizoigiza.

Early life
Rachel alizaliwa mkoani Ruvuma kwenye wilaya ya Songea na kupata elimu yake katika Shule ya msing Luida iliyopo wilayani hukohoko Songea. Baada ya Muda alihamia Dar essalaam na kusoma shule ya sekondari ya Baptist iliyopo magomeni na baadaye kwenda kumalizia elimu yake ya sekondari katika Hanga. Baada ya hapo Rachel alijiunga na chuo cha magogoni kilichopo jijini Dar es salaam katika kujiendeleza zaidi kielimu.

Career
Historia ya Rachel katika maigizo inaanza rasmi mwaka 2009 katika kikundi cha maigizo cha mburahati. Baada ya kukaa kwenye kikundi hicho ndipo alipojiingiza rasmi kwenye uigizaji wa filamu.

Rachel mara nyingi amekuwa akizungumziwa na vyombo mbalimbali vya habari hasa kutokana na mavazi yake. Hupendelea kuvaa nguo fupi ambazo huonesha vizuri umbo lake na mara nyingi amekuwa ni kivutio kwa watu wengi anapoonekana kwenye matukio mbalimbali kwani wengi hutugemea kumuoa akiwa ndani ya nguo fupi.

Katika moja ya interviews zake Rachel aliwahi kusema kuwa hupendelea kuvaa nguo fupi kwani humfanya ajisikie huru na amani pindi anapofanya shughuli zake.

Chanzo:bongomovies
.


Shughuli za mazishi ya msanii Rachel
 

Attachments

 • Recho2.jpg
  File size
  111.6 KB
  Views
  4,244
 • rachel 1.jpg
  File size
  121.6 KB
  Views
  3,377
 • Rachel 2.jpg
  File size
  59.9 KB
  Views
  609
 • Rachel 3.jpg
  File size
  51.7 KB
  Views
  3,069
 • Rachal 6.JPG
  File size
  144.1 KB
  Views
  3,080
 • Rachel 4.jpg
  File size
  80.7 KB
  Views
  3,024
 • Rachel 5.jpg
  File size
  91.4 KB
  Views
  3,199

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,157
2,000


RECHO AFARIKI: Msanii Rachel Haule 'Recho' afariki asubuhi hii Muhimbili Hosp, Dar baada kujifungua kwa upasuaji. Mtoto alifariki jana, Bongo Movie yathibitisha

===
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Habari zilizotufikia na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.


Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita.

"Vifo hivi vya wasanii wetu, vimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo."


"Habari zaidi zitawajia baadaye..."
 

La Princesa

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
1,002
2,000
Msanii maarufu Wa filamu za kibongo maarufu Recho Haule maarufu kama Recho Wa Saguda saga dunia alfajiri ya Leo

Chanzo makini cha habari kimeeleza kuwa Recho amefariki kutokana na matatizo yaliyojitokeza wakati Wa kujifungua.

Mtoto alifariki Jana muda mfupi baada ya kuzaliwa na mama alilazwa ICU mpaka alipokumbwa na mauti alfajiri ya Leo

Safari yake duniani imekwisha iwe funzo kwetu tuliobaki kwamba duniani tunapita tu.....Amen
 

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
1,654
0
Seriously im so shocked, kwa kweli
ila kazi ya Mungu haina makosa,
Rachel ni mwanafamilia wa Bongo
Movie amefariki asubuhi kwa taarifa
zaidi tutapata kwa mwenyekiti wa
Bongo Movie Steve Nyerere ambaye
anaelekea Muhimbili sasa ambapo
mwili wa marehemu ulipo
hifadhiwa, Poleni sana wafiwa na
fans wa Rachel na Bongo Movie kwa
ujumla maana hiki ni kipindi
kigumu sana.....
RIP RACHEL HAULE


Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve
Nyerere, zimesema kuwa Recho
alikwenda Muhimbili jana kujifungua
ambapo mara baada ya kujifungua
mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa
mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU
ambako hali ilizidi kuwa mbaya na
baadae kufariki dunia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom