TANZIA: Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Shebuge afariki dunia

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
229
485
Karani wa Baraza la Mawaziri Hassan Ramadhani Shebuge (mara nyingi husimama pembeni mwa Rais wakati wa viapo), amefariki dunia.

Shebuge.jpg

======

Shebugee.jpg

Pichani, marehemu Hassan Shebuge akishuhudia Prof Jumanne Maghembe akila kiapo cha kuwa waziri wa maliasili na utalii mwaka 2015.

Shebuge 4.JPG

Pichani marehemu Hassan Rashid Shebuge(Kushoto) enzi za uhai wake akiwa katika banda la Utumishi wa Umma wakati wa maonesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kama Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma akiwahudumia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliotembelea banda hilo katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa.

IMG_1033.JPG
 
Daaah!
Jamaa nilikuwa sikosi kumuona tangu enzi za Balozi Ombeni akiwa CS japo sikuwahi kumuona akifanya jambo lolote zaid ya kusimama tu pembeni na mikono kakunja kwa Mbele!
Allah AMPE kauli thabiti huko Akhera!
JPM natarajia atahudhuria Msiba!
 
Inna lillah kwa mara ya kwanza nilimuona mubashara Dodoma Hazina Square , wakiwa yeye Waziri Mpango, Sam Mahela na mlinzi fulani wa mh Rais.

Jamaa very smart alikuwa anajipenda sana.
 
Back
Top Bottom