Tanzania's Unusual Immigration Case

Anapewa permanent residence permit. Uraia lazima aombe!!!
 
Kwa hiyo, siku ambayo Muungano utavunjika, which will be, basi na Wapemba wote wakiwepo wale waliozaliwa huku Bara wafukuzwe fasta kwa sababu kimenuka?

Muungano upo kimaandishi na katiba inaelezea ,uhamiaji wa wanyarwanda na wengineo ulitokea kwa sababu ya ukimbizi wa vita,kutafuta maisha na mambo mengine? Hatujawahi kuungana na Rwanda na kua nchi moja...two uncomparable events
 
Sina hakika kama agizo la Rais wetu Jakaya limeeleweka vizuri kwa watendaji na watekelezaji wake. Isije ikawa kama lile agizo la Mwalimu la kuhamia vijiji vya ujamaa au lile la maduka ya vijiji.

Nimeongea na Polisi mmoja hapa Dar ananiambia wanatengeneza sio chini ya milioni 10 kwa siku kwa "wahamiaji haramu" walioko hapa jijini hasa wale wa jamii ya ki-Asia na ki-Somali!
 

Amakweli tz imeingiliwa na itikadi ya chuki dhidi ya watusi,kama kweli mnapenda amani wakati watusi walipokua wakichinjwa mlifanya nini? mbona hamkutuma majeshi ya kupambana na wauaji? Lakini leo watusi wa kongo wanauawa na kabila akishirikiana na FDLR,tz inakimbilia kusaidia hao wauaji eti M23 inaua?wakati wao ndio wana uawa.
 
watusi acheni hizo!!!!!rudini kwenu bana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.mna utamaduni wa kishenzi sana.mkienda nchi za wengine mnangangania huko na kusema ni kwenu.rudini nawaambieni.

Acheni roho mbaya hiyo,mnachotaka nikupora mali zao tu,fikiri hawa munaofukuza nikixazi cha wakimbizi walio ingia tz 1959 nawengi wa wazazi wao wameisha kufa wamezaliwa tz hawajui rwanda na wala hawana ardhi ya kuishi rwanda kwani baada ya kufukuzwa rwanda ardhi zao zilichukuliwa na wahutu,wewe kumfukuza nikama kukufukuza wewe mwenyewe uende nchi ambayo huijui,fikiria hali hiyo,wanasema kabla hujatendea mtu kitu kibaya anza kwanza ujiweke mahala pake.
 

Wakimbizi wa mwaka 1959 nafikiri walipewa uraia. Na Sera moja wapo ya ujamaa ya Nyerere ilikua kuchanganya wananchi kutoka sehem moja hadi nyingine, yani vijiji vya ujamaa. Hao walioko huko pembezoni kwenye mapori ya boringi wengi wao wamekuja juzi juzi tu baada ya vita ya 1994. Wale waliokuja mwaka 1960 nyerere ali wa mix ktk jamii na wako mjini.
 
Umeanzisha nyuzi kule nimekupiga maswali kumi na mbili,umekimbia. Unaleta hoja zile zile ulizokimbia u[pande mwingine. Nakufuata kwasababu watu wa propaganda kama ninyi mnzidi kututia hasira na mtaondolewa tu!
Kwanza some hii hapa kijuibu hoja zako hapo juu Hapa ni kuwa ushahidi wao unaonyesha wanakubali ni illegal immigrants.
Pili wanakiri wamekuja hivi karibuni, hoja ya kusema walikuja mwaka 1959 ni propaganda ziache zinatia hasira na wanaoteseka ni ndugu zako.

Pili, roho mbaya gani Tanzania imefanya? Sheria gani za kimataifa Tanzania imekiuka? Haki gani za kibinadamu Tanzania imekiuka?

Kuporwa mali ni halali kwasababu hawaku declare wamekuja na kitu gani.
Pili, wamechuma hizo mali kwa kuua watu leo unadhani wana uhalali wa kurudi nazoi.

Tatu hawapaswi kudai mali, walipaswa kushukuru kwasababu sehemu ya kwanza ilikuwa mahakamani wapewe miaka wakitoka huko warudishwe na nguo zao.

Propaganda zenu zinazidisha moto na watatafutwa popote walipo makanisani au misituni.

Wakongo, Warundi, Waganda hawana malalamiko.

Wanyarwanda wanageuza hili suala liwe la xenophobia ili waachiwe kuleta madhara zaidi.
Hapa hakuna watusi au wahautu tunaongelea wahamaiji haramu.

Hivi mwenye roho mbaya ni yule anayekuambia urudi nyumbani au yule aliyekufukuza.
 

Nilipoona hapo kwenye bold letters nika-dismiss article yote hapo hapo, ------- kabisa unapiga propaganda hata katika hili, nani hakumuona kikwete kwenye TV? Angesema hivo si tungemkoma mushikiwabo
 
Nilipoona hapo kwenye bold letters nika-dismiss article yote hapo hapo, ------- kabisa unapiga propaganda hata katika hili, nani hakumuona kikwete kwenye TV? Angesema hivo si tungemkoma mushikiwabo
Gazeti la The East Africa limepoteza credibility kwasababu ya kutofanya uandishi wa kisomi bali kushabikia tu. Jk hakusema Wanyarwanda, alisema wahamiaji haramu. Ilikuwa ni juu ya mhariri kujitridhisha na madai ya msemaji au kuyaweka sawa na si kushabikia.

