Tanzia iliyochelewa: Dkt. Edith Kitambi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,928
30,279
Nimesoma kuhusu kifo cha Dr. Edith Kitambi leo keshafariki muda mrefu na watu wameandika kama kumbukumbu.

Kwangu mimi ikawa ni msiba mpya na machungu yake naomboleza wakati wenzangu weshapoa.

Nilimfahamu Edith University of Wales Cardiff mwaka wa 1991 sote tukiwa Postgraduate Students kutoka Tanzania.

Alinizoea zaidi alipojua kuwa mimi na Ledgar Tenga aliyekuwa mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ni marafiki.

Tenga ni kaka yake.

Alikuwa bint mzuri wa tabia na sura.

Nakumbuka yeye ndiye aliyenipa jina la "Sheikh" pale Cardiff na likaniganda kiasi jina langu likafa na wanafunzi kutoka Tanzania wote wakawa wananiita, "Sheikh."

Ukisikia Sheikh basi hakuna mwengine ila mimi.

Sababu ya jina hili ni kuwa ilikuwa kila Jumamosi kuna mahali nadhani ilikuwa club wanafunzi wengi wakienda kucheza disco na kujiburudisha na vinywaji.

Cardiff ni mji mdogo sana ukifananisha na London na miji mingine ya Uingereza kama Liverpool hivyo hata sehemu za starehe si nyingi watu hukutana mahali pamoja siku zote.

Ikawa siku zinapita wanafunzi wenzangu hawanioni kujumuika na wao.

Ulaya kwa mgeni ni mahali pa upweke sana ingawa mimi nilikuwa nimeshafika Uingereza kabla na napaelewa kwa kiasi kidogo.

Siku moja Edith akaniuliza kulikoni?

Nikistarehe sana kuzungumza na Edith sababu yeye tofauti na wengine wote alikuwa akisema Kiswahili kwa "accent" ya Dar es Salaam kabisa, utasema mwanamke wa Kizaramo wa Kariakoo.

Nilipata kumuuliza imekuwaje akaniambia kuwa yeye lau ni Mchagga lakini kazaliwa na kukulia Dar-es-Salaam.

Ikawa sasa hata tukiwa na party za Watanzania 9 Desemba au Sabasaba hanioni kucheza muziki na Edith akitaka kuninyanyua kucheza namtuliza kwa kumwambia Sheikh hachezi dansi.

Yeye akiishia kucheka.

Na Edith akifanya hivi kwa kutumwa na wenzake ili wapate kucheka kwa kumuona sheikh anamwagika kwenye "dance floor."

Miaka ile kulikuwa na bendi kutoka Kenya, "Virunga," "Mazembe" ambazo miziki yake ikipendwa na kuvuma hadi Ulaya katika jumuiya za watu weusi.

Nakumbuka hawa Virunga walipata kufika Cardiff na wanafunzi kutoka Kenya wakawa wanauza tiketi za dansi.

Kulikuwa katika party zile muziki wa Judy Baucher sina hakika na hili jina yeye alikuwa na nyimbo za "blues" hizi zikiwatoa fahamu vijana wengi khasa mashairi yake ya mapenzi.

Nyimbo hizi zilikuwa lazima zipigwe.
Party za Watanzania zikinoga sana.

Vijana wa Kizungu walikuwa haziwapiti wakiwapenda sana dada zetu zaidi wanavyojua kucheza.

Ulaya ukialikwa party unakwenda na kinywaji chako.

Edith masikini akipenda kunitania nami siku zote nikimchekesha kwa kumwambia mie mzee na sheikh siwezi kucheza muziki afanye staha.

Tukazoeana sana nikawa nimepata pia daktari kidogo nikijisikia namwendea.

Edith alikuwa anafanya shahada ya pili katika Public Health.

Nakumbuka alipata kuniambia kuwa kwa tatizo nililokuwanalo la tumbo atanitibia kwa njia ya "food elimination," na akaniwekea orodha ya kutokula vyakula fulani kimoja baada ya kingine kwa muda mfupi niangalie tatizo langu kama litaendelea au la.

Nilipona.

Alipata siku moja kunipa mhadhara mzima wa ukimwi.

Akaniambia ni tabu mtu kupata ukimwi akiwa kajituliza lakini ni rahisi kuugua akiwa kinyume chake.

Akanieleza kuwa yeye katibia wagonjwa wengi na hili kaligundua kutokana na utafiti wake katika "lifestyles."

