Tanzanians Diaspora Summit on 18th December 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzanians Diaspora Summit on 18th December 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sanctus Mtsimbe, Jan 7, 2009.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  update 1:


  Wana JF; ule muda wa ile Conference yetu umewadia na maendeleo ni mazuri. Kuna mbadiliko kidogo ya Kimsingi:

  Dates:

  Saasa itakuwa ni kwa siku moja tu: Friday 18th December 2009

  Venue:

  Golden Tulip Hotel; Masaki; Dar Es Salaam

  Participation Fees*:

  TZS 50,000

  -----------------------------------------------------------------------------------------------------
  Wana JF na Wazalendo Wenzangu;

  Heri ya Mwaka Mpya wa 2009.

  Moja ya mikakati ya TPN Mwaka huu wa 2009 ni kuitisha Mkutano Mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi na wale waliopo nyumbani mwezi December 2009.

  Mkutano huu unatarajia kuwakutanisha Wanataaluma, Watanzania waishio Nje ya Nchi, Wasomi, Vyama vya Kitaaluma na Biashara nk.

  Wazo kuu la Mkutano huu ni kuihusisha Serikali, Wawekezaji wa Ndani na Nje, Wafadhili na Mabenki katika kujadili na kuainisha mikakati na utekelezaji utakaosaidia Kukua kwa Uchumi wa Tanzania kama mmoja ya jambo muhimu katika kujenga Uchumi imara na endelevu.

  Sababu nyingine ya Mkutano huu ni kuelezea mali na rasilimali tulizonazo na jinsi zinavyoweza kusaidia kuleta maendeleo ya Nchi.

  Pia tungependa kujadili na kubuni mikakati ya jinsi gani Watanzania waliopo Nje na Ndani ya Nchi wanaweza kushirikiana kwa uaminifu wa hali ya juu katika kuendesha miradi na biashara za pamoja ili kujiletea maendeleo.

  Tunapenda mwishoni mwa Mkutano huu, kutoa mapendekezo yetu kwa Serikali na wadau wote ni vipi tunaweza kushirikiana na kwa mikakati ipi kujiletea maendeleo ya Nchi na Watu wake.

  Tayari tulishafanya mazungumzo ya awali na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na pia baadhi ya watanzania waishio nje ya nchi na wengi wanaunga mkono wazo hili. Wengi waishio nje walipendekeza kuwa kwa kuwa mwisho wa Mwaka wengi hupenda kurudi Tanzania kusalimia nyumbani na kufanya mambo mengine ya Kimaendeleo, ni vema tukafanya Mkutano huo Mwezi wa December 2009.

  Tunapenda kukaribisha mawazo zaidi ya kufanikisha Mkutano huu na utekelezaji wa mapendekezo yake.

  Napenda pia kutumia fursa hii kuwajulisha juu ya uwepo wa TPN Chapter huko Marekani na Uingereza.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Wazo zuri ndugu!

  Venue itakuwa wapi? Kwa Obama au kwa Braun?
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo MzalendoHalisi

  Mwelekeo uliokuwepo ni kuwa, ama tufanyie mkutano huu Kijijini kabisa lakini ambapo ni accessible ili pia kupata feeling ya nini kinatakiwa tufanye baada ya kuona hali halisi ya kijijini. Kama wazo hili likikubalika, basi itabidi kuweka mahema ya kisasa kwa ajili ya Mkutano huo.

  Wazo lingine ni kuwa tufanyie DSM ama Arusha. In that case itabidi tufanye katika kumbi kubwa kama AICC, Ubungo Plaza, Sabasaba au Diamond Jubilee.

  Mawazo zaidi yanakaribishwa.
   
