Nimeingia ofisi moja binafsi hapa jijini Mwanza nikiwa nahitaji kufanya shughuli fulani,ila nikaambiwa kuwa ofisi inafungwa kwa vile mufti wa Tanzania kafariki,wakasema wanafunga ofisi kufuatilia zaidi habari hizo,naomba kabla sijageuza kurudi Dar mwenye taarifa kamili atujulishe tafadhali,ili kama sio kweli niendelee kuwasubiri tukamilishe kazi yetu.
إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ Habari zilizopatikana ni kwamba Sheikh Mkuu wa Tanzania Issa Shaabani bin Simba amefariki Dunia. Taarifa zinasema Mufti Simba amefariki asubuhi hii katika Hospitali ya TMJ ya jijini Dar es Salaam. Mufti amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya sukari kwa muda mrefu. Source: ahbaabur blog