Tanzania yangu kunatokea nini ? Mbona matukio yanafuatana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yangu kunatokea nini ? Mbona matukio yanafuatana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Oct 19, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::10/19/2009Risasi, mabomu yatumika kumuokoa meneja 'mshirikina' Dar[​IMG]Na Geofrey Nyang’oro

  POLISI katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana walilazimika kutumia risasi za moto na mabomu ya kutoa machozi, kutawanya zaidi ya vibarua 2,000 wa Kiwanda cha Mohamed Enterprise Ltd, waliokuwa wakizuia kuondolewa kwa Meneja wa kiwanda hicho, waliyekuwa wakimtuhumu kwa imani za ushirikina.

  Tukio hilo lilitokea katika kiwanda hicho kilichoko eneo la Vingunguti kando kando mwa Barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Meneja huyo wa kiwanda kinajihusisha na utengenezaji wa maji na juisi, alikutwa na kadhia hiyo kati ya saa nne na saa tano asubuhi baada ya kutuhumiwa kumfanyia kafara, Mariam Sanga (26), mfanyakazi wa kiwanda hicho na kumsababishia kupoteza fahamu.

  Polisi walioingia katika eneo la kiwanda saa sita mchana na walipofika walikuta tayari wafanyakazi wakiwa wamempiga meneja huyo na kumlazimisha kufukua kitu alichokuwa amefukia katika lango la kuingilia ndani ya kiwanda hicho, kwa madai kuwa ndicho kilichokuwa kinachangia mwenzao kuwewseka.

  Katika sakata hilo, magurudumu ya gari ndogo iliyotumiwa na polisi kuingia katika kiwanda hicho, yalitolewa upepo na kuifanya ishindwe kuondoka.

  Hali kadhalika gari kubwa aina ya Defender, lilirushiwa mawe na kusababisha vioo kuvunjika.

  Mapambano hayo yaliyodumu kwa muda wa nusu saa yaliwalazimisha polisi kuongeza nguvu baada ya kuwasili kwa gari nyingine iliyokuwa na askari zaidi wakiwa na silaha.

  Walipofika katika eneo hilo walifyatua risasi hewani na kurusha mabomu ya kutoa machozi, ili kuwatawanya wafanyakazi.

  Hatua hiyo ilisaidia kuwafanya wafanyakazi kutawanyika na kutoa nafasi kwa gari lililokuwa limembeba meneja huyo, kuondoka katika eneo hilo.

  Wafanyakazi hao walisema walichukua hatua hiyo wakitaka mtuhumiwa wa ushirikina atoke katika kiwanda hicho akiwa na kidhibiti cha ushirikina walichomkuta nacho.

  “Sisi tunachotaka aondoke hapa akiwa na kidhibiti chake kile tulichokifukua pale mlangoni,” alisisika mmoja wa wafanyakazi hao huku Polisi wakiwa wamemfungia meneja huyo kwenye gari ndogo wakihofia usalama wake.

  Akisimulia kisa hicho cha kishirikina Mariam Sanga (26) anayedaiwa kufanyiwa kafara, alisema aliitwa na meneja huyo na kuamuriwa kuchimba shimo kwenye lango la kuingilia ndani ya kiwanda hicho. Alisema baada ya kuchimba shimo, ambalo lilikuwa dogo alitumwa kwenda kuchota maji kwenye ndoa na kuyaleta mlangoni ambako meneja wake alikuwepo.
  Tuma maoni kwa Mhariri
  Facebook
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Day after day, people are running out of options and tolerence is wearing out very fast. Anyway they now know that they have nothing to loose but their chains.
   
Loading...