Tumeona makala nyingi zinatoka Kigali na zile za Nairobi ni kuongeza chumvi.
Nalipenda gazeti hili lakini limepoteza credibility sana.
 

acha uongo dunia nzima inalaani vitendo vya hili kundi kuua,kubaka,kupora mali za wa congomani,kupora madini na maliasili,kama wanasimamia haki ni kwa nini wakina ntaganda wako icc!!!na kuna wengine kibao wanatafutwa!!!!
 
Nimetoa machozi. Hakika kikombe hiki kiiangulie CCM na viongozi wake. 😢
 
Mi ni mtanzania, tena msukuma! Kila anayeunga mkono kunyang'anya mali na kufukuza wakimbizi kama mbwa na alaaniwe! Na ni mseeengerrt
 
Tunatia aibu. Hawa tunaowaita "illegal immigrants" wametukosea nini? Hizi ni siasa za chuki, vindictiveness na xenophobia. Hazikutakiwa kuwa na nafasi katika nchi kama yetu.

Amandla.....
What are we becoming as a people? Mtu anafukuzwa tu kwa kutizama urefu wa pua yake na wembamba? Kikwete is a national disgrace.
 
acha uongo dunia nzima inalaani vitendo vya hili kundi kuua,kubaka,kupora mali za wa congomani,kupora madini na maliasili,kama wanasimamia haki ni kwa nini wakina ntaganda wako icc!!!na kuna wengine kibao wanatafutwa!!!!
Hivi, wewe kwa akili zako timamu unaweza kulaani kabila zima au jumuiya nzima kwa vitendo vya wachache? Kwa sababu Ntaganda yuko ICC basi Watusi wote au wanyarwanda wote wenye asili ya kitutsi ni guilty? Mkimaliza kuwahukumu Wanyarwanda mtageukia akina nani tena? Kwa sababu dhambi ya ubaguzi wa kikabila ni kama kula nyama ya mtu.
 

jibu hoja na uache fitina, ni uongo kagame aliondoka rwanda akiwa mtoto wa miaka minne akatunzwa na kulelewa kama mtoto wa uganda lakini baada ya miaka zaidi ya 40 akarudi rwanda? ni uwongo james kaberebe ni alilelewa kama mtoto wa kongo na kodi za wakongo lakini leo amewageuka na kuwachinja waliomlea kama kuku? watusi si watu
 
Nguruvi3,
Sisi si watoto wadogo. Kikwete aliposema wakimbizi haramu akiwa mkoa wa Kagera kila mtu mwenye akili alijua wanaolengwa ni akina nani. Hata kama Waganda 50 wamekumbwa katika msako huo walioathirika zaidi ni Wanyarwanda, hata wale ambao wameishi Tanzania zaidi ya miaka sitini. Sijaona popote pale zoezi la kuwakamata na kuwafukuza Wachina ambao wana madanguro yao Dar-es-Salaam likiendelea, au Wahindi na wapakistan ambao wanaitana na kupeana ajira katika viwanda wanavyoongoza, au wasomali ambao nasikia wamejaa na kununua mashamba Rufiji. Sijaona. Mpaka nitakapoona hivyo, na muda unazidi kwenda, nitaendelea kuamini kuwa Kikwete alilenga Wanyarwanda kwa sababu za kisasi chake tu kwa Kagame.
 

Hawa wamekuja baada ya mwaka 1996. Mwaka 1996 wanyarwanda warirudishwa rwanda na burundi. Nakumbuka enzi hizo walikua wana amuru kuimba hata ubeti mmoja wa wimbo wa taifa ama wa tanzania tanzania. Hawa waliopo sahizi ni wajuzi juzi tu, na nifikiri si kweli wanatumia hiyo creteria ya urefu kwani hakuna watanzania warefu? wanaorudishwa ni wahamiaji kweli kweli, sema kuna mapungufu kwa wale walio olewa na kuolewa, lakini majority ni wahamiaji haramu.

Na je umesikia katika walalamishi kwamba yeye ni msukuma, ama mhaya ama mkwele? Tanzania hatuna kabila la wahutu ama watusi. Hivyo yoyote ambaye hajaolewa ama kuoa mtanzania na hana karatasi ni mhamiaji haramu.

Birth certificate, zilikua hazitolewi mahospitalini mtu alipokua anazaliwa kwa sehemu kubwa sana ya Tanzania na tena huko ngara,karangwe na b,mulo zilikuwa hazitolewi kabisa na ilikua haiwezekani kuipata labda kama unataka kujiunga na jeshi,polisi ama chuo. Sasa hao wenye nazo wamezipata lini waweke copy kwenye mtandao. Eti kisingizio zimechukuliwa, wote wamenyang'anywa hata wale waliopitia porini na ng'ombe zao?
 

mokala 1989 unanichosha mdogo wangu....kwani mtu kwenda anakotaka shida ipo wapi?hata kama ni ------ au msukuma anahaki ya kuhamia nchi yoyote atakayo...balali (R.I.P)si alikuwa(kama kweli alikufa) mmarekani unajua hilo?usiseme hivo brain drain iliyopo huko bongo pekee inatisha achana na watu wanaohama nchi....wewe siyo mahaka kutuhumu Gen James Kabarebe......watutsi ni watu....Tuache ubaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…