Tanzia: Diwani wa CCM Ifakara afariki dunia!

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
8,008
13,733
Diwani wa CCM kata ya Ifakara ndg Ramadhani Kiombile, ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa halmashauri amefariki dunia leo katika hospitali Muhimbili. Chanzo changu kutoka ndani ya halmashauri kimenithibitishia habari hizi. R I P Diwani.
 
Poleni sana wafiwa, Mungu awape Faraja.

Jana pia tulisikia Diwani mwingine wa CCM kule Monduli amefariki dunia.

Naona Nape na Mwigulu sasa Jasho lishaanza kuwatoka maana......
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
Pumzika kwa amani.
Dunia inafujo nyingi na masumbufu, marehemu ni shahidi wa hilo, maana kwenye mbio za udiwani aliona mengi!

Wadau, nawaomba tusianze kuongelea mambo ya nafasi ya udiwani, maana tayari wengine wakisikiaga vifo vya wenzao udenda unawatoka!
Tuongelee kuhusu kumpumzisha mwenzetu.
 
RIP Diwani poleni Ndugu na Wana CCM nyinyi mlimpenda lakini Mungu Kampenda Zaidi.
 
Mimi nadhani kuanza kupigia chapuo ile kata ni jambo la muhimu sana. kumbuka kifo ni namna ya kubalance nature. The man is gone na maisha lazima yaendelee. Kazi kwa CDM maana Ifakara (na jimbo la Kilombero kwa jumla) ilifanyiwa mchakachuo wa kufa mtu 2010.
 
Rip Gamba! It's time for M4C. Uchaguzi lini lakini? Maana Uchaguzi ndio point ya msingi Hapa mengineyo ni kawaida kufa kufaana.
 
Diwani wa CCM kata ya Ifakara ndg Ramadhani Kiombile, ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa halmashauri amefariki dunia leo katika hospitali Muhimbili. Chanzo changu kutoka ndani ya halmashauri kimenithibitishia habari hizi. R I P Diwani.

RIP diwani..
 
Mkuu hapo kwenye red ndio mpango mzima, tumpumzishe vipi wakati uko aliko anajibu aliyoyafanya duniani? Kapumzika mwili tuu ila roho bado ni mchakamchaka

Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
Pumzika kwa amani.
Dunia inafujo nyingi na masumbufu, marehemu ni shahidi wa hilo, maana kwenye mbio za udiwani aliona mengi!

Wadau, nawaomba tusianze kuongelea mambo ya nafasi ya udiwani, maana tayari wengine wakisikiaga vifo vya wenzao udenda unawatoka!
Tuongelee kuhusu kumpumzisha mwenzetu.
 
Mwenyekiti wa halmashauri ya kilombero na diwani wa kata ya ifakara kwa tiketi ya ccm ndg Ramadhani Kiombile amefariki leo asubuhi katika hospitali ya rufaa ya muhimbili alikokua amelazwa kwa matibabu
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
Pumzika kwa amani.
Dunia inafujo nyingi na masumbufu, marehemu ni shahidi wa hilo, maana kwenye mbio za udiwani aliona mengi!

Wadau, nawaomba tusianze kuongelea mambo ya nafasi ya udiwani, maana tayari wengine wakisikiaga vifo vya wenzao udenda unawatoka!
Tuongelee kuhusu kumpumzisha mwenzetu.
Kuna tatizo gani?
Muda ni kitu muhimu sana katika maendeleo, wakati tunapanga mikakati ya mazishi ni vyema pia kuzungumzia mustakabari wa kisiasa kwa wana Ifakara.

Ni vyema vitu hivi vikaenda sambasamba.
 
Back
Top Bottom