Ni muda muafaka kuongeza Vivutio vya Utalii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

MHE. FESTO SANGA - NI MUDA MUAFAKA KUONGEZA VIVUTIO VYA UTALII

Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe. Festo Richard Sanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mpango wake wa 'The Royal Tour' ambao umesaidia kuongeza watalii na kuweka rekodi ya kupokea watalii wengi zaidi tangu kuasisiwa kwa sekta hiyo.

Sanga pia amemshauri waziri wa Wizara ya utalii Mohamed Mchengerwa kuwa na mpango wa kufuatilia watalii wanaokuja nchini, kujua wanavyohudumiwa na uzoefu wanaokutana nao ili kutafuta muarobaini wa sababu inayosababisha watalii kutorudi kwa mara ya pili kutalii.

Sanga amesema kujua vyema maisha na uzoefu wa watalii wanaokuja nchini ni vizuri wizara ikazungumza na madereva wa magari ya watalii na wasaidizi wa watalii kwani wao ndiyo wanaokaa muda mrefu na watalii wanaokuja kutalii nchini.

Mbunge huyo wa Makete mkoani Njombe pia ameishauri serikali kuwekeza malazi ya kisasa kwenye maeneo yenye vivutio vya utalii, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na taasisi za kifedha ili kusaidia mikopo itakayohamasisha watanzania kujenga hoteli za kisasa kwaajili ya kusisimua utalii kwenye maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii
 

Attachments

  • FxCz2RKWYAANbRp.jpg
    FxCz2RKWYAANbRp.jpg
    328.6 KB · Views: 1
Kuna mbuga za wanyama nyingi ila zingine hazina hadhi ya kimataifa
Inatakiwa barabara ziboreshwe na hata kuweka sehemu za mapumziko kama hoteli za uhakika

Sehemu kama Ugala mbunge alieomba waboreshe ana haki
Ina vutia sana ila haina hadhi
 
Back
Top Bottom