Tanzania yaongoza duniani kwa utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” amesema.

Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, amesema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.

“Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na BOT, ” amesema.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu amesema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” amesema.

Profesa Ndulu amesema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kumuza uchumi wa nchi.

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” amesema.

Ameongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

Chanzo:
Dewji Blog
 
Ni hatua nzuri sana lakini bado biashara nyingi hata zile kubwa kama za kuuza magari na vifaa vya kilimo, etc zilizo nchini hazipo kwenye internet!!! Tafadhali tujitahidi kila uwanja kwani mawasiliano haya yanakuza uchumi na kufanya maisha kuwa nafuu sana.
 
Na kweli kama sio hizi money transfer life lingekua tight sana kwa wengi wetu biashara ninazofanya haziwezi kwenda bila hii system so me ni mdau number moja.
 
Mie sishangai hilo
Maana sikumbuki lini nimeenda Bank,na nina Account Amana na CRDB na zote zipo Active sana tu.
Sasa kote huko natumia sim tu,maana siendi kwenye foleni kabisaaaaaaaaaaaa
Unless niwe nahamisha kwa umuhim wa kipekee au amount kubwa sana.

Lazima vie Bank uchwara vifunge,maana asikudanganye mtu,zile foleni za Bank kabla ya sim walikuwa wanaingiza pesa sana kwa miamala kupitia kwao

Ila kwa huduma ya sim,duhh,kuna watu Bank nilikuwa nakutananao enzi hizo ukienda leo kwa dharaura counter anakuuliza hivi fulani yupo au amefunga account,namuambia yupo na account yake ipo vizuri na anaingiza pesa na kutoka kwa sim

Hongereni sana kampuni za Sim,maana kabla ya hapo nilikuwa na Account NBC,ila kwa foleni ilibidi niifunge na kuisamehe.Maana unaingia saa tatu asubuhi unatoka saa sita au saba,aisee
 
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” amesema.

Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, amesema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.

“Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na BOT, ” amesema.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu amesema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” amesema.

Profesa Ndulu amesema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kumuza uchumi wa nchi.

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” amesema.

Ameongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

Chanzo:
Dewji Blog

Je kodi inalipwa au wana kwepa kodi ya Serikali ??????
 
Bado ni mzigo kwa watumiaji coz tozo ya miamala wanayowakata watumiaji ni kubwa mno kulinganisha na Huduma itolewayo na hata kodi ilipwayo kwa gvt.
 
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” amesema.

Chanzo:
Dewji Blog

Hiyo habari ni fix.
Nchi inayoongoza kwa mobile money transactions duniani ni Kenya. Ndiyo maana Visa sasa wameanzisha mVisa app, smartphone app yenye nia ya kushindana na mPesa Kenya. Of course, wana mpango wa ku-expand hadi Tanzania, Rwanda hadi Nigeria.

Cheki sources:

Mobile money: the African lesson we can learn | Rachel Botsman

Ripoti ya GSMA juu ya mobile money http://www.gsma.com/mobilefordevelopment/wp-content/uploads/2016/04/SOTIR_2015.pdf

Infographic ikionyesha hali ilivyokuwa mwaka 1 uliopita The top 7 African countries for mobile money (Infographics)

Na story ya mVisa app Visa is taking on the world’s largest mobile money platform on its home turf
 
Taasisi za kibenki zimezidiwa na simu katika kusafirisha pesa. Ingawa gharama za kusafirisha pesa kwa simu ni bei sana kulinganisha na benki
 
Back
Top Bottom