 4. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #4
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa watakaopata nafasi ya kuja December 2009, ni wazo jema kama wataonyesha nia yao ya kuhudhuria Summit. Wanakaribishwa.
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...wakati wa ile mijadala ya dual citizen kuna wasio na aibu(majority) waliita watanzania wanaokaa nje ni traitor,wabangaizaji,wazamiaji,unpatriotic etc tena cha ajabu ni wasomi na wengine hata wali suggest kuwa na dual citizen itafanya watumike kama spy/vibaraka,sasa leo vipi wanaona nao kumbe wanaweza kuchangia maendeleo ya taifa?
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sanctusi Mtsimbe,
  Kwanza shukrani kwa taarifa hizi na ningependa kukuhakikishia kwamba tupo pamnoja ila tu nina maswali mawili matatu...
  Kwanza TPN ni chombo gani hiki? nini kirefu chake..
  Pili, Kuna wajumbe ghani wanaowakilisha Diaspora hadi sasa hivi?
  Na mwisho, Agenda zipi zimekwisha tayarishwa ambazo zita husiana na washiriki wote ktk kujadili na kuainisha hiyo mikakati.. Kwa sababu hizi hadithi za mijadala na mazungumzo mengi huwa zinanipa kichefuchefu ikiwa hakuna mikakati ambayo tayari imekwisha tayarishwa...
  Nitakupa mfano mmoja wa Wachina.. Hawa jamaa zetu wamefungua matawi ya benki zao huku na wanapatiwa mikopo ambayo inahusiana na Uagizaji wa mali zao wenyewe kutoka China..Kwa hiyo huyo diaspora ndiye anakuwa importer wa mali zao na ku supply ktk maduka ya rejareja badala ya kutegemea Mr. Smith ambaye kwanza hafahamu kama Tanzania ndio main producer wa Korosho..
  Sasa hivi wenzetu most of electronic Accessories hasa ktk PC na simu zinaingizwa North America na Wachina wenyewe ambao wanaziuza katika mashirika kama Dell na kadhalika..Sisi hapa sijawahi kuonba hata siku moja kitu kinachotengenezwa Tanzania hata iwe Khanga tu.. nakumbuka zamani sana enzi za mwalimu niliwahi kuona mashuka na nakumbuka viatu vya safari boots... Toka hapo sijaona tena zaidi ya maduka ya Watanzania ambao wanaouza rejareja nguo za Kipopo (Nigeria), na vinyago..

  Hata hivyo mkuu wangu panga pangua msinisahau kunipa mwaliko nitapenda sana kuwapanua fikra jinsi wenzetu wanavyofanya..
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Sanctus Mtsimbe:

  Wengine tumesharudisha kadi za chama, je bado tunahesabiwa kama Diaspora ?

  Vilevile je kuna mafanikio gani mpaka sasa au ni-get together kama za kawaida?
   
 8. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  I am with you man but we need to be serious. This is a bright idea and hope most people will join in.

  On location issue, my opinion is to host the first meeting in one of the city, (Dar, Arusha, ATL, London, Mexico City, Abuja, New Delhi or any other city) and later on once we are well organized, groups can send delegates to the venue and other can use technology, video conference.

  Just throwing ideas around but we can definately DO THIS.
   
 9. K

  Koba JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  RWANDA Diaspora

  BY EDMUND KAGIRE
  NYARUGENGE - The Rwandan Diaspora together with the National Bank of Rwanda (BNR) have finalised plans to establish an investment fund by Rwandans living in the Diaspora that will be fully operational by March this year.

  The fund, known as the Rwandan Diaspora Mutual Fund (RDMF) fine tuned and adopted by the 2008 Diaspora Retreat last month, is a pool of funds to be created by Rwandans abroad to empower and mobilise themselves to invest in their home country through remittances as a way of contributing to national development.

  Presenting the current progress of the fund to BNR and the Ministry of Foreign Affairs (MINAFETT), the RDMF Promoting team consisting of Rwandans living in Diaspora, revealed that the mutual fund, supported by the majority of Rwandans in the Diaspora, will be fully established in March 2009.

  “This initiative is an indicator that Rwandans in Diaspora have moved from talking to concrete actions. It is purely a business initiative that will yield very great returns to investors and our motherland,” said Providence Bikumbi Newport, the head of the Promoting Team.

  The fund is aimed at promoting the financial well being of the Rwandan Diaspora while participating in the socio-economic development of their country instead of investing outside Rwanda.

  The idea was conceived during the 2007 Diaspora retreat but never took shape until the 2008 retreat where it was agreed that such a fund if created, would not only benefit the economy but also the economic lives of Rwandans in Diaspora and their families.

  Speaking at the press conference, the BNR Governor Francois Kanimba re-assured members of the Diaspora that the National Bank in conjunction with the Capital Markets Advisory Council (CMAC) are ready to provide all the necessary support required during the establishment and investment of the fund.

  “We appreciate the fact that Diaspora members have now agreed to shift from words to actions. This idea is very welcome and we will always come in to help at any moment,” said Kanimba.

  After its establishment, the Mutual Fund will be invested in Treasury Bonds, guaranteed by BNR and at a later stage the interest gained from the bonds will be invested in higher risk products such as corporate bonds and stocks though it is also expected that the fund will be invested abroad in the long run, to earn more interest which will then be repatriated back to Rwanda.

  The fund will be monitored and controlled by the Diaspora General Directorate in MINAFETT together with the Central Bank and CMAC to ensure that its is properly used and that owners of the fund receive their dividends and returns on the amount of money each invested.

  “This is entirely a business idea for Rwandans in Diaspora that is aimed at mobilizing them to invest their money in their home country and earn from their investment while benefiting the economy,” added Bikumbi, a resident of Canada.

  The Promoting Team is set to embark on a mobilising campaign across the globe that will see an estimated million Rwandans living in the Diaspora convinced to invest their money in Rwanda other than investing it abroad.

  According to the Director General of the Diaspora General Directorate, Robert Masozera, the ministry has planned several conventions and international conferences across the globe aimed at mobilising Rwandans to invest in the country.

  Among other things, the directorate launched a Diaspora website which will be used as a link for Rwandans in the Diaspora to network, while Rwandan embassies across the globe have been encouraged to sensitise Rwandans in their particular countries.

  The government of Rwanda has developed a comprehensive plan to involve the Rwandan Diaspora in the development process through remittances and profit repatriation as one way for the country to reduce on overdependence on foreign aid.

  According to Kanimba, remittances from abroad reached an estimated $150m in 2008 compared to $103m the previous year.

  “Those are the figures recorded officially through recognised money transfers and Forex Exchange but we imagine it could have gone beyond that. We are developing a new strategy to monitor remittances as they come in so that we know what exactly came in” added Kanimba.

  In the same development, Banque de Kigali allowed zero money transfer costs on remittance transfers as an incentive towards the creation of the Fund, a move highly welcomed by Diaspora members.

  Ends
   
 10. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #10
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu Koba;

  Sijui source ya information zako au ni nani hao unaowazungumzia. Hata hivyo Beliefs na values za TPN zinaelezea wazi jinsi Watanzania walioko nje ya Nchi wanavyopasa kuthaminiwa na mchango wao mkubwa wanaotoa. Dual Citizenship Idea inakubalika ndani ya TPN.

  So, we can make it as one of the key agenda.
   
 11. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #11
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  TPN ni chombo kinachounganisha Wanataaluma wote wa ngazi zote na kirefu chake ni Tanzania Professionals Network. Kwa maelezo zaidi tafadhali rejea thread hii: https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/15629-jamii-forums-karibuni-tanzania-professionals-network.html

  Mzalendo, sasa hivi ndiyo tunataka kuanza maandalizi. Kila aliyepo Diaspora mwenye uwezo wa kuhudhuria Summit anakaribishwa.


  Kiongozi, madhumuni ya Thread hii na consultation zingine zinazoendelea ni kuwashirikisha Wadau katika maandalizi ikiwa ni pamoja na kuchangia mawazo. Je, unaweza kuona dokezo za ajenda katika postkuu hiyo hapo juu?

  Ndugu yangu Mawazo yako ni Mazuri sana na ninapendekeza hili nalo tuliweke katika Summit na kuangalia maeneo yote ambayo Watanzania in Diaspora wanaweza kusaidia nchi kuanzia Tanzanite, Utalii, etc etc.

