Hii ishuu tusiichukulie kishabiki sana. Marekanikwanza ni mpinzani mkubwa wa Kanisa Katoliki, pili ubaguzi wa rangi haujaisha. Ukisoma vizuri habari utagundua kuwa Solomon Bandiho aliteuliwa kuwa paroko (Parochial Administrator) wa Mesa. Kwa wazungu hata hiyo nafasi kupewa mtu mweusi tena wa kuja inawauma. Ndiyo maana unaona ni kama mbinu ilifanywa ili kumkomoa. Yupo padri mwingine alikuwa mshauri wa papa Paulo wa II na papa Benedict wa 16 aliamua kujiuzulu kazi ya ushauri na kurudi Bukoba baada ya kutegeshewa madawa ya kulevya akaruka hicho kiunzi, kila akishika simu au kompyuta anapigwa shoti. Alitoka Roma kwa ulinzi mkali na aliwaambia ndugu zake ametoka huko kwa ajili ya kulinda usalama wake na alijiapiza kutorudi Ulaya kamwe. Hivyo ishu ya Solomon tuitazame kwa macho mawili. Mpaka sasa hatujui kesi yenyewe inakwenda vipi na imeishia wapi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.