Tanzanians Diaspora Summit on 18th December 2009

Wazalendo Wenzangu;

Napenda kuwajulisha kuwa Registration imekwishaanza na tayari Wazalendo wa Ndani na Nje ya Nchi Wamejitokeza.

Kujiandikisha unaweza kuomba form, kuijaza na kuituma kwa: President@tpn.co.tz

Tunaomba pia tusaidiane kueneza habari hii kwa wale wote tunaowafahamu hususani nje ya nchi.
 
Wana JF; ule muda wa ile Conference yetu umewadia na maendeleo ni mazuri. Kuna mbadiliko kidogo ya Kimsingi:

Dates:

Saasa itakuwa ni kwa siku moja tu: Friday 18th December 2009

Venue:

Golden Tulip Hotel; Masaki; Dar Es Salaam

Participation Fees*:

TZS 50,000
 
Sanctus Mtsimbe,
Mkuu wazo zuri sana lakini kitu kimoja tu.. Ulipoweka kiingilio, hii kidogo haikukaa sawa..
Ni muhimu sana kwa chombo kama hiki kujaribu kuvuta watu ktk mkutano wake wa kwanza hasa ikiwa unafanyika nyumbani Tz. Unapoweka kiingilio una limit nafasi na kuondoa uwezekano mkubwa wa kufanikisha kikao cha kwanza.

Ni wazo zuri sana kuunda Taasisi hii, lakini ikiwa serikali yenyewe haitambui umuhimu wa Taasisi hii sioni sabau kabisa ya kujaribu kuitongoza serikali. Taasisi zote za Diasporas huanzishwa kwa baraka za serikali zao na ukweli ni kwamba serikali nyingi hujaribu kuuza hoja hii kwa wakazi wake nje badala ya wakazi wa nje kujikusanya wao wakaanzisha chombo hiki ama kuishawishi serikali, jambo ambalo naliona hapa.

KIla nchi utakayo kwenda ktk dunia ya kwanza utakuta watu wa Mataifa wakiendesha biashara na kuitangaza nchi yao tena basi huchukua mtaa mzima kama sii kitongoji..Miji yote utayokwenda duyniani mchezo ni huo huo na ndio maana nchi kama India, China, na hata Vietnam leo wanatupita tukiwa tumesimama..
Na kulingana na mfumo mzima wa Utandawazi, hawa Diaspora ndio huwa importer wa asilimia kubwa ya mali zinzotoka nchini kwao..Hawa ndio mabalozi wa Uchumi wa nchi zao wakiuza bidhaa hadi culture yao. Leo hii hatuna sababu kabisa ya kupeleka Korosho zetu India ambao wana soko Marekani hali meneja wa masoko ktk shirika la Marekani ni Mtanzania...Acha mbali kuwa na meneja, wapo Watanzania wanafahamu mashirka yanayo agiza Korosho toka India. Hatuan sababu kabisa ya mali yetu kupitia India ili ipate soko Marekani..Huo ulikuwa wakati wa vita baridi..Ukuta wa Berlin kiuchumi umeisha vunjwa wazee wetu..

Leo hii wapo Watyanzaniua wenye madini husafiri hadi Thaioland na China kuuza vito vyao kwa walanguzi China hali tunao Watanzania wanaoweza kuifanya kazi hiyo na kwa malipo mara mbili..Mbali na hayo, masomo ya juu ktk University na kadhalika ni vyama hivi huwawezesha wananchi wake kupata nafasi nchi za nje kirahisi zaidi na kwa gharama ndogo ktk exchange programs acha mbali Matibabu ktk Hospital na Zahanati..
Wakati umefika serikali yetu ikome zile fikra za Kijamaa na kikorosho..Diasporas ni win win situation, kwa msemo wa Kikwete!

Mkuu nitakuwepo ktk mkutano, nikijaliwa - Inshaallah!
 
Ijumaa nishai

bora wangefanya Jumamosi...asubuhi mnaenda kwenye mkutano mpaka time ya Lunch kisha mchana haoooo mnarudi kubadilisha nguo kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zingine

Ijumaa kama unavyojua Dar na ile foleni nani atakuwa na muda wa kwenda kwenye mambo ya diaspora?

Pili kwa nini wasingechukua ule ukumbi wa BOT au pale Movenpick?

Hii kitu is bound to fail...hivi kuna mtu anayo website yao?
 