  Mkuu, post hii ni Mwaliko. Baada ya kupata maoni ya wadau wengi wa Ndani na Nje, Kuanzia Mwezi April 2009, Official communication zitaanza. Kwa sasa inatosha tu kuelezea nia yako. Pia unaweza kuwasiliana na ofisi ili kuweka interest yako katika records.
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mtsimbe nakupongeza kwa constructive idea ya kufanya hiyo event.
  TPN mpaka sasa mmefikia wapi kwenye ule mfuko wa kuwawezesha vijana wasomi?
  Nilikuwa napenda kujua status na challenges mnazoface katika kumobilize hiyo fund.

  Vipi so far kuna bank yeyote nchini au taasisi iliyoonyesha ari ya kuunga mkono wazo la kutoa mikopo kwa vijana through their business idea as collateral and then waanzishe biashara na kulipa???
   
 13. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #13
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kiongozi Zakumi . . . . kwanza Salaam sana. Bado nakukumbuka.

  Nadhani tukiongelea Diaspora tuna maana Watanzania Waishio Nje ya Nchi. Wanachama wanaweza kuwa ndani au Nje ya Nchi. Haijalishi.

  Mafanikio yapo mengi ikiwa ni pamoja na kuandaa: Networking & Economic Empowerment Seminars kama

  - Mentorship & Practical Entrepreneurship
  - Financial Empowerment for Professionals
  - Business Networking & Sharing of Investor Contacts Professionals
  - Microfinance for Professionals, etc etc
  Katika Seminars hizi CDS na Hardcopies huwa zinatolewa.

  Pia kuna wengi ambao kupitia TPN wameweza kuungana na kuanzisha makampuni yao na kupata Mitaji. Mfano:Fortune Property a Real Estate Compnay ambao waliweza kupata mtaji wa zaidi ya TZS 50 Million. Sasa hivi Fortune wameweza kununua 2 Property/Plot Mikocheni na kufanya mambo mengine mengi.

  Kuna makampuni mengine pia yameanzishwa yakiwepo ya Kilimo, Muziki nk. Kila mara katika Mikutano yetu Wadau mbalimbali wanapata fursa ya kupresent business idea na kuanzisgha makampuni.

  Pia tulituma wajumbe kuhudhuria China-Africa Business Meeting huko Arusha na Sullivan Summit ambako tulijifunza mengi.

  Pia tumeweza kufungua Chapter Arusha, Tanga, Dodoma, USA na UK na mikakati ya kufungua sehemu zingine inaendelea.

  Pia tumeanzisha TPN Fund.

  Mwaka huu tunaanzisha Award ya Mtanzania aliyefanya vizuri. habari zaidi pata hapa: https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/16002-tuzo-kwa-mtanzania-aliyefanya-vyema.html.

  Get together? . . . . Mwaka huu tutafanya Mwisho wa February 2009
   
 14. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #14
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Tatu, asante sana.

  Juu ya sehemu ya kufanyia Mkutano maoni ya kuwa Watanzania wengi waliopo Nje hupenda kurudi nyumbani kwa likizo nk miezi ya Mwisho wa Mwaka. So, tunaweza kufanyia DSM au Arusha.

  Nashukuru kwa wazo zuri. Tutaangalia uwezekano wa kutumia Technology kama Conference Call na Video Conferencing.
   
 15. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #15
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Koba;

  Ubarikiwe sana. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Wenzetu. Tanzanians as well we can do that.

  Jamani tuunganishe nguvu zetu.
   
 16. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #16
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kiongozi Nyauba . . . Asante sana.

  Mfuko umeshaanzishwa rasmi baada ya Resolution ya AGM iliyofanyika mwishoni mwa August 2008. Unaeza kusubscribe katika hiyo fund pia. Ni kweli tunazo challenge za kumobilize fund. Hata hivyo hiki chombo kinajitegemea ingawa ni Mtoto wa TPN. kama una mawazo ya kuboresha unakaribishwa Mzalendo.

  Bado benki zetu hazikubali kuwa Business Ideas ziwe Collateral na ndiyo maana tunataka tuyaalike mabenk katika Summit. Hata hivyo kuna mabenki matatu ambayo CEO's wamekubali kufanya mazungumzo kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana nasi.
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sanctus,

  Hongera kwa wazo zuri sana. Ushauri tu ni kwamba jaribuni kuanza na malengo machache na madogo ambayo mnaweza kutekeleza na kisha kusonga mbele. Watanzania ni wagumu sana, mnaweza kutumia muda mwingi kufanya conference kubwa kama hii lakini siku ya siku msipate hao Diaspora.

