TANZIA: Mtaalamu na Nguli wa Kiswahili Mzee Makih Hassan, amefariki dunia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mtaalamu na nguli wa kiswahili Mzee Makih Hassan, ambaye ni miongoni mwa wachambuzi na waanzilishi wa kipindi cha kumepambazuka Kiswahili Radio One kinachorushwa kila Jumamosi, amefariki dunia.

=======

Mtaalamu na nguli wa lugha ya kiswahili nchini Makih Hassan ameaga dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya figo.

Marehemu Makih Hassan ambaye amejulikana kwa umahiri wake wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili katika kituo cha matangazo ya Radio One, amefariki usiku wa tarehe moja majira ya saa mbili usiku.

Wapenzi, wachambuzi na wasomi wabobozi wa lugha ya kiswahili, hakika watamkumbuka Makih Hassan kwani ndiye miongoni mwa wachambuzi waanzilishi wa kipindi cha Kumepambazuka Kiswahili Radio One, kinachorushwa siku ya Jumamosi.

FB_IMG_15464371378212388.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom