Tanzania yetu na elimu bure.

bigcell

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
219
60
Habari za jioni wanajamvi, jioni hii kwenye kipindi habari za radio clouds FM, mtangazaji kaeleza kuwa ktk jimbo la Ilemela Shule ya msingi Hekima yenye wanafunzi wapatao zaidi ya 850 wamepewa mgawo Tsh. 450,000/- toka Serekali kuu za mpango wa elimu bure. Na uongozi wa shule unasubiri maekezo toka halmashauri mini cha kufanya.


Kwa mpango kweli Serikali ya JPM watafanikiwa?
 
w Wazitumie zikiisha wafunge shule, serikali imesha zoea kuchezea elimu ya nchi hii.
 
w Wazitumie zikiisha wafunge shule, serikali imesha zoea kuchezea elimu ya nchi hii.
Sasa Kama wameweka pesa kwenye accounts za shule kwa matumizi ya kunulia vifaa vya shule mwongozo wa mini tena? Au ni mbinu ya kuzifanya ziongezeke na za miezi ijayo ili zionekane nyingi? Viongozi wa nchi hii ni shida. Wanakurupuka kama pimbi kwenye vichuguu ili waonekane wanachapa kazi kumbe sanaa nyiiiingi. Chaki na vifaa vingine walimu watoe fedha zao?
 
Hii ngoma walidandia treni kwa mbele. Nadhani serikali ingelipa ada michango wazazi wangeendelea kutoa
 
Ushabiki na Kupenda sifa kutatufikisha pabaya! mi naona serikali pamoja na kujitoa kwa kiwango kutoa elimu bure lakini ingeruhusu wazazi nao kuchangia katika mambo baadhi ili kuleta tija na ufanisi katika elimu yetu! mi sioni kama kuluhusu wazazi kubweteka juu ya elimu ya watoto wao kwamba ni jambo la maana!
 
Back
Top Bottom