Tanzania Yaongoza Unywaji wa Mataputapu

Tanzania Yaongoza Unywaji wa Mataputapu

Hao CNN kwanza walisema tunaongoza kwa uchawi Afrika sasa hivi wametujia na mataputapu. Kwahiyo tunaongoza kwenye mambo mabaya mabaya!.
 
ningefurahi kama ingeshika nafasi ya kwanza; hicho ni kinywaji asili cha mwafrika mzungu ndiye mnywa mataputapu asiyejua hata yatokako
 
Ukiona hivyo ujue huko Kenya wanaokunywa pombe za kienyeji ni wachache, binafsi naona kuziita pombe hizo mataputapu ni tusi. Huyo Dr. aliyefanya utafiti namshangaa kujifanya haelewi chanzo cha msongo wa mawazo hapa kwetu. Tatizo ni umaskini maana wanywaji wa pombe hizo ukiwapelekea bia watafurahi. Pato lao haliwaruhusu kununua bia. Sababu kubwa ya kunywa pombe yoyote iwe ya kienyeji au kizungu si msongo wa mawazo wanywaji uchukulia pombe kama kiburudisho na hivyo uwaongezea furaha katika maisha.

Pamoja na hasara zake ikiwemo kusababisha magonjwa, kudhoofisha uchumi, kusababisha njaa, hajari nk bado jamii inaendelea kutengeneza na kunywa pombe. Binafsi naona tunachotakiwa kufanya ni kuimprove namna ya kuandaa pombe hizo ili tupunguze madhara kwa wanywaji. Ukiangalia vitu viletavyo madhara kwenye afya za watanzania ni vingi sana kikiwemo chakula tunachokula kutokana na mazingira kinavyozalishwa na kuandaliwa. Yapo mambo mengi sana tunakohitaji maboresho.

Mtu akielimika na kipato chake kikaongezeka anakuwa macho na anachokula pamoja na kunywa. Lakini kwa hizo Division zero za form IV na wale wanaomaliza darasa la saba bila kujua kusoma au kuandika kuna Elimu hapo? Wamarekani wana msemo wao usemao " You are what you eat" (eat= kula na kunywa). Slogan ya CCM wakati wa uchaguzi ilikuwa maisha bora kwa kila mtanzania labda niwaombe akina Nape watueleze huwa wana maana gani wanaposema maisha bora? Na watwambie ni hatua gani mtu wa kijijini au watanzania walio wengi waliyopiga kuhusu kuelekea maisha bora. Maana to honest maisha bora kwa walio wengi hakuna. Unywaji wa pombe uliokithiri pamoja na mambo mengine yasiyokubalika katika jamii ni kielelezo tosha kwamba hatuna maisha bora.

Nyando nakuunga mkono kwenye suala la kusimamia ubora wa hizi pombe zilizooitwa Mataputapu! Hizi pombe ni za asili; zikiweza kutengenezwa katika mazingira masafi na pia zikauzwa\kunywewa katika maeneo safi hazina taabu yoyote,
Nchi jirani kama Mozambique wanao utaratibu wa kusimamia utengenezaji na usafi wa GONGO. Matokeo yake afya za watumiaji zinalindwa na watu wanakunywa kwa amani zaidi (hapa Bongo ukiwa kwa Mama Muuza, ukiskia vishindo vya boots unahisi ni polisi=lazima ufakamie chap na kukimbia). Kwa hiyo hata kulewa kwake kunakuwa kwa hvyohovyo!
 
CNN siwapendi kwani hawanaga zuri la kuripoti kuhusu Afrika! Ni kama Mwigulu na Nape wasioona zuri lolote ndani ya CDM.
 
Vizur viko ulaya Afrika wanaita pombe chafu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom