Tanzania yatajwa kama nchi pekee isiyokuwa na Covid 19 Ulimwenguni

Utafiti ambao wazungu itawachukua muda mrefu ni kwanini watanzania hawajapata corona na hakuna case yeyote iliyoripotiwa na wakiangalia Kenya, Uganda wote kesi za corona zipo.

Wao hawajui kuwa hata wale Nzige kwetu hawakugusa walienda Kenya, Uganda wakafika Kagera wakageuza kwenda India

Tuendeleee kuomba Mungu
Tuendelee. Kujifukiza
Acheni ujinga nyie mnaowaza bila akili! COVID ipo na inaua sana tu. Tatizo sisi Tz. hatutangazi matokeo ya upimaji kama nchi nyingine zinavyofanya!
 
Watanzania tumeichukulia corona kama mapepo.

Mimi ni miongoniwa wasioamini kwenye upuuzi wa "mapepo"....Mtu mmoja tu anajaribu kukuaminisha kuwa una mapepo na ni hatari kwa maisha yako alafu na wewe kwa udhaifu tu wa imani na akili unaingia kingi na kujifanya/kukubali una mapepo.
 
Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Bara la Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti magonjwa (ECDC) na baadaye ripoti hiyo kuchambuliwa na kusomwa na kituo kikubwa cha habari cha nchini Ujerumani cha Deutsche Welle (DW) imeitaja Tanzania kuwa nchi pekee duniani ambayo haijaripoti maambukizi yoyote ya mgonjwa wa Corona kwa wiki nne (4) zilizopita huku ikiwa salama na ugonjwa huo hatari duniani kwa sasa kwa takribani wiki 46.

Ripoti hiyo iliyotolewa na kituo hicho chenye makao makuu yake jijini Solna nchini Sweden, inaeleza kwamba wakati dunia nzima ikiwa kwenye giza totoro na isijue la kufanya kwa kuendelea kuripoti maambukizi ya Corona kila kukicha, Tanzania iko salama kabisa na balaa hilo na watu wakiendelea na shughuli zao za kila siku bila ya vizuizi wala masharti yoyote ya Corona.

CHANZO: CRI Swahili
Wachana na awamu ya tano
 
Unajuaje hilo? Unahakikishaje hilo?
Ugonjwa unao sambaa kwa kasi na kuuwa kwa muda mfupi huwezi kuficha taarifa zake za wagonjwa na vifo. Misiba ingekuwa mingi sana, na watu usingewaona wanajazana kwenye matukio makubwa kama kwenye mechi ya Simba na Yanga.

Huo ugonjwa ungekuwepo vifo vingesikika kila kona ya nchi, nawatu tunapenda kuishi tusingekutana hata kwenye kampeni. Kumbuka mikutano ya Magufuli aliyofanya CCM Kirumba na kule Kigoma watu walijaa Linex katoka alikotoka kapanda jukwaani kaamshaamsha shangwe,kelele,miruzi,ndelemo na vifijo mpaka unashangaa na bado akaenda jukwaa kuu kwa Waheshimiwa ambao hawajavaa barakoa na Linex mwenyewe hakuvaa barakoa, kama ugonjwa upo na taarifa zinafichwa inamaana viongozi taarifa hizo wanazo. Sasa kama taarifa hizo wanazo hakika Linex asingeweza kupata ruhusa ya kwenda jukwaa kuu na kuvalishwa kofia, achana na hiyo Diamond Mwanza CCM Kirumba kaimba mpaka anaenda kwa wanainchi anarukaruka kule uwanja mzima afu anaitwa jukwaa kuu.

Kwa mifano hiyo tu huyo Covid-19 kama angekuepo sasa tungekuwa tunapeperusha bendera nusu mlingoti.
 
Lissu na timu ya taifa ni asilimia ngapi ya watu wote wa Tanzania?

mi naona asilimia sometimes hai apply kote

mfano ukisema 40% (40/100) wameambukizwa alfu vipimo vijavyo ikatokea wale 60 ambao walikua safe wakapimwa 50 majibu yanakuja 0% (0/50) 😂😂

sjui imeeleweka vizur ninachotaka kumaanisha..
 