  Balozi wetu wa UK anaweza kukupa ushauri mzuri sana kuhusu Watanzania. Amefanya juhudi nyingi na pia nafikiri ameweza kutuelewa sisi Watanzania, longo longo nyingi lakini matendo anajua mungu.

  Kama wananchi wanaona kuna mafanikio watakuja tu na kujiunga. Ndio maana ni muhimu kuanza na vile vitu ambavyo kila mtu anaweza kuona faida yake kwa macho yake.

  Mafanikio mema, kama nitabeba boxes za kutosha mwaka huu, ningependa kushiriki.
   
 18. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #18
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Mtanzania; Salaam sana. Bado nakukumbuka.

  Kama ulivyoshauri at TPN we are taking one step at a go na tunafanya kile kitu ambacho tunadhani tunakiweza.

  Tunachofanya sasa hivi ni kupata maoni kwanza na kufanya survey ya idadi ya wale watakaoweza kuja. Tutaanza Registration Mapema sana ili by June 2009 tuwe na uhakika na mwelekeo ulivyo na kisha tuamue cha kufanya.

  Ni kweli baadhi ya Wanataaluma wetu bado wana longolongo nyingi hata kwa mambo ambayo yana faida ya moja kwa moja kwao. Tulipoonana na Minisdtry of Foreign Affairs walitueleza mengi juu ya Diaspora Meeting ya London na hata resolutions zake ingawa sijawahi kusikia mikakati ya utekelezaji.

  Mtanzania, the road to Success sometimes is very hard and full of challenges. Na challenge moja kubwa ambayo bado tunayo ni attitude ya watu wetu katika mambo mbalimbali.

  Njoo December 2009 Mzalendo Mwenzangu, I believe it might be the beginning of a New Era. Karibu sana Mkuu!
   
 19. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka Sanctus,

  Nshukuru kwamba umeweza weka jamvini hili jambo ili kupata mawazo ya wana JF. Ni jambo jema kwa maendeleo ya individuals na Taifa kwa ujumla na i trully believe that Watanzania tunaweza fanikisha hili as long as we put our mind, true dedication and efforts katika kulifanikisha.

  Tutakuwa pamoja mpaka mwisho kuhakikisha mafanikio ya kweli...
   
 20. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #20
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Mzozo wa Mzozo;

  Asante sana kwa kuunga mkono jambo hili.

  Naomba tu niweke wazi kuwa sisi sote kama Wazalendo halisi wa Tanzania tulalo jukumu la kusaidia kuleta maendeleo yetu pale tunapoweza. Ninayo imani kubwa sana kuwa uwezo huo tunao, challenge tuliyonayo ni vipi tunaweza kufanikiwa.

  Siamini sana kama kweli Foreigners ndiyo wanaoweza kuleta maendeleo ya Nchi hii. Tunao vijana wetu nje ya nchi, wengi tu na wengine wana mafanikio makubwa huko waliko ila hawana imani sana na ku-Invest nyumbani kutokana na karaha mbalimbali k.m. Kero za mfumo wa kuanzisha biashara na suala zima la kodi hasa Exemptions za Kodi, Mitaji, Utapeli wa baadhi ya partner wa TZ, kuna wengine ambao wamekuwa wakituma pesa nyumbani kwa ajili ya ujenzi au biashara lakini wametapeliwa, kuna wengine hawana watu wa kuwaamini kufanya nao biashara, kuna wengine wana pesa lakini hawajui nini wafanye nk.

  Tunahitaji kukaa chini na kusemezana wenyewe . . . hakuna mtu atakuja kutusaidia kwa hili. Kuna baadhi ya foreigners wanaona loopholes nyingi sana na wana-take advantage kwa kuwa wanatuona kama tumelala usingizi.

  Asante sana ndugu yangu kwa kuunga mkono, tutafahamishana jinsi mipango inavyokwenda.
   
Loading...