TANZIA: Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jaji Maulidi amefariki dunia

LUKAZA

Senior Member
Nov 30, 2010
140
70
Habari kutoka kwa Rafiki wa Karibu wa Marehem amenipa taarifa hizo Mh Jaji Zubeir Maulid alikuwa ni mwalimu na aliwahi kuwa Jaji na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini.

Jaji Zuberi pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC).

Marehemu amefariki nyumbani kwake kwa mchina mjini Zanzibar na maziko yanatarajiwa kufanyika kwao Mbuzini Unguja.
 
Habari kutoka kwa Rafiki wa Karibu wa Marehem amenipa taarifa hizo Mh Jaj Zubeir Maulid alikiwa ni mwalim na Aliwahi kuwa Jaji na amewahi kushika nyazifa mbali mbali Serekalini Ikiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Marehem Amefariki Nyumbani kwake Kwamchina mjini Zanzibar na maziko yanatarajiwa kufanyika kwao Mbuzini Unguja

Leo naona ' Israeli ' amekasirika kwani alianza na Mr. Six saa 10 alfajiri huko Germany, akaja kwa Mzee ' Side boy ' wa Azam na sasa kamaliza Jaji ' Mau ' kwa kurudisha ' namba '.
 
Jamani tujifunze kuishi vema na kuwatendea haki binadamu wenzetu. Duniani tunaishi mara moja tu. Kutumiwa kwa maslahi ya wengine hakutujengei heshima wala kupata baraka. Si vyema kuitwa "Bwana yule " wakati una jina lako . Ona sasa aliyefariki ni Bw. Maulid lakini watu wanaongea juu ya "Bwana Yule " aliyewanyima haki Wazanzibari. Hivyo unajisikiaje ndugu yetu !l RIP mzee wetu Maulid.
 
Mungu awarehemu marehemu wote awape pumziko la milele wapumzike kwa amani...Amina.
Huku Sitta kule Zubeir Maulid mwenyewe hapa jamaa yangu karudisha namba leo kajiua kwa sumu na nilikuwa nae juzi tu.all in all ni njia yetu sote tusijisahau kwa kuweka miguu juu kanakwamba tumeumbwa na bunduki kuja kuilinda dunia nasi ipo siku macho tutayafunga so..tunapaswa kusali kila mtu kwa imani yake ili mwisho tuwe na hatma nzuri.
 
Salary slip tuambie na huyu alitamka nini kuhusu mgombea wenu? Maana siku hizi kila kiongozi akifa utambiwa alimsema vibaya malaika wa upendo kwa watanzania. Maana anavyo tupenda mpaka alifikia mpango wa kutuletea mvua ya mabomu.

Pole yenu wafiwa.

Na washawsha!
 
Habari kutoka kwa Rafiki wa Karibu wa Marehem amenipa taarifa hizo Mh Jaj Zubeir Maulid alikiwa ni mwalim na Aliwahi kuwa Jaji na amewahi kushika nyazifa mbali mbali Serekalini Ikiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Marehem Amefariki Nyumbani kwake Kwamchina mjini Zanzibar na maziko yanatarajiwa kufanyika kwao Mbuzini Unguja
Mdau.
Mungu anatuma/anatoa ujumbe mzito leo?
Je ni huyu mwenyekiti wa tume "huru"?
 
Back
Top Bottom