Nilimwacha Dr. Edith Kitambi Cardiff lakini nilipata kurudi tena Uingereza, London kwa muda mfupi nilimtembelea nyumbani kwake.

Baada ya hapo sikupata taarifa zake hadi leo zaidi ya miaka 30 kupita nasikia amefariki.

Nitaingia Maktaba kuangalia picha za Cardiff nikipata picha yake In Shaa Allah nitaiweka hapa.

1696539704431.png

Kulia Mwandishi na anefuatia ni Dr. Edith Kitambi
 
Pole sana Mzee kwa msiba wa rafiki yako Edith. Pia nakupongeza mno kwa kuweza kuandika uzi bila kuwataja kina Sykes wala kuingiza mambo ya kidini. Hakika mzee umeupiga mwingi.
Mama...
Wewe si wa kwanza kujaribu kuwafuta Sykes katika historia ya Waafrika wa Tanganyika na harakati za uhuru.

Unaweza kuandika historia ya vijiji vya ujamaa bila ya kumtaja Nyerere?

Jibu ni wazi kabisa haiwezekani.

Unaweza kuandika historia ya uhuru wa Kenya bila ya kuwataja Wakikuyu na Mau Mau?

Haiwezekani.

Ndivyo ilivyo kwa Sykes.

Huwezi kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika bila kuwataja Sykes.

Hapo juu ni taazia.

Sykes anaingije katika taazia ya Dr. Edith Kitambi?

Ingekuwa historia ya Wissman na Deutsch-Ostafrika na African Association na TANU ningewataja Sykes.

Hili nimeliweka mwisho kwa makusudi.

Mimi nimo katika Cambridge Journal of African History na nimo katika Dictionary of African Biography na kilichoniingiza humo ni kutafiti na kuandika historia ya Sykes kuanzia mwishoni mwa 1800 hadi mwanzoni 2000.

Ningekuwa naandika dini nisingeweza kuwa katika viwanja hivyo.

Lakini kitu kimoja tambua hata ikiwa hupendezewi kama wengi walivyokuwa hawakupenda kabla yako, mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika hauna mfanowe.

Sykes ndiyo walioasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 baada ya kuasisi African Association 1929.

Historia hii inakuudhi?
 
Jibu zuri sana.
Kwamba hauwaandiki kina Sykes kwa sababu ni waislam wenzako, bali ni kwa sabab walipigania uhuru na historia inayofundishwa na watawala haiwataji.

Binafsi naomba unisaidie kufaham, hiv kwanini baadhi ya wapigania uhuru wa nchi yetu wamesahauliwa? Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Suleiman Takadir nikiwataja kwa uchache.

By the way naomba nifikishie salam kwa mama yangu mhe. Ridhiki Shahali Ngwali, japo hanifahamu ila nilikua tayari kumchagua kuwa m/kiti wa CUF taifa katika uchaguzi uliovurugika wa 2016.
 
Dingi si ungesema tu Sykes hahusiki na stori ya Dr Edith? 🤣🤣🤣. Mimi naona ulipitiwa ila ungeshajikuta unasema bibi yake na Dr Edith alikuwa shogake na mke wa Sykes.. yaani huwa kwa namna yoyote ile lazima uchomekee jina Sykes kwenye uzi.
 
Suala la historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na wahusika wa harakati hizi ni kitu kilikuwa nyeti sana katika miaka iliyopita.

Hapa naona wewe umeligeuza jambo hili kuwa somo la kunikejeli na kuweka picha za vichekesho.

Sykes siwachomeki katika historia ya Tanganyika.

Vipi utamchomeka Kleist Sykes mzalendo aliyeasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 na vyama hivi vyote vilipambana na ukoloni?

Vipi utamchomeka Abdul Sykes na nduguze wazalendo waliokuwa wafadhili, viongozi na waasisi wa TANU na walimpokea Nyerere na kuishi na yeye?

Nimeandika kitabu kizima kuhusu Sykes (1998) na kitabu kimechapwa matoleo manne.

Kila aliyesoma kitabu hiki kimemuathiri.

Kitabu hiki kimebadili historia kwanza ya uhuru wa Tanganyika na pia historia ya Julius Nyerere.

Waliowatoa Sykes katika historia leo wanajifunza upya historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere.
 
Mama...
Nasikitika kwa kunipa jina "Dingi."

Mimi siko hapa kufanya vichekesho bali nipo hapa kusomesha.

Unapenda baki darasani usome.
La unaona historia hii inakuchoma moyo achananayo.

