Tanzia: Aliyekuwa mbunge wa Dodoma mjini Padre Severino Supa amefariki dunia

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Mmojawapo wa wa wabunge machachari wa Dodoma mjini Enzi za Mzee Nyerere amefariki dunia usiku wa kuamkia leo saa 5.30 mjini Dodoma

Kwa kizazi kipya wengi hawamfahamu akiwepo mbunge wa sasa mteule Mh. Antony Mavunde.

Mbunge huyu alitawala Dodoma mjini kuanzia 1975 mpaka 1980. Alipokea kijiti toka kwa Padri Simon Chiwanga aliyetawala kuanzia 1970 mpaka 1975 ambapo alikuwa pia waziri wa Elimu enzi za Mwalimu.

Ikumbukwe kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1980 mjini Dodoma ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenye mvutano mkubwa kuliko yote Tanzania nzima ulikuwa unafanana na upinzani mkali katika uchaguzi mkuu uliopita.

Upinzani ulitokana na kwamba wote walikuwa ni Mapadri na wote walikuwa ni wasomi na wote walikuwa wabunge Padri Supa alikuwa mbunge wa taifa akiwakilisha wazazi (TAPA). Padri Supa alikuwa ndiye msomi zaidi maana teyari alikuwa na Ph.D tangu mwaka 1962.

Katika uchaguzi huo Padri Simon Chiwanga alishinda ila Padri Supa alipinga ushindi huo mahakamani kwa kigezo kwamba Padri Simon Chiwanga ushindi wake ulichagizwa kwa kuhonga majembe kijiji cha Nkong`onta ambako sasa ni UDOM(majembe haya ya kulima kwa mkono).

Petition hiyo Padri Supa alishinda na Padri Chiwanga akafukuzwa ubunge, na ndiyo ilikuwa ndiyo mara ya kwanza mbunge kushinda kesi ya kupinga matokeo mahakamani, kilichofuata ni chaguzi ndogo ambapo walioomba kupendekezwa ni pamoja na yeye Padri Supa, kamati kuu ilimkata jina na kuweka wagombea wawili ambao ni Marehemu Sala Mwenge na Donald Kusenhta, mshindi akawa ni Sala Mwenge.

Kutoka marehemu Sala Mwenge kijiti cha ubunge wa Dodoma mjini kilienda kwa Merehemu Hashim Saggafu , toka marehemu Saggafu ubunge wa Dodoma mjini uliendekwa Mh. Madeje, toka kwa Madeje Ubunge ulienda kwa Mh. Malole na sasa ni Mh.Antony Mavunde.

Mwenye kilio kikubwa kabisa cha kifo cha Mbunge huyu ni Mshehereshaji mkuu kitaifa Peter Mavunde baba yake mzazi Antony Mavunde mbunge wa sasa kwani huyu mzee ndio alikuwa mwalimu wake alisoma kwenye secondary yake ya Ovada, ndiko ujanja wake wote alikoupatia kwa huyo mzee, bila huyo Mzee Peter Mavunde angekuwa anachunga ng`ombe kwao kijiji cha Chivutuka.

Poleni sana wananchi wa Dodoma mjini kwa kifo cha mpendwa wenu mbunge wenye historia ndefu mno nikipata muda nitawaeleza kwenye jukwaa la historia.

Fasten your belt, stay tuned enjoy the reading in the coming podium.
 
RIP
kuweka kumbukumbu sawa, dodoma haijawahi kuwa na kiongozi makini, labda malecela kwa mbali
 
Nyerere mpokee mbunge wako na umuonyeshe viwanja vyote vikali Vya ahera
Mpeleke Kwenye mademu wakaliiiii asijione bado anaendeleza upadre
 
Mkiambiwa nchi hii ni ya wakatoliki hamtaki kusikia .....

Nyerere ndo alikuwa Mdini kuliko wote ! Misingi ya CCM imejengwa katika misingi ya kanisa katoliki.... Maslahi ya kanisa ni maslahi ya CCM ndo maslahi ya watawala .... no wonder Rais lazima awe Mkatoliki ..
 
Mkiambiwa nchi hii ni ya wakatoliki hamtaki kusikia ..... Nyerere ndo alikuwa Mdini kuliko wote ! Misingi ya CCM imejengwa katika misingi ya kanisa katoliki.... Maslahi ya kanisa ni maslahi ya CCM ndo maslahi ya watawala .... no wonder Rais lazima awe Mkatoliki ..

Acha uchochezi ww
 
Mkiambiwa nchi hii ni ya wakatoliki hamtaki kusikia ..... Nyerere ndo alikuwa Mdini kuliko wote ! Misingi ya CCM imejengwa katika misingi ya kanisa katoliki.... Maslahi ya kanisa ni maslahi ya CCM ndo maslahi ya watawala .... no wonder Rais lazima awe Mkatoliki ..

Mwinyi na JK nao ni wakatoliki?
 
Kijiji ni ng'ong'ona, mbunge ni sara mwenge, Donald kusenha na kijiji kingine ni chizi tukawasamehe.
Tulia uandike vizuri haraka ya nini?
 
Nyerere mpokee mbunge wako na umuonyeshe viwanja vyote vikali Vya ahera
Mpeleke Kwenye mademu wakaliiiii asijione bado anaendeleza upadre
Nafikiri hii siyo busara kwa GT wa JF kuandika kitu kama hiki! Hii dhihaka ungefanyiwa mpendwa wako ungejisikiaje kama ni muungwana?
 
R.I.P mkuu padre severino
kumbe enzi za mwalimu zilikuwa tamu
hadi mapadre wali ruhusiwa kuwa wabunge
na wanachama wa vyama vya siasa.
 
Mbona wazee wa historia humu JF hawajawahi kutuambia stori za hawa mapadri badala yake tunawekewa stori za wazee wa Kariakoo Gerezani tu?
 
Apumzike kwa amani, hata mimi namfahamu padre huyu miaka ya 1979 na 1980 nilipokuwa nafanya mafundisho ya komunio pale kanisa la mtakatifu Paulo wa Msalaba Dodoma
 
Hao wabunge wa dodoma woote ni mizigo tu, miaka yoote dodoma mjini hawajawahi kutoa mbunge wa maana, ndio maana hakuna mbinyo wowote wa kuifanya serikali ihamie huko.
 
Back
Top Bottom