Shukurani
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 251
- 11
Dah! Mkuu kumbe nawe ni mmoja wa kipindi kile cha "Introduction to third phase cost sharing". Nakumbuka ilikuwa kivumbi pale magomeni.
hakika, Mungu amsamehe huyu mama. Nakumbuka wakati wa kujaza form za mikopo pale magomeni alimtandika vibao dada moja alikuwa akisoma UDSM hali ambayo ulizusha mtafaruku mkubwa na wazazi wa yule binti. Ilibidi vijana tuandamane mpaka kwa Makamba Boma hili kupata msaada. Mama alikuwa anatisha ile mbaya utafikiri MUNGU mtu. Alipokwenda kule Mbarali mambo nako yakawa balaa kwa wafugaji. Kwa kweli, mola wetu mwenye rehema na upendo mwingi Msamehe tu. Nijuavyo mimi mateso ya kansa ni makubwa sana, hayo tu mola yanatosha, mrehemu huyu mama