Sanctus Mtsimbe,
Mkuu wazo zuri sana lakini kitu kimoja tu.. Ulipoweka kiingilio, hii kidogo haikukaa sawa..

Ni muhimu sana kwa chombo kama hiki kujaribu kuvuta watu ktk mkutano wake wa kwanza hasa ikiwa unafanyika nyumbani Tz. Unapoweka kiingilio una limit nafasi na kuondoa uwezekano mkubwa wa kufanikisha kikao cha kwanza.

Mzalendo Mkandara kwa maoni yako juu ya Kiingilio. Bahati mbaya maoni yako yanakuja baada ya Waraka wa Kiini (Concept Paper), kujadiliwa kwa karibu takribani mwaka mzima likiwepo suala la kiingilio.

Kihistoria TPN toka awali ilijiwekea makakati kwamba si jambo jema sana kutegemea Donors kwani watakufanya ushindwe kuwa huru kunapokuwa na mambo ya kukinzana na hao donors. Pili TPN kama advocate wa kujiwezesha kiuchumi si vema sana kutegemea donors. Msingi huu umekuwa ndo msingi mkuu katika uendeshaji wa TPN tokea ilipoanzishwa mwishoni mwa 2007. Kwa hiyo hata katika Kongamano hili TPN yenyewe ndiyo inagharamia kupitia michango ya washiriki wa hili kongamano.

Awali kuweza kumudu gaharama zote, tulifanya kiingilio kiwe TZS 150,000, lakini baada ya wanachama na wakereketwa kujikamua zaidi tukaona ni vema tupunguze kiingilio na kurekebisha mambo fulani fulani.

Tusigeweza kuweka kiingilio bure wakati chakula, maji na chai za saa nne na saa kumi, ukumbi, PA system nk peke yake ni US $ 35 kwa mshiriki.

Lakini niseme pia kuwa TPN haijafunga milango milango, kama kuna mtu ana nia ya dhati ya kuja kuhudhria Kongamano lakini hana ada ya ushiriki basi tunaomba awasiliane na TPN. Bado tunao wanachama wakereketwa na sponsors wa ndani ya TPN ambao nina uhakika wanaweza kuwalipia.

Lakini ni vizuri kutambua kwamba mikutano hii ina gharama, na gharama lazima zichangiwe. Tukumbuke kwamba ghrama za mikutano haziishia hapo, kuna gharama za makabrasha ya mkutano, vifaa vya kuendeshea mikutano, matangazo, mawasiliano na watu mbalimbali km wawezeshaji na hata wakereketwa wachache sana ambao wasaidia gharama fulani fulani.

Pia lengo la mkutano huusiyo kuwa na namba kubwa ya ushiriki, bali ni utayari wa washiriki kuleta mabadiliko kwa wao wenyewe na wanataaluma wengine. Kama mwana taaluma wa kawaida ataona hiyo hela ni kubwa sana hawezi, basi kwa kweli 'we have a long way to go'.

TPN inategemea kama kuna watakaotaka subsidies wawe wanafunzi, na wale walioko kwenye transition ya between school and jobs. Lakini wako wapi wanataaluma wote hawa tunaokutana nao kwenye vikao vya harusi? kwenye kuvunja kamati? kamati za kipa imara na gradutaion? kwenye vijiwe vya rose garden n.k hawa walioshika nafasi tayari ambao wakiwa na right attitude watawachangia wale wasio na uwezo?

Hakuna maendeleo ya kweli ya kujitegemea kwa kupitia subsidies, hebu tusaidiane kutiana changamoto ili ili liwe wazi kwa wengi.

Ni wazo zuri sana kuunda Taasisi hii, lakini ikiwa serikali yenyewe haitambui umuhimu wa Taasisi hii sioni sabau kabisa ya kujaribu kuitongoza serikali. Taasisi zote za Diasporas huanzishwa kwa baraka za serikali zao na ukweli ni kwamba serikali nyingi hujaribu kuuza hoja hii kwa wakazi wake nje badala ya wakazi wa nje kujikusanya wao wakaanzisha chombo hiki ama kuishawishi serikali, jambo ambalo naliona hapa.

Mzalendo TPN ni tasisi ambayo ipo tayari ambayo ina malengo yake na kubwa likiwa ni Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa kutumia nguvu ya akili (Power of the Brain). TPN inaamani kuwa Wanataaluma na Wasomi tunayo nafasi ya kuleta maendeleo hasa kwa watu binafsi bila kuilalamikia serikali kwa kufanya sehemu yetu.

