TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

Majibu ya maombi ya siku tatu

Mungu sio mnafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Baba Swalehe unaongea nini aisee, unawaza kinyumenyume mkuu! watu wakienda kulia wewe kushoto! kwani ulikuwa ukimchukia Mama? kakufanyaje?

Sio kwamba tuna ya kujifunza katika maisha yake hasa kukuza elimu kwa shule zake bora sana? au ni yale makofi alipiga bungeni ile si ni mob psychology tu wenzio wakipiga makofi nawewe unapiga au?

kifo cha mtu mkubwa ni ukumbusho kwa kila mmoja wetu hasa zaidi kwa mafisadi , leo akaunti yako benki imenona pesa ya umma kesho hamad! ni marehemu , pesa zako zote ambazo hakuna mtu alijua ni ngapi leo zinajulikana na zinarudi kwa umma (watoto wako) ambao watazitumbua bila hofu tena tofauti kabisa na misingi yako!!
 
Nadhani sasa Tanzania Assemblies of God wataanzisha mchakato wa kuchukua kanisa lao. Muda si mrefu mgogoro utaanza.
Hakuna mgogoro hapo. Kanisa lilikuwa na usajili wake. Hakuna uhusiano wa Kanisa lake na Tanzania Assemblies of God. Askofu alikuwa ndiye mwenyewe na mwanzilishi ni yeye.
 
Hakuna daktari duniani anayeweza sema mgonjwa kafa kwa ugonjwa gani publically ni Siri yake na mgonjwa tu aweza waeleza familia yake tu ambao walimuuguuza.Huyo pathologia wako hawezi sema lolote zaidi ya kuiambia familia.Unajuaje Kama hajafanyiwa?
Na familia yake kupewa ripoti?

.Huyo Ni.mbunge ujue.Nitajie pathologia yeyote aliyewahi Anika jina la mgonjwa na kusema kafa kwa ugonjwa gani publically
 
Rest in Peace Mama Getrude. Nayakumbuka sana maombezi yako ya upepo wa kisulisuli pamoja na jitihada zako za kuombea CORONA isiingie Tanzania, japo siku iliyofuata Corona ikatia timu.
 
Reactions: amu
Badilisha hicho kichwa cha habari sema "Mbunge na Mfanyibiashara Maarufu...."

Rip

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ataelewa wapi huyo mdeki barabara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upumzike kwa amani mama, na Mungu akusamehe Dhambi zako ,Hatimaye Covid -19 imekuchukua, wala siyo presha Kama wanavyodanganya,Presha haijakuua miaka yote, ije ikuue kwenye janga la Corona wakati masharti yote ya Presha uliyazingatia.
Serikali kuweni wazi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaburi 90: 1 -12, Maombi ya Musa mtu wa Mungu.
Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.

Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama majani yameayo. Asubuhi yachipuka na kumea,
Jioni yakatika na kukauka. Maana tumetoweshwa kwa hasira yako, Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.

Umeyaweka maovu yetu mbele zako, Siri zetu katika mwanga wa uso wako. Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite. Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.

Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako? Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako? Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.

Coment:
Tuyatumie maisha haya mafupi kwa hekima. Hekima kuu ni kujiandalia utakapoishi milele. Bwana Yesu akawafariji wafiwa wote na washirika wote. BWANA akawaangalie watu wake na kuwafunika. Ametangulia katika njia yetu sote. Kwa wakati wetu tutaitika. BWANA utupe hekima ya kuzihesabu siku zetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…