Tanzania's 100 most influential people

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
1. Dr Slaa
2. Mengi

Nawaombeni tutengeneze hii list. Kwa maoni yangu Rais wa nchi anastahili kabisa kuwemo katika list hii, lakini Kikwete hana sifa yoyote ya kuwemo katika list hii au mafisadi wote wa Tanzania kama tunavyowajua. Haya kazi kwenu.
 
Rostam Aziz, ndiye the most influential person nchini TZ kwa sasa ..... no doubt about that!

Kagoda, Richmond, Dowans .... wengine angalau wanafikishwa mahakamani, lakini yeye bado anapeta tu!
 
BAK,
Kabla sijachangia naomba nikuulize... influential katika nyanja gani maana kuna wanasiasa, kuna wenye vijisenti, nk tuangalie vigezo vipi?
 
BAK,
Kabla sijachangia naomba nikuulize... influential katika nyanja gani maana kuna wanasiasa, kuna wenye vijisenti, nk tuangalie vigezo vipi?

Swali zuri sana, WoS. Wanaweza kabisa kuwa na vijisenti, lakini walivyovipata kihalali kama Mengi, siyo kama akina Mkapa, Chenge, Rostam, Mramba n.k. Wanaweza pia kuwa wanasiasa, maprofessor, wafanyabiashara na hata wanamichezo pia lakini nyendo zao kimaisha zinakubalika na walio wengi katika jamii ya Watanzania. Kuna huyu jamaa anayeitwa John Mashaka naye anastahili kabisa kuwemo kwenye list hiyo. Wanaweza pia kuwa wanaishi Tanzania au nje ya Tanzania.
 
BAK,
Kabla sijachangia naomba nikuulize... influential katika nyanja gani maana kuna wanasiasa, kuna wenye vijisenti, nk tuangalie vigezo vipi?

Nadhani mtu akiwa influential, no matter yuko wapi, bado atabaki influential!

Jesus, is masihi, mtume, (NIKO AMBAYE NIKO) -religion

Newton-scince

Pele-mpira

Michael Jackson-muziki

hawa wote ni influential ktk nyanja tofauti lakini so long wanafanya kwa jamii, watajulikana tu!

1. Nyerere

2. Chachage

Au walio hai tu??

1. Masanja Mkandamizaji
2. Joti
3. xxxxxxx
 
Wana influence nini? Religious thought, political landscape, popular culture, music, and art;?, scientific and technological development? Business and investment? Labda tuweke wigo wa aina fulani hivi (focusing) vinginevyo, unaweza kukuta watu wanainfluence vitu vingi tu na watu ni wengi mno na namba ya 100 haitawatendea haki wengine
 
I will go by BAK's clarification:
-Professor Issa Shivji - huyu ni gwiji katika Sheria na anaheshimika sana katika Sheria za Ardhi na Ajira
- Anne Kilango Malechela- nadhani hakun aubishi kuwa hapa karibuni michango yake bungeni imezua gumzo na anakubalika - amewezesha kubadili sura nzima ya namna chama tawala kilivyokuwa kina behave Bungeni kwa maana ya kulindana hata kwenye mambo bayana kama hili la kukosa uwajibikaji na rushwa.
- Jaji Joseph Sinde Warioba - huyu naye anaaminika kama mmoja wa viongozi wachache safi wenye uhalali wa kukemea rushwa na akizungumzia kero hii watu wanamsikiliza
-Mchungaji Mwakasege - huyu anakubalika kutokana na mahubiri yake ya kuupinga umaskini na kuonyesha kupitia maandiko ni jinsi gani mtu unaweza kupata pesa kihalali, uitawaleje pesa hiyo na pia serikali ifanye nini kuwezesha wananchi wake wasitumbukie zaidi na zaidi katika umaskini.
 
