TANZIA: Mama Mzazi wa mbunge Zitto Kabwe, Shida Salum afariki Dunia

Nchi Hii tunakuja kuwa Kama Wakenya...kila kitu Siasa...Mara Chadema hawakwendaa kumuona ,...Sasa jeneza pale msikitini limetoka Haina benderaaa..
 
Chadema lazima iondolewe katika uso wa tanzania.ni lazima ifutwe imejaa watu wakatili ambao wakiachiwa wataeneza sumu.
 
akimaliza msiba tuhuma zake ziko palepale.

Chuki zako za kisiasa usiziingize kwenye misiba. Zitto nae ni binadamu anastahili kufarijiwa. Isitoshe huyo mama ni kada wa CDM inabidi tusikitike.
Iko siku na wewe yatakukuta kama haya.....
 
Tumezaliwa, Tunaishi Na Tutakufaa.

Muacheni mama apumzike kwa amani, na raha ya milele imuangazie ehe bwana.

Kuna watu wanakufa kila siku bila msaada, bendera ya chana na ndege ya serikari n.k

Kilicchofanyika wassira ni waziri na kazi yake ni anti~wapinzani, amechukua ndege ya serikar kwa makusudi, mzee ndesa ametoa ndege wakakata bendela wamekata n.k

RIP MAMA SHIDA.
 
Mwanasheria mkuu wa Chadema Ndugu Tundu Antipas Lissu amesema kuwa Zitto kuondokewa na mama ni pigo na simanzi kubwa na kudai kuwa anakumbuka jinsi alivyopata simanzi kwa kuondokewa na mama yake mzazi ambaye alimpenda sana.

Tundu Lissu pia ametoa salamu za pole kwa Zitto na familia kufuatia msiba huo limeripoti gazeti la Raia Tanzania..

Aidha Tundu Lissu pamoja na wabunge na viongozi wa Chadema wanatarajiwa kuwepo Kigoma leo kuungana na wanafamilia katika mazishi ya mama Zitto.
 
Mm nimeliona hilo ndio maana nmesema kama CDM itachukua nchi hii mm sitakuwa mtanzania ni bora niende kununua urai wa Malawi kuliko kuongozwa na watu waliojaa ubaguzi wa kikabila na kikanda.....

Chadema kama mnafikiri ipo sku mtachukua nchi hii basi nisawa na nyani anavyofikir atajenga nyumba pindi anyesheapo na mvua..

Labda muunde nchi yenu ya kichaga ndio mkaongoze na ukabila wenu na ukandawenu.
Lakin sio Tanzania hii
 
Ndugu zangu kwanza niwape pole kwa msiba Wa mama yetu shida salum mjumbe Wa baraza LA katiba siku hizi mpita njia akifa au dereva piki piki chadema wanapeleka bendera yao kufunikia jeneza

Hata mwanaccm akifa Kama ndugu zake kwaa asilimia nyingi ni chadema wanauteka msiba na jeneza kufunikwa kwa bendera ya chadema mfano ni Dada yake Mbowe liliani alikuwa mwanaccm lakini siku ya msiba Redbriged walikuja na bendera kuanzia pale kanisa LA kkkt wazo hili

Jana nimeshangazwa kwa kutoona jeneza LA mjumbe Wa kamati kuu ya chadema kutofunikwa na bendera ya chama kwani ugomvi na mtoto wake unakizuia chama kumzika kwa heshima mjumbe wao?

Chadema acheni ubaguzi uliyopitiliza kuwani na moyo Wa kibinaadamu huyu mama amekuwa chadema maisha yake yote nakukieshimu chama chake ila mmeamua kumlipa hayo

Haya nayo mabwaku ......
 
Naamini Nipashe wenyewe wamejazia maneno, eti ndege ya serikali. sijui labda flightlink ni ndege ya serikali siku hizi!!!!!!!!!!!!!!!
Nadhani tuache maji taka tuomboleze. nani ameenda msibani nani hajaenda hilo halituhusu humu, maana mwisho wa siku tutaanza "oooh waliohudhuria msiba wa mama zitto ni mafisadi na magamba si unaona jinsi walivyo karibu nae kwa uthibitisho wa ufisadi wake" Tumwache zitto amalize msiba ndiyo tumwaanzie majungu.
 
sasa mimi chadema inanihusu nini? tuhuma za zitto ziko palepale wala yeye si wa kwanza kufiwa, wanaokufa kila siku wanaacha majozi kwenye familia zao.

Asante mkuu? me mwenywe nimetoka juzi kuzika jembe langu, nimepiga konde moyo nasonga mbele, tusitumie msibaha huu kisiasa na kuzani kama kafa mungu vile ni Shida raia kama sisi.

RIP DADA SHIDA.
 
R.I.P Mama Zitto, huu ni muda wa kumfariji mwenzetu, hata kama kuna tofauti haitoshi kwa chadema kushindwa kwenda hata kiunafiki.
 
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

U mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi

Hatuna budi kuwashukuru wote waliojitokeza na kuchangia kwa hali na mali na pia wale walikuwa na familia kifikra wakati wa shughuli za msiba Dar es Salaam kabla ya kusafirisha kuelekea katika nyumba ya mapumziko ya milele.
=================================================================

Zitto_mother.jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza kwenye gari jeneza lenye mwili wa Saida Salum, mama mzazi wa Zitto tayari kuelekea uwanja wa ndege.


1.JPG

Wakazi wa jiji wakiingiza mwili wa Mama mzazi wa Zito Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Shida Salumu)katika gari tayari kwa Safari ya kuelekea Kigoma mara baada ya kuswaliwa katika msikiti wa Maamul jijini Dar es Salaam jana.Marehemu anatarajiwa kuzikwa mjini kigoma
2.JPG

Mbunge wa Musuma Vijijini Nimrod Mkono (kulia) na Mbunge wa Bunda Stephen Wasira (kushoto) wakifariji Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zito Kabwe kwa kufiwa na Mama yake Mzazi.


Picha chini zinaonyesha baadhi ya waombolezaji waliohudhuria swala ya kuswalia Marehemu Shida Salum, Mama yake Zitto Kabwe.
zito+rosatam.jpg

zitto_murtaza.jpg

shivji.JPG

zitto+wasira.jpg

MAMA1.jpg

Zitto kabwe akiwa na Prof Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi.
mama4.jpg

Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe.
mama5.jpg

Kardinali Polycarp Pengo akiwa na Rais wa TASWA, Juma Pinto akiwa VIP JKN Airport walipokutana wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe,
MAMA2.jpg

Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe, Bi Shida Salum kuingiza kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi
MAMA3.jpg

Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na mwezie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko

Dunia ni mapito.
 
nilipitapita kwenye mitandao, tv, magazeti, nigundua kuwa vyombo vingi vya habari zenye mlengo wa ccm wanatoa sana habari za zito.Hi ni nadra sana kukuta habari za wapinzani kwenye hivi vyombo. Hii inaonyesha jamaa sio mpinzani.nenda kwenye blog ya ccm millad ayo michuzi nk utathibitisha hilo

JF umeisahau, nayo ni ya uccm?
 
Back
Top Bottom