Tunatambua kuwa Serikali inatambua kuwepo kwa TPN na kwa kupitia shughuli mbalimbali ambazo viongozi wa serilkali wameshiriki na pia hata watumishi wa serikali kuwa ama wanachama wa TPN ama wafuatiliaji wa TPN.

Katika mkutano huu, vimealikwa na bado vinaendelea kualikwa vyama mbali mbali vya kitaaluma ili kuweka nguvu ya wanataaluma wengi.

Na kulingana na mfumo mzima wa Utandawazi, hawa Diaspora ndio huwa importer wa asilimia kubwa ya mali zinzotoka nchini kwao..Hawa ndio mabalozi wa Uchumi wa nchi zao wakiuza bidhaa hadi culture yao. Leo hii hatuna sababu kabisa ya kupeleka Korosho zetu India ambao wana soko Marekani hali meneja wa masoko ktk shirika la Marekani ni Mtanzania...

Acha mbali kuwa na meneja, wapo Watanzania wanafahamu mashirka yanayo agiza Korosho toka India. Hatuan sababu kabisa ya mali yetu kupitia India ili ipate soko Marekani..Huo ulikuwa wakati wa vita baridi..Ukuta wa Berlin kiuchumi umeisha vunjwa wazee wetu..

Leo hii wapo Watyanzaniua wenye madini husafiri hadi Thaioland na China kuuza vito vyao kwa walanguzi China hali tunao Watanzania wanaoweza kuifanya kazi hiyo na kwa malipo mara mbili..Mbali na hayo, masomo ya juu ktk University na kadhalika ni vyama hivi huwawezesha wananchi wake kupata nafasi nchi za nje kirahisi zaidi na kwa gharama ndogo ktk exchange programs acha mbali Matibabu ktk Hospital na Zahanati..

Wakati umefika serikali yetu ikome zile fikra za Kijamaa na kikorosho..Diasporas ni win win situation, kwa msemo wa Kikwete!

Mzalendo, hoja yako hapo juu, ni moja ya sababu ni kwa nini TPN na wadau wengine wameandaa kongamano hili. Karibuni tuweke mikakati ya vitendo.

Mkuu nitakuwepo ktk mkutano, nikijaliwa - Inshaallah!

Mzalendo karibu sana. Unaweza kuwasiliana kupitia contacts zilizotolewa na utatumiwa Registration Form na Concept Paper.

Mwisho, kwa yeyote mwenye hoja za kimsingi na ana nia ya kweli ya kushiriki lakini hana uwezo wa ada ya ushiriki tafadhali tuwasiliane.

Na kwa wale wenye vipaji vya kuongea na kushawishi, Speakers, pia wanakaribishwa.
 
Ijumaa nishai

bora wangefanya Jumamosi...asubuhi mnaenda kwenye mkutano mpaka time ya Lunch kisha mchana haoooo mnarudi kubadilisha nguo kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zingine

Ijumaa kama unavyojua Dar na ile foleni nani atakuwa na muda wa kwenda kwenye mambo ya diaspora?

Pili kwa nini wasingechukua ule ukumbi wa BOT au pale Movenpick?

Hii kitu is bound to fail...hivi kuna mtu anayo website yao?

Mzalendo GT;

Siku hii ya Ijumaa imefikiwa baada ya majidaliano ya kina na muda mrefu. Huenda ungekuwa katika kamati pia ungeliafiki.

Kongamano hili si la second priority kiasi cha kuweka katika siku ya Jumamosi. Kama kuna Wazalendo wako serious na kweli wanaguswa na maendeleo ya nchi yao basi siku si hoja. Hata hivyo nikubaliane na wewe si kila mtu anweza kuona umuhimu wa Kongamano hilo. kama ulivyoainisha kwa yule ambaye atataka kuwahi foleni, definetely Kongamano si priority yake.

Kuhusu ukumbi, tumechagua ukumbu kutokaana na convenience na budget. kama nilivyoeleza hapo juu, TPN inajitahidi kuendesha mambo yake bila kutegemea sana wafadhili. Hivyo kwa hili, baada ya analysisi kufanyika, makubaliano yalifikiwa tufanyie katika venue iliyotajwa: Golden Tulip.

Kongamano hili aliwezi kufail. Tayari kuna baadhi ya washiriki toka nje ya nchi ambao wemeshaanza kufika na pia washiriki wandani. wawezeshaji wapo tayari na vyama mbali mbali vya kitaaluma vinaalikwa na wanaendelea kuthibitisha kushiriki.

