Tanzanian journalists for sale? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzanian journalists for sale?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Sep 6, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asalaam Aleykum,

  Taarifa nilizokuwa nazo ni kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeunda kamati
  ya propaganda kwenye kampeni za uchaguzi inayo ongozwa na PRINCE BAGENDA
  akisaidiwa na MUHINGO RWEYEMAMU.

  Kamati hii ndiyo inayofanya kazi za kumchafua Dk. Willibrod Slaa kupitia magazeti na waandishi walionunuliwa na CCM.

  Magazeti haya yakiandika habari za ndoa ya Slaa au taarifa zozote za uzushi, basi hununuliwa nakala zote na CCM na kugawiwa bure kwenye mikutano ya chama hiko.

  Pia, CCM imekuwa inaongoza kwa kutoa rushwa kwa waandishi wa habari kwenye kampeni zao. Posho ambayo CCM inatoa kwa waandishi wa habari kwenye kampeni zao ni zaidi ya mara mbili ya posho inayotolewa na vyama vya upinzani.

  Vifuatavyo ni viwango vya posho (daily allowances) ambazo timu za wagombea wa Urais zinatoa kwa waandishi wa habari:

  1. Jakaya Kikwete (100,000/-)
  2. Dk. Willibrod Slaa (45,000/-)
  3. Prof. Ibrahim Lipumba (40,000/-)

  Waandishi wa habari wote sasa hivi wanakimbilia kuwepo kwenye timu ya kampeni ya Kikwete kwani huko ndiko kwenye pesa nyingi. Wanalipwa milioni 1 kwa siku 10 tu.

  Hii ndiyo maana kuwa wamekuwa wakitumwa na CCM kuandika habari za kumpamba JK na mwandishi anayeandika habari tofauti na matakwa ya CCM anatimuliwa kwenye posho.

  Kulipwa posho kwa waandishi na vyama vya siasa ni kinyume kabisa na maadili ya uandishi wa habari na ni ishara kuwa waandishi, wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania wananunulika kirahisi.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Go to hell Journarist
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Huwa najua waandishi wa habari makini wapo Mwananchi, Tanzania Daima, Raia mwema na Mwanahalisi tu. Hayo ndo magazeti ambayo huwa naweza kuyanunua. Siwezi hata siku moja nikanunua magazeti ya udaku kama habari leo, Rai, Mtanzania na Changamoto. Katu siwezi kuyanunua magaezeti hayo, iwe ni wakati wa uchaguzi au siyo.
   
 4. moto ya mbongo

  moto ya mbongo JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 336
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  We King Of Kings unasema to hell with Journalists!je unajua kuwa CCM wana nguvu nyingi kwa kuwa ni wakongwe na wanatia sumu profession ya Journalism 2005 waliichukua HABARI CORPORATION iliyokuwa na magazeti makini kama RAI,MTANZANIA wakaweka mambo yao pale ili choko choko za ukweli zipungue siku hizi hayo magazeti ni utumbo mtupu wanayaendesha kwa hela za ROSTAM sio kwamba yanauza kwa kufikia rekodi ya miaka ile.

  Sasa tunapopewa taarifa kama hizi kwa kweli ni kubaka fani hiyo na wenye fani wawe makini hizo pesa zitawafanya wawe watumwa wa CCM milele.naishia hapa
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Tukija kuchukua sheria mkononi tusilaumiane..................pesa za epa bado zingali hewani zinzendelea kututesa kila kukicha......yaani professionalism imekuwa compromised na tuposho twa mwezi mmoja....haki ya nani hao waandishi wanasubiri huruma ya jk na baadaye watahamishiwa tbc ili kuendelea kusambaza propaganda zao.....
  Mungu tuepushie hili balaa....
   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KINGS OF KINGS:
  Kwani wanasheria wetu wanatuambiaje kuhusu sheria ya media hapa tanzania

  PART VII
  GENERAL PROVISIONS
  Duties of
  Government
  media
  Cap.343
  28.-(1) The candidate for the Office of the President in
  an election shall have the right to utilize the Government
  broadcasting service and television during the election campaign,
  in accordance with the provisions of the National Elections Act.
  Election Expenses
  22
  (2) The Government media shall include in their
  publications information related to the electoral process without
  bias and such publication shall not tamper with information or
  discriminate against any candidate.
  Sasa sijui tunalalamika nini hapa bado niko kwenye giza kwasababu media za serekali zinampa nafasi zaidi aliyeko madarakani au vipi.