Wana influence nini? Religious thought, political landscape, popular culture, music, and art;?, scientific and technological development? Business and investment? Labda tuweke wigo wa aina fulani hivi (focusing) vinginevyo, unaweza kukuta watu wanainfluence vitu vingi tu na watu ni wengi mno na namba ya 100 haitawatendea haki wengine

Inaweza kuwa katika mambo ya kisiasa, elimu, haki za binadamu, dini, michezo n.k. ali mradi mambo ambayo yana fuatiliwa kwa karibu na walio wengi katika jamii. Kwa mfano kwa Marekani pamoja na watu kama Michael Jordan na Magic Johnson kuretire miaka miangi katika mchezo wa Basketball bado wana influence kubwa katika mambo mbali ya kijamii Marekani. Oprah Winfrey pamoja na kuwa tunaweza kusema ni Mtangazaji tu lakini anaheshimika sana miongoni mwa Wamarekani wengi wakiwemo wazungu, weuzi na hara rangi nyingine. Na kama utakumbuka alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kumpa support Obama pamoja na kuwa hajawahi kufanya hivyo katika chaguzi zote za Marais wa Marekani zilizopita katika miaka ya nyuma.
 
Nadhani mtu akiwa influential, no matter yuko wapi, bado atabaki influential!

Jesus, is masihi, mtume, (NIKO AMBAYE NIKO) -religion

Newton-scince

Pele-mpira

Michael Jackson-muziki

hawa wote ni influential ktk nyanja tofauti lakini so long wanafanya kwa jamii, watajulikana tu!

1. Nyerere

2. Chachage

Au walio hai tu??

1. Masanja Mkandamizaji
2. Joti
3. xxxxxxx

Mie nilikusudia walio hai tu, lakini ukiangalia Nyerere pamoja na kuwa hayuko nasi lakini bado watu wengi tunamuenzi kwa mengi mazuri aliyoyafanya kwa Tanzania na hata kwa nchi nyingine za Kiafrika bado wengi wanamuona kama ni shujaa. Hata hii leo nikikutana na Waafrika wengi, wengi hupenda kuulizia kuhusu Nyerere pamoja na kuwa aling'atuka madarakani miaka 24 iliyopita, hawaulizi kabisa kuhusu Mwinyi, Mkapa au Kikwete. Naona tuwaweke walio hai tu.
 
Swali zuri sana, WoS. Wanaweza kabisa kuwa na vijisenti, lakini walivyovipata kihalali kama Mengi, siyo kama akina Mkapa, Chenge, Rostam, Mramba n.k. Wanaweza pia kuwa wanasiasa, maprofessor, wafanyabiashara na hata wanamichezo pia lakini nyendo zao kimaisha zinakubalika na walio wengi katika jamii ya Watanzania. Kuna huyu jamaa anayeitwa John Mashaka naye anastahili kabisa kuwemo kwenye list hiyo. Wanaweza pia kuwa wanaishi Tanzania au nje ya Tanzania.

Wengine madhambi yao bado kujulikana ingawa wanapata fedha unazoziita za "halali". Je wanalipa kodi stahiki kwa Selikari? Hawanyonyi wafanyakazi waliopo chini yao? Wanaweza kuwa influential lakini pia wakawa wamefanya maovu kibao ila wanahakikisha hayaifikii jamii. Kuna baadhi ya maprof, ambao hula Uroda na wanafunzi wao, je nao tuwaweke au kwa vile taarifa zao hatuna hivyo hakuna uhalali wa kuwaacha? Na yule ambaye tunasema ni fisadi je pale mahakama itakapomsafisha tutam include katika list? Ndugu ungeweka vigezo vinavyoeleweka na ambavyo havijicontradict.
 
Dr Slaa:
Huyu juhudi zake kubwa za kupambana na mafisadi na kuwa mstari wa mbele katika kutete maslahi ya Wtanzania walio wengi. Kama mtakumbuka hivi karibuni alikuwa mstari wa mbele pale alipotaka mishahara na marupurupu ya Wabunge yapunguzwe na kutumia pesa hizo katika kuongeza mishahara ya Walimu.

Pia pamoja na vitisho toka kwa watu mbali mbali ndani ya CCM na Serikali kuhusu list ya mafisadi aliyoitoa na ufisadi wa EPA, hakuyumba alisimama kidete dhidi ya watu hao na hii leo kumekuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya wengi ambao walikuwemo katika list ya mafisadi.

Mengi:
Huyu kwa kuonyesha kwamba unaweza kabisa kufanya biashara bila kutumia njia za haramu na biashara zako kuwa na mafanikio ya hali ya juu. Na pia kwa kutumia utajiri wake kusaidia yatima mbali mbali ndani ya nchi yetu na siku za karibuni amekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya mafisadi. Hivi karibuni walirushiana maneno na Mkuu wa PCCB pale alipomwambia kwamba hafanyi kazi zake za kupambana na rushwa na ufisadi kama inavyostahili.

