Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,521
- 6,517
RIP Col. Aliwahi pita shuleni kwetu kipindi shule zinachomwa chomwa moto in 90s
Dah! RIP Colonel! You were a very tough soldier. Nilikuwa Mafinga Op Mazingira 1992, wewe ulikuw op gani Mpemba?Alikuwa ni Mkuu wetu wa Kikosi tukiwa Mafinga - tulipopita pale kwa Mujibu wa Sheria - RIP Colonel.
Dah! RIP Colonel! You were a very tough soldier. Nilikuwa Mafinga Op Mazingira 1992, wewe ulikuw op gani Mpemba?
Marehemu atakumbukwa kwa mengi. Huko huko Jkt Ruvu siku tumekwenda kulinda mahindi. Si tunachukia debe la kuchemshia mahindi tukifika tunatayarisha moto, maji jikoni, kukwanyua mahindi mti wa mhindi unabaki wima. Wakati huo kuna patrol njia zote asije tokea kamanda tukapigwa taiti. Siku ya kufa bwana Marehemu kaingilia huku engineering na kundi lake kapita katikati ya shamba hamadi huyu katokeza kwenye debe la mahindi linachemka " kamata wote" debe lilipigwa teke moto kuvurugwa kila mtu kaingia shambani.Marehemu akasikika akisema "Afadhali nguruwe mnyama kuliko nguruwe binadamu" sisi tuko undercover tunachungulia kwa mbali gizani. Zilikuwa enzi za mafunzo RIP MLAY
Mkuu hapo umenikumbusha mambo ya "Green Vest ya kijani".Nilikuwa Mbele yako kidogo "Mr. BigMan" - Operesheni Kambarage 1990/91. Nilikuwa "D" Coy - Sir Major wetu alikuwa Mchaga Mmoja Msumbufu sana anaitwa Ndossa. Tukiwa bado kuruta wageni - tulikuwa tukisafisha/ tukipiga deki sakafu za zile Hanga zetu kwa yale magudulia ya maji ya kupikia - anakuja saa sita za usiku na kifimbo chake na kuchokonoa zile sehemu za sakafu ambazo hazina cement; Halafu anasema hatukufanya kitu - then adhabu hakuna kulala mpaka tusafishe tena - hivyo tukawa tunalala saa nane usiku; na kuamka saa kumi na moja. Tukamjulia nini cha kufanya - tukawa tunafagia tu - halafu tunachukua kitambaa na kusafisha zile sehemu za sakafu ambazo hazina cement. Akija kukagua - anasema kazi nzuri. 😀😀😀😀
Mkuu Naona tulikuwa wote, mimi nilikuwa D- Coy usawa wa ngedere!!!Kuna rafiki yangu mmoja aliiba mayai Ruvu JKT OPERESHENI TUJISAHIHISHE sasa akipita eneo la admin Kamanda marehemu Mlay akamwona. Akamwita akamwambia lala chini vingirika yale mayai yakavunjika combat yote upande wa chini ikalowa akamwambia nenda. Alikuja kule kombaini B yuko hoi kutueleza tulicheka. Lakini aliiba mayai anavyosema mpaka akanunua 177 radio
Plus Maj Gen Makame Rashid. RIP.Huyu kundi lake lilikuwa la akina Kanali Meena, Matingasi na wengineo.
Hii ya mke wake ilitokea kj 822 buhemba jktSiku moja pale Msange mkuu wa majeshi Major General N. Mkisi alikua anatoa hotuba mbele ya maaskari na makamanda. Katikati ya hotuba akamwamrisha mkuu wa kikosi cha Msange Lt. Col.Sanga Awape makamanda soda. Mlay bila kusimama akasema yeye sio mtoto mdogo wa kunywa soda. Mkisi akasema. Sanga mke kamanda beer. Alikua ni mwanamme wa shoka. Alishawahi kumuweka mke wake quarter guard.RIP KAMANDA
Dah! Mambo ya kuazima appetite kama huna! Really missing those daysMkuu hapo umenikumbusha mambo ya "Green Vest ya kijani".
.....hakupenda Askari wake ale msosi mbovu, alikuwa anakagua mpaka nyanya. Harage wese na wali wese !
Mlalakuwa tukaja kula wali wa kuchemsha kama wachina. Mafuta wanauza hivi hivi tunaona.
.....hakupenda Askari wake ale msosi mbovu, alikuwa anakagua mpaka nyanya. Harage wese na wali wese !
Mlalakuwa tukaja kula wali wa kuchemsha kama wachina. Mafuta wanauza hivi hivi tunaona.