Yaani Ile mechi ya SIMBA na YANGA watu walivyojazana vileee....

Yaani kampeni za CCM na CDM na ile nyomiii....

Mapambano ya kina MWAKINYO na wengineo.....

HAKIKA ASHUKURIWE MUUMBA MBINGU NA NCHI...MUNGU PEKEE WA MWANZO NA MWISHO....Umetakasika Umetakasika Umetakasika!!!
Nakubali mzee baba
 
Isiyokuwa na Corona au haijaripoti Corona?

Haya ni mambo mawili tofauti.

Kuna mtu yuko hospitali alikuwa anapewa oxygen namfuatilia kama wamemtoa kwenye oxygen.
Lakini mkuu hizo oxgen si zilikuwa zinatumika kabla hata ya corona?
 
Tumewapoteza wapendwa wetu wengi sana na huu ugojwa sababu data zilikuwa zinafichwa na baadae watu waliokuwa wanakufa na huu ugojwa madaktali walitoa ripoti ya mengine yaliyokuwa yanaua
"Marehemu alikuwa akiugua na maradhi mengine"


Kauli tata sana hii ilikuwa ikitumika kwenye kutangaza vifo vya waliyokufa kwa corona.
 
Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Bara la Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti magonjwa (ECDC) na baadaye ripoti hiyo kuchambuliwa na kusomwa na kituo kikubwa cha habari cha nchini Ujerumani cha Deutsche Welle (DW) imeitaja Tanzania kuwa nchi pekee duniani ambayo haijaripoti maambukizi yoyote ya mgonjwa wa Corona kwa wiki nne (4) zilizopita huku ikiwa salama na ugonjwa huo hatari duniani kwa sasa kwa takribani wiki 46.

Ripoti hiyo iliyotolewa na kituo hicho chenye makao makuu yake jijini Solna nchini Sweden, inaeleza kwamba wakati dunia nzima ikiwa kwenye giza totoro na isijue la kufanya kwa kuendelea kuripoti maambukizi ya Corona kila kukicha, Tanzania iko salama kabisa na balaa hilo na watu wakiendelea na shughuli zao za kila siku bila ya vizuizi wala masharti yoyote ya Corona.

CHANZO: CRI Swahili
Kama hupimi utajuaje ugonjwa haupo? Ni kisa cha mbuni kufukia kichwa ardhini akidhani adui hamuoni.
 
Wewe ndio umethubutu kusema kweli watu wengi wanapotea mno na huu ugonjwa kama hutaambiwa kifua kimebana ghafla utaambiwa homa kali. Bado watu wanasema hakuna corona....... Mungu tuu atuepushe kwa kweli
Mkuu unakumbuka hospitali wahudumu walikuwa wanaogopa wagonjwa kipindi kile cha mwanzoni mwanzoni? Muhimbili pale ulikuwa hupiti bila barakoa na lazima upigwe sanitizer wakati wa kuingia na kutoka,ila sasa hakuna hayo mambo unaingia na kutoka kama kawaida uvae barakoa usivae hakuna mwenye kukuuliza.

Ukiangalia Rais na viongozi wote wa serikali hawaoneshi kutambua kuwa kuna uwepo wa corona Tz na hivyo wanatakiwa kuzingatia tahadhali zote za kujikinga.
 
Hahahaa..

nchi inayoongozwa na maviongozi masokwe ni vichekesho sana!
Na tatizo lawama zetu ni kwa hao viongozi masokwe kana kwamba tumewatoa msituni kumbe wametokana na sisi,yani ni marafiki zetu ndugu na jamaa zetu ndio hupatikana hao viongozi masokwe. Suluhisho ni sisi kuacha kuwa masokwe ndio hatutopata viongozi masokwe ila bila ya hivyo tutaendelea kupata viongozi masokwe tu.
 
Back
Top Bottom