Suala la historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na wahusika wa harakati hizi ni kitu kilikuwa nyeti sana katika miaka iliyopita.

Hapa naona wewe umeligeuza jambo hili kuwa somo la kunikejeli na kuweka picha za vichekesho.

Sykes siwachomeki katika historia ya Tanganyika.

Vipi utamchomeka Kleist Sykes mzalendo aliyeasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 na vyama hivi vyote vilipambana na ukoloni?

Vipi utamchomeka Abdul Sykes na nduguze wazalendo waliokuwa wafadhili, viongozi na waasisi wa TANU na walimpokea Nyerere na kuishi na yeye?

Nimeandika kitabu kizima kuhusu Sykes (1998) na kitabu kimechapwa matoleo manne.

Kila aliyesoma kitabu hiki kimemuathiri.

Kitabu hiki kimebadili historia kwanza ya uhuru wa Tanganyika na pia historia ya Julius Nyerere.

Waliowatoa Sykes katika historia leo wanajifunza upya historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere.
 
Babu shikamoo, nyie wenzetu mlibahatika mlipata elimu ya first grade. Lakini siku hizi elimu imechakachuliwa sana na sijui ni kwanini...? Ila Babu sema ukweli Dkt. Edith Kitambi {mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi} hakuwa bibi yetu kweli huyu...?

Kama ni kweli Babu uliopoa 🥰🤣🙈🙈​
 
🙄🙄🙄🙄ina maaana Leo andiko lote hamna Sykes na uislamu? Ngoja nirudie kusoma
Mpaji...
Nakuwekea wapi utamsoma Nyerere kutoka kalamu yangu na wapi utawasoma Waislam na Uislam kutoka kwangu:

''Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961 Salum Abdallah Popo aliachana mkono na Nyerere kama wengi walivyofanya na aliwekwa kizuizini na serikali chini ya sheria ya Preventive Dentetion Act of 1962 kwa ajili ya msimamo wake wa kuamini kuwa vyama vya wafanyakazi viwe huru.

Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU)...''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes).

Huyu Salum Abdallah ni babu yangu na picha yake hiyo hapo chini:

1696564760332.png

Kulia: Kassanga Tumbo (Katibu) anemfuatia ni Salum Abdallah (Mwenyekiti) TRAU miaka ya 1950 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika
Sasa tusome Uislam na Waislam:

Waikela alinieleza jinsi Waislam kwa umoja wao walivyomuunga mkono Julius Nyerere na harakati za uhuru.

Vilevile alinieleza kwa muhtasari siku zake kizuizini pamoja na babu yangu katika gereza la Uyui, Tabora kwa kile kilichoitwa kosa la ‘’kuchanganya dini na siasa.’’

1696565253718.png

Waliosimama nyuma kulia wa kwanza ni Bilal Rehani Waikela chini yake ni Julius Nyerere alipokwenda Tabora mwaka wa 1955 katika juhudi za kuijenga TANU.​

Nina deni kubwa kwake kwa Mzee Waikela kwa kunipa picha za wakati ule na nyaraka zake binafsi juu ya ‘’mgogoro,’’ wa EAMWS uliozushwa mara baada ya uhuru.

Bwana Mpaji,
Huenda historia hii inakukera kama ilivyowaudhi wengi hadi kufika kuweka mikakati wakaifuta.

Kwangu mimi kama ulivyosoma hapo juu ni historia ya wazee wangu wengine kwa nasaba na wengine kwa ujamaa wa karibu sana.

Sikuweza kustahamili kuona historia iliyopo si ya kweli ikabidi nitafiti na nimeandika kitabu kizima.

Historia hii sasa ipo huu mwaka wa 25 na ibra kubwa ni kuwa watu hawachoki kuihadithia na kuniuliza maswali na baadhi kama wewe kunikejeli.

Nasikitika kuwa huna hata ustaarabu wa kuweka staha na heshima kwenye taazia ya marehemu Dr. Edith Kitambi.
 
Babu shikamoo, nyie wenzetu mlibahatika mlipata elimu ya first grade. Lakini siku hizi elimu imechakachuliwa sana na sijui ni kwanini...? Ila Babu sema ukweli Dkt. Edith Kitambi {mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi} hakuwa bibi yetu kweli huyu...?

Kama ni kweli Babu uliopoa
"Tukazoeana sana nikawa nimepata pia daktari kidogo nikijisikia namwendea."

Jibu lako lipo hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom