nina wasiwasi na uraia wako, huwezi kuwa mtanzania halisi wewe lazima mama yako atakuwa ni mtusi!
Well, kama nilizaliwa Tanzania kwa mama mtusi na baba Mtanzania bado siwezi kuwa Mtanzania? Mkuu naona na wewe umeambukizwa ugonjwa wa wanasiasa hasa pale wanapozidiwa hoja na kuishia kuhoji uraia wa mhusika.
Nafikiri Watanzania wengi tumekuwa programmed jinsi tunavyofikiri na kuhoji mambo. We have been programmed to think in the same way tukidhani kufanya hivyo ndiyo kuonyesha uzalendo na utaifa. Ukiwa critical au ukihoji mambo hasa juu ya serikali unadhaniwa kuwa siyo mzalendo au mtaifa.
Hii kasumba imeenea mpaka kwenye vyama vya siasa. Ukihoji masuala fulani juu ya CCM, automatically WanaCCM wanakuweka katika kundi la Chadema. Pia ukihoji masuala ya Chadema, wafuasi wake wanakuweka katika kundi la CCM. Kwa hiyo, usidhani kuwa unaweza kunitisha na wasiwasi wako juu ya uraia wangu kwa kuwa wewe siyo mtu wa kwanza kunihisi hivyo. Who are you to question my nationality anyway?
Nimeshaambiwa mara kibao kuwa mimi siyo mzalendo na mtaifa na hivyo mhaini. Kwa mfano, Taifa Stars ilishafungwa, nikahoji kiwango chao cha soka nikaambiwa ni mhaini. Nilihoji ushauri alioutoa JK kwa PG in another perspective, nikahisiwa kuwa ni mtusi, though Marais hao walikuja kuonekana wakishikana mikono huku wakicheka to the disappointment ya watu wengi. Kuna mchangiaji mwigine kaniambia kwenye uzi huu huu kuwa yoyote anayehoji suala la wahamiaji haramu ni mhaini.
Pale tunaposhindwa kutetea hoja zetu, tunakuwa na tabia ya kujaribu kuwagawa watu kama siyo kivyama, basi kwa kutumia maneno kama uzalendo, utaifa na hata kuhoji uraia wa mhusika. Tunakopi na kupaste maneno wanayotumia wanasiasa hasa pale wanapokosolewa. I will never fall in that trap.
In fact, sitamsifia mtu mzima au serikali kwa kufanya kazi kwa mujibu wa majukumu yao. They are not babies ili wasifiwe kila mara. Neither have they done something extraordinary to the extent ya kupewa nishani ya kusifiwa. Wanatimiza tuu majukumu yao na ahadi walizozitoa wakati wakiomba kura.
So, what I expect from them is a pay back. Hivyo, sitasita kuikosoa serikali pale nitakapodhani kuwa imefanya kazi yake chini ya kiwango kinachotegemewa au ilichohaidi kufanya. Uzalendo na utaifa wangu ni kuikosoa serikali yoyote ile iliyo madarakani ili next time isirudie makosa iliyoyafanya huko nyuma.