Ninachukua nafasi hii kuwaomba wale viongozi wa vyama vya kitaaluma wanaopenda kushiriki tuwasiliane kwa mipango zaidi.

Website: www.tpntz.org

bado inaendelea kuboreshwa na kuwa updated.

karibu sana GT tuje tupeane mikakati.
 
Hii mada yenu (TPN) inachekesha sana:
Mada: Namna Wanataaluma Wanavyoweza Kuchochea Maendeleo
.....and that's it!

Watakaochangia mada mtawaorodhesha lini?
Wakihudhuria watu 300, makusanyo ni 15,000,000. Where does this money go?

SOURCE: http://issamichuzi.blogspot.com/2009/11/kongamano-la-wanataaluma-waishio-ndani.html#comments

Lazy Dog; unaweza ukapata concept paper. iandikie TPN: president@tpn.co.tz. Kuna mengi sana ambayo utayaelewa. Si rahisi katika tangazo kuweka mambo yote.

Kutakuwa na Makabrasha ya Mktano pia ambayo yameorodhesha Speakers wote ambao ni wazuri sana na kutakuwa na Interventions pia.

Idadi ya mahudhurio si hoja. Hoja ni ubora wa Kongamano. Hata hivyo kwa taarifa ni kuwa gharama za mkutano tayari ni kubwa kuliko mapato yanayotarajiwa. Kuna wanachama na wakreketwa mabo wamejitolea.
 
Tanzania Professionals Network (TPN)

Nyumbani Ni Nyumbani 2009

Kongamano la Wanataaluma Waishio Ndani na Nje ya Nchi

Mada: Namna Wanataaluma Wanavyoweza Kuchochea Maendeleo

1.Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara

2.Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao

3.Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.

4.Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini

5.Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi Wake

6.Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua Za Kuleta Mabadiliko Na kwa Namna Gani?

7.Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka/

Siku na Muda:

Ijumaa; 18th December 2009; Saa 2.00 Asubuhi -11.00 Jioni

Mahali:

Golden Tulip Toure Drive, Msasani Peninsula

Washiriki:

Wanataaluma na Wasomi Wote Wazalendo Mnaombwa Kufika Bila Kukosa

Ada ya Ushiriki:

TZS 50,000 (Kwa ajili ya Ukumbi; Chakula; Tea na Snacks, PA, Documents nk)

Angalizo:

Viongozi wa Vyama Vya Kitaaluma na Wanataaluma Wanaharakati wa Maendeleo Walioko Mikoani Wamewekewa Nafasi Zao na Watalipiwa Ada ya Ushiriki; Tuwasiliane. Huu si wakati wa Kulaumu. Kama Umeguswa naMada, usikose kuja Kutoa Mawazo yako.

Kujiandikisha na Maelezo Zaidi:

0715 740 047 ; president@tpn.co.tz; www.tpntz.org

Waandaaji: TPN – Costech - TSN– OUT – UDSM - Serikali
 
Waandaaji: TPN – Costech - TSN– OUT – UDSM - Serikali

Santu

Mimi nitakuja [inshallah]; ila uwe wazi kwamba 50K is way high kwa huduma za tulip labda kama mnataka kulipata posho kama akina mwakyembe

Nitakuja na naomba kama unaweza nitumie concept paper
 
Santu

Mimi nitakuja [inshallah]; ila uwe wazi kwamba 50K is way high kwa huduma za tulip labda kama mnataka kulipata posho kama akina mwakyembe

Nitakuja na naomba kama unaweza nitumie concept paper

Mzalendo MTM;

Salaam Sana. Naomba Uni-PM Email yako nitakutumia Concept Paper.