Mbunge Shellukindo:

Huyu kwa kusimama kidete kulinda maslahi ya nchi katika sakata la Richmond na pia kupinga manunuzi ya mitambo chakavu ya Richmond/Dowans. Alionyesha ujasiri wa kuongea bila woga au kufuata mstari wa kutetea maslahi ya CCM
 
Wengine madhambi yao bado kujulikana ingawa wanapata fedha unazoziita za "halali". Je wanalipa kodi stahiki kwa Selikari? Hawanyonyi wafanyakazi waliopo chini yao? Wanaweza kuwa influential lakini pia wakawa wamefanya maovu kibao ila wanahakikisha hayaifikii jamii. Kuna baadhi ya maprof, ambao hula Uroda na wanafunzi wao, je nao tuwaweke au kwa vile taarifa zao hatuna hivyo hakuna uhalali wa kuwaacha? Na yule ambaye tunasema ni fisadi je pale mahakama itakapomsafisha tutam include katika list? Ndugu ungeweka vigezo vinavyoeleweka na ambavyo havijicontradict.

Nadhani kama hakuna tuhuma dhidi ya watu hao, basi tuwaone kwamba ni safi na hii ni JF wanaweza kabisa wakatokea wanaJF wakamwaga tuhuma nzito dhidi ya watu hao ambao hatujui uchafu wao. Siyo maprofessor wote wa vyuo vyetu wanakula uroda bado naamini kwamba kuna baadhi ambao wanafanya kazi zao bila kupindisha ethics za taaluma zao wanaweza kuwa Tanzania au nje ya Tanzania.
 
Wengine madhambi yao bado kujulikana ingawa wanapata fedha unazoziita za "halali". Je wanalipa kodi stahiki kwa Selikari? Hawanyonyi wafanyakazi waliopo chini yao? Wanaweza kuwa influential lakini pia wakawa wamefanya maovu kibao ila wanahakikisha hayaifikii jamii. Kuna baadhi ya maprof, ambao hula Uroda na wanafunzi wao, je nao tuwaweke au kwa vile taarifa zao hatuna hivyo hakuna uhalali wa kuwaacha? Na yule ambaye tunasema ni fisadi je pale mahakama itakapomsafisha tutam include katika list? Ndugu ungeweka vigezo vinavyoeleweka na ambavyo havijicontradict.

Angalizo zuri sana hilikwa sababu wengine wanaonekana kama malaika kumbe wana madhambi kuliko hawa wanaoimbwa kila siku kuwa ni mafisadi
 
Angalizo zuri sana hilikwa sababu wengine wanaonekana kama malaika kumbe wana madhambi kuliko hawa wanaoimbwa kila siku kuwa ni mafisadi

Yawekwe hapa basi madhambi hayo!!! Hapa ni JF where were dare to talk openly!!! Vinginevyo tutawashuku hata wasiostahili kushukiwa. Mbongo anaweza kujishindia Lotto ya $20 millioni akirudi bongo kufanya vitu vyake huku anameremeta basi machoni mwa wengi watamuona ni fisadi. Mimi naamini kabisa bado wapo Watanzania wengi ndani na nje ya nchi ambao wanaishi kihalali kabisa, ni asilimia ndogo sana ya Watanzania ndiyo mafisadi haifiki hata 10%
 
Inawezekana hawa watu wana mapungufu yao katika utendaji ila kazi zao zinaonekana katika jamii nzima.

1.John Magufuli
2.Helen Kijo-Bisimba
3.Late Chachage
 
Professor Wangwe: Kwa kutetea maslahi ya nchi na kukemea mambo mbali ndani ya serikali ikiwemo ufisadi.
 
Tundu Lissu - Kwa kuinfluence mjadala wa uporaji wa madini
Eric Shigongo - Kwa kuinfluence fasihi andishi na usomaji
Zitto Kabwe - Kwa kuinfluence hoja na mijadala ya bunge
 
Tunasogea kidogo kidogo, lakini sikutegemea hili liwe gumu kiasi hiki, lakini tutafika tu.
 
Back
Top Bottom