TANZIA: Col T. N. Mlay (rtd) has passed away

TANZIA: Col T. N. Mlay (rtd) has passed away

Kuna jamaa yangu alikuwa anaitwa Kapongo, alimzingua Hakimu wa Kambi zigua mmoja akiitwa Waziri. Akamkamata akamfubgulia mashtaka, akaendesha kesi mwenyewe kama Hakimu na kisha akamfunga wiki mbili. Kapongo aka andika barua kwa CO TN Mlai akilalamika haki haikutendeka na Captain Waziri anaitumia Mahakama vibaya. CO TN Mlai akamsikiliza na akatengua uhakimu wa Captain Waziri.
 
Masahihisho madogo

Hatukuwahi kuwa na mkuu wa majeshi akiitwa Major General Mkisi.

Ila kama kumbukumbu zangu zinanielekeza vyema ni kuwa tuliwahi kuwa na mkuu wa jkt akiitwa Major General Mkisi
Ninakumbuka enzi hizo sister alikuwa JKT Mgulani. Akitoroka kuja home saa ya kuondoka anasubiri daladala, akiona gari ya Mkisi tumbo joto
 
Masahihisho madogo

Hatukuwahi kuwa na mkuu wa majeshi akiitwa Major General Mkisi.

Ila kama kumbukumbu zangu zinanielekeza vyema ni kuwa tuliwahi kuwa na mkuu wa jkt akiitwa Major General Mkisi
Sawa kabisa na kabla ya hapo alikuwepo Mzee Kaswende na kabla hapo Mzee Nkulila kama wakuu wa JKT.
 
R.I.P Col Mlay! Nakukumbuka uliwapenda san kuruti ila hukuwa mtu wa mchezo mchezo. Kuna kuruti walipeana Mimba pale Mafinga ukatuambia hapa sio sekondari hatufukuzi mtu. Badala yake ukasema lazima uwafungishe ndoa ya kiserikalo iwe fundisho kwa wengine. Jamaa walikaa mahabusu mpaka wazazi wote pande mbili wakaja wakaamua kuyamaliza masuala hayo home ila binti alikatisha mafunzo na kurudi home.
 
Siku moja pale Msange mkuu wa majeshi Major General N. Mkisi alikua anatoa hotuba mbele ya maaskari na makamanda. Katikati ya hotuba akamwamrisha mkuu wa kikosi cha Msange Lt. Col.Sanga Awape makamanda soda. Mlay bila kusimama akasema yeye sio mtoto mdogo wa kunywa soda. Mkisi akasema. Sanga mke kamanda beer. Alikua ni mwanamme wa shoka. Alishawahi kumuweka mke wake quarter guard.RIP KAMANDA
Kweli kabisa, alimuweka mkewe ndani kwa kosa la kuchelewa kwenye paredi yake pale Ruvu JKT wakati huo akiwa Captain.
 
Back
Top Bottom