   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Si unajua kusema/kuandika ni kitu kimoja na kutenda ni kitu kingine.............yameandikwa sawa lakini utendaji wake ndiyo huu...tuwafanye nini hawa mbwiga?....ndiyo maana hata kikwete alisaini kwa mbwembwe muswada kuhusu gharama za uchaguzi na yeye mwenyewe anaenda kinyume chake akiwekewa pingamizi anatafuta pa kukimbilia kwa kutumia wale aliowaweka na ambao ndio watekelezaji wa sheria yenyewe.....yamneandikwa kwenye makaratasi ila matendo ni tofauti ..........
   
 8. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna tatizo kubwa sana kwenye media hapa nchini. Inabidi Barala la Habari lifanye kazi ya ziada kubadili mwenendo huu wa kijinga unaoendeshwa na wanahabari wetu. Magazeti kama Habari Leo na Mtanzania hivi sasa kwishney! Sijui kama bado kuna watu wanayanunua. Nasikia yanagawiwa bure na kwenye kampeni za CCM. Ni aibu kubwa sana. Naambiwa kwamba Mhariri wa Habari Leo ni mla rushwa mkubwa na ananunulika kirahisi sana. Kwa upande wa gazeti la Mtanzania, wote tunajua kwamba linamilikiwa na fisadi papa Rostam Aziz. Huyu anapigana kuhakikisha kwamba Dk Slaa haingii Ikulu kwa sababu ndio itakuwa mwisho wake. Atalazimika kufungasha na kurejea kwao Iran baada ya kufilisiwa mali yote aliyowaibia Watz.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kuna mambo ya Hovyo ambayo waandishi wanafanya , yanawadhalilisha saana, wanatia kinyaa.
  ile dhana ya kua WAANDISHI WA HABARI NA SEKTA YA HABARI NI MUHIMILI MWINGINE wa dola ni dhana mfu kabisa hapa Tanzania.
  kweli leo waandishi hawa wa Mtanzania , Jambo Tz, Rai, na wapuuzi wengine wakariba yao, wanaweza kuja kuandika habari za kukemea jambo fulani kisha wakasikilizika.
  sijui kama ni matokeo ya elimu ndogo, ama ni elimu iliyochakachuliwa kwa vyeti fake ama wizi wa mitihani ? ama niukosefu wa bodi yakusimamia maadili yao ambayo itawabind hawa jamaa kisheria bindi inapodhihirika waandishi wamenunuliwa.

  Binafsi Uhuru , Mzalendo na Radio Uhuru ni bora wanamaadili na jukumu lao ni kupiga kampeni ya ccm, Sasa hawa wamevuka mipaka, ni zaidi ya kampeni, hawa wanapiga vita Ustawi wa demokrasia, katika kuweka mazingira mazuri ya mafisadi kuishi Tanzania.

  sioni tofauti ya mambo ya waandishi wa Kitanzania na ujinga wa kina Mangungo.
  wao wahujumu harakati za haki za kidemokrasia , ili kuwafanya waua nchi washamiri na kupendeza.
  Ipo siku , Yana mwisho haya.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  I love my freedom!!!!!!!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  There has never been true journalism in Tanzania....
   
 12. M

  Maluo Member

  #12
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  inaniuma sana inanisikitisha sana kweli utu wetu kwa taifa umefikia hapa nadhani hata hayati mwalimu asingeacha kurudisha kadi ya ccm kweli watu wanakufa hawana dawa mahosipitalini wakina mama wanajifungua hata vyandarua vya mbu hakuna mnaweza kweli waandishi wa habari mkawa peponi kwa kushabikia viongozi wabovu wasiyo na maono wala jipya kisa tshs. 100,000.00 kweli unawajali ndugu zako ama rafiki zako unawajali watu wote kweli ama unanijali wewe mwenyewe waliokomboa tanzania wangekuwa ni watu wenye ubinafsi kama waandishi wa habari kwa kweli ukombozi tusingeuona kabisa
   