Kuhusu Fees Mkuu, hakika gharama za Mkutano ni zaidi ya hiyo TZS 50,000 na tunawashukuru baadhi ya Wazalendo ambao wamejitoa zaidi kufanikisha hili. Unaweza kwa haraka haraka ukafanya makisio ya haraka uone gharama zitakuwa kiasi gani kwa vitu vichache tu kama:

  • Conference Venue for a Full 1 day including refreshments and lunch
  • PA System
  • LCD Projectors
  • Presenters Allowances
  • Closing Ceremonies Refreshments
  • Publicity and Promotional and Conference Materials
  • Media and Publicity: Radio; TV; Newspapers
  • Preparations costs, transport, Postage and Communications and Logistics
  • Security Arrangements
  • Decorations
  • Participants Certificates, nk
 
Mkuu Msimbe, kwanza naomba nikupongeze kwa mda na resources zako ambazo umeinvest katika matayarisho ya hii shughuli. Tangu uweke hili tangazo mwanzoni mwa mwaka..mpaka leo..inaonyesha ni jinsi gani ulivyo mfuatiliaji wa mambo. I can only say. Splendid. Usiwasikilize wanaokwambia kwamba this thing is bound to fail. JAMANI ni ulimwengu upi utapata vya bure? Its a shame kuona kwamba mpaka leo tunatumia umaskini wa wananchi wenzetu (maana wanaokuja humu JF uwezo wa kulipa 50k WANAO) Kujustify arguments zetu. Harafu sielewi kwa nini mpaka leo..watu tupende kufanyia kila kitu katika CBD..jamani mji unapanuka....we ought to go out..infact next time it should be Bagamoyo au kwingineko.

Ni changamoto kubwa kwetu wote (tuliokwenda shule) kwamba we should reach a point tuache kulalamika. Maendeleo ni sisi wenyewe. Kwa kweli naamini hii initiative ni mwanzo tuu. Its something which we should all be proud of. Only kuwepo na TRANSPARENCY NA ACCOUNTABILITY. I will be onboard!

LAKINI ushauri wangu ingekuwa vyema mkawa consistent in whatever you do. Tatizo kubwa tulilonalo sisi wananchi especially watanzania..ni kufanya mambo na kuishia njiani. Kama kweli mmedhamiria..ningewashuri mjenge structures za hii kitu kwamba hata kama wewe haupo..itaendelea kufunction.

Mkuu, kwa bahati mbaya mimi sitohudhuria kwa sababu ya majukumu yaliyoingiliana. Lakini naomba niwatakie kheri kabisa katika huu mkutano na ni tegemeo letu kwamba next year, tutaweza kujumuika. Inshallah.

Kama utaweza nitumie concept paper. na paperz za presenters.

Masanja,
 
Tanzania Professionals Network (TPN)

Nyumbani Ni Nyumbani 2009

Kongamano la Wanataaluma Waishio Ndani na Nje ya Nchi

Mada: Namna Wanataaluma Wanavyoweza Kuchochea Maendeleo

1.Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara

2.Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao

3.Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.

4.Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini

5.Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi Wake

6.Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua Za Kuleta Mabadiliko Na kwa Namna Gani?

7.Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka/

Siku na Muda:

Ijumaa; 18th December 2009; Saa 2.00 Asubuhi -11.00 Jioni

Mahali:

Golden Tulip Toure Drive, Msasani Peninsula

Washiriki:

Wanataaluma na Wasomi Wote Wazalendo Mnaombwa Kufika Bila Kukosa

Ada ya Ushiriki:

TZS 50,000 (Kwa ajili ya Ukumbi; Chakula; Tea na Snacks, PA, Documents nk)

Angalizo:

Viongozi wa Vyama Vya Kitaaluma na Wanataaluma Wanaharakati wa Maendeleo Walioko Mikoani Wamewekewa Nafasi Zao na Watalipiwa Ada ya Ushiriki; Tuwasiliane. Huu si wakati wa Kulaumu. Kama Umeguswa naMada, usikose kuja Kutoa Mawazo yako.

Kujiandikisha na Maelezo Zaidi:

0715 740 047 ; president@tpn.co.tz; www.tpntz.org

Waandaaji: TPN – Costech - TSN– OUT – UDSM - Serikali

Mkuu Sanctus.........vipi kuhusu live communications na kwenye mkutano.......be it video conference facility, radio or whatever the case may be....unauja tena teknolojia.........haya mambo yanawezekana.....kama hilo halipo basi mlifikirie kwa mikutano ijayo..........
 
Mkuu. tunafikiria mwawili;

Kwanza kama nje ya Nchi kuna watu ambao wanaweza wakaji-organize pamoja na kuwa na Video Conferencing Centre, kuna uwezekano wa Kuwa na Live Video Communications. Tujulishane mapema kwa hilo.

Lapili kama kuna mdau atakuwa ana Bandwidth kubwa ya Kutosha Video Sype Chat, basi pia tunaweza kufanya:

TPN ID itakuwa ni: TPN_TZ
 
Back
Top Bottom