 13. M

  Maluo Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wanasheria wetu ni wachache sana wanaweza kujua walisoma nini na kwa nini ni wanasheria kwa kuwa hawa watu huwa wanapenda kujiita learned brother and sisters wakasau kusema few of has who utilize the knowledge for the benefit of wafisadi nashindwa kuelewa hata wale wasomi kama kina dr. Fulani wa kule kaskazini na nyanda za juu kusini wataalamu wa katiba haya hawana uwezo wa kusema maana ni wanakula na kulala na kuwa na magari ya kifahari kwa kuwa ni wana wa ccm = chukua chako mapema katika ari mpya nguvu mpya na kasi mpya ama kwa kifupi chake ni anguka

  inaniuma sana kupita ukakuta mtu amesajiliwa kabisa kama advocate
  au kama mtu anajitambulisha kama mwanasheria na yupo ndani ya kundi la wapinda sheria wazuia haki wala rushwa yeye inamsaidia nini haswa
   
 14. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Makahaba hao, hawajui uhuru wao nini
   
 15. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na dr Slaa kwamba hapa ndo tunapohitaji rais mwenye utashi wa kisiasa. Atupatie katiba mpya. Slaa for Tanzanians
   
 16. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #16
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao waandishi nawapa pole
  maana mwisho wa ajira zao ni 31-10-2010
  Tutabanana huku huku uraiani
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  These rates should have been controlled by the electoral commission; am I wrong?
   
 18. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  use it to free others too
   
 19. n

  nndondo JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wala msiwe frustrated na the likes of Muhingo na Bagenda kwa kuwa hawana any impact, hivi kuna mtu anasoma magazeti yao? ni kweli hivi sasa circualation figure yao wanaijua wao wenyewe kwa kuwa wanayemwandikia na huyo papa wao na vikaragosi vyao, hakuna mtanzania anayewasoma, actually tunawapa mileage kwa kuwajadili hapa, hebu ona tofauti wakati wao priority na focus yao ni uchupi sisi tuendelee ku focus on matters of National interest, tuko huko tuko mbali sana nao, hayo wanayoandika ndio wanayoyajua, ila kwa mwaka huu wamekosea, wasije kusema wametukanwa, Juu ya matarishi wa habari hao ni kweli kabisa, na sasa habari kamili ni kwamba alipowafuata amewaahidi u DC safari hii na kuwaomba wamsaidie, naomba sana watanzania wenzangu mwaka huu tukatae, tuwakatae na kuwatoa maana hela ni za kodi zetu, ni cha kushangaza sana kwamba kodi hizo hizo ndio wanazochezea kuwahonga hao watu, hebu wewe fikiria Muhingo huyo ndio aliyemtukana na kumchafua Diplomat wa kimataifa na mtu ambaye Tanzania inaendelea kujivunia mpaka leo Dr Salim Ahmed Salim, mtanzania mwenye kuongea lugha 17 zikiwemo 7 za kimataifa, H.H Prince Agakhan aliona hilo na kumfukuza, pale mwananchi leo hii anaitwa kuwa head wa kitengo cha habari, Je Dr Salim anajisikiaje? Inamaana huyo muhingo ni bora kwa CCM ambayo kwa leo hii ni JK na Ridhwani kuliko Dr Salim, cha kushangaa ni kwa Salim nae kukaa kimya badala ya ku make a statement na kuwashauri CCM wachague bega. PIli hilo baraza la habari nalo hakuna kitu, sijui kama wamehongwa ama uwezo wa watendaji na finyu, kwa sasa waandishi hawana control yoyote tena mara kumi TAMWA wanaweza kutoa statement ikasikika na kusikilizwa kuliko MCT na hata hiyo editors forum. Sasa dawa ni hiyo hiyo, jino kwa jino tuwashughulikie ile mbaya jamani, Pili kwa taarifa yenu mgombea wa CCM jana kazomewa Turiani, mwenye habari kamili aturushie hapa, wananchi wanadai kurudishiwa mashamba yao na hasa yale ambayo wenyewe hawayatumii likiwemo la Sumaye, yeye anasema atalishughulikia manake ni la kisheria, hapo ndio palipoleta utamu,
   
 20. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pesa yoyote ile itakayolipwa hata iwe ndogo kiwango gani WATABAKA HABARI TU!

  Kwa nini wakubali kulipwa na tujadili eti kiwango ni kikubwa au kidogo, hata hao CHADEMA wakilipa hicho kiwango watatia kirusi habari, maana hakuna atakayeandika OBJECTIVE JOURNALISM but rather LAPDOG JOURNALISM.

  Muandishi anapaswa kuwa independent from any pollution from the source iwe pesa, usafiri au hata kinywaji...ni wangapi wanaweza? wapo wachache sana na magazeti yao yanafahamika...
   
Loading...