Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani

Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Posts
8,167
Reaction score
3,272
Tanzania imemkataa Balozi mteule wa Ujerumani ambaye alitakiwa kuja kufanya kazi nchini. Balozi huyo, Margit Hellwig-Boette alikuwa amemaliza muda wake nchini Kenya na alitakiwa kuja kuiwakilisha nchi yake Tanzania.
Balozi Hellwig-Boette alikaririwa na Gazeti la Standard la Kenya akieleza kuwa anajipanga kurudi kwao baada ya kukataliwa na Serikali ya Tanzania.

Alipoulizwa juu ya suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: "Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje ndio wanaoshughulika na hayo mambo, waulizeni."

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema wizara yake haijapata taarifa za kukataliwa kwa balozi huyo.

"Suala hilo linahusu ofisi ya Rais, mambo ya uteuzi ni ya Rais. Wizara ya Mambo ya Nje haina hiyo taarifa na hata kama ingekuwapo hiyo taarifa siyo ya `public'.

"Siyo taarifa ya umma kwa maana kwamba, mchakato wake ni wa siri na hayo mambo hayana kuuliza kwa nini. Ukileta jina la mtu unayetaka aje kuwa balozi likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni kwa nini.

"Unachofanya ni kuleta jina jingine, hata Rais hapa akipeleka jina la mtu kwenye nchi nyingine lisiporudi, hakuna kuuliza unachofanya ni kuteua tu jina jingine," alisema Mkumbwa.

Alikariri Kifungu cha Nne cha Azimio la Vienna ambacho kinaruhusu nchi kukataa balozi wa nchi nyingine bila ya kutoa sababu.
"Nchi inayopeleka balozi katika nchi nyingine inatakiwa kutoa jina mapema kwa nchi nyingine. Hata hivyo, nchi hiyo ina uwezo wa kumkubali au kukataa uteuzi," kinaelekeza kifungu hicho.

Gazeti hilo la The Standard, lilimkariri Balozi Hellwig-Boette akisema kuwa amekataliwa kuja Tanzania bila ya kuelezwa sababu.

"Ndiyo, Tanzania imekataa uteuzi wangu. Kwa mujibu wa itifaki za kidiplomasia, nchi husika ina haki ya kumkataa mtu aliyeteuliwa kwenda kuwakilisha nchi yake au kumkubali.

Tanzania imenikataa lakini haijatoa sababu yoyote ya kufanya hivyo. "Nitaondoka Nairobi kurudi Berlin Alhamisi (leo) asubuhi ili nikapangiwe sehemu nyingine," lilieleza gazeti hilo.

Hivi karibuni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga aliandaa chakula cha jioni, lengo likiwa ni kumuaga balozi huyo baada ya kumaliza kipindi cha miaka minne akiwa anaiwakilisha Ujerumani nchini Kenya.
Misimamo yake imemponza

Gazeti hilo limesema Hellwig-Botte ambaye alikuwa Balozi wa Ujerumani nchini Kenya tangu mwaka 2009, alikuwa anajulikana kutokana na misimamo yake na hasa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu na mara nyingine kuunga mkono vyama vya upinzani.

Anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Serikali ya Kenya kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kushtakiwa kwenye Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Kimataifa huko The Hague, Uholanzi kutokana na kuhusishwa na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Source: Mwananchi

------------------------------------------------------
Tanzania rejects outgoing German envoy Margit Hellwig-Boette!


By Geoffrey Mosoku

NAIROBI, KENYA: Tanzania has rejected the posting of Margit Hellwig-Boette, who has just finished her tour of duty in Kenya as Germany's ambassador to Dar-es-Salam.

It's not clear why the government of President JakayaKikwete rejected the envoy, who unlike her predecessors was less controversial, while serving in Nairobi.Margit has confirmed to the Standard that her posting has been rejected and saying she will be leaving to Berlin for redeployment.

"Yes, Tanzania has rejected my appointment. Under Diplomatic Code, a host country reserves the right to give consent for the posting of an envoy or reject.Tanzania has rejected but is not under any obligation to explain the reasons," she said. The envoy added; "I am leaving Nairobi for Berlin tomorrow (Thursday) morning for redeployment." Reports indicate that Kikwete's administration was not keen on taking the diplomat, who has just served in a neighbouring country.

On Thursday night, former Prime Minister Raila Odinga hosted the Germany envoy for a dinner to celebrate the end of her four year tour of duty. During the event, the diplomat said that in Kenya's 50-year history, the promulgation of the Constitution was the most significant event that promised to propel the country to prosperity.

"In my four-year stay here, I cannot think of anything else the leadership can bequeath the people of Kenya other than the full implementation of the Constitution," she said.
 
Amemaliza muda wake Kenya majuzi. Swali, kwani iko nini?

Tanzania has rejected the posting of Margit Hellwig-Boette, who has just finished her tour of duty in Kenya as Germany's ambassador to Dar-es-Salam.

It's not clear why the government of President Jakaya Kikwete rejected the envoy, who unlike her predecessors was less controversial, while serving in Nairobi.

Margit has confirmed to the Standard that her posting has been rejected and saying she will be leaving to Berlin for redeployment.

"Yes, Tanzania has rejected my appointment. Under Diplomatic Code, a host country reserves the right to give consent for the posting of an envoy or reject. Tanzania has rejected but is not under any obligation to explain the reasons," she said.

The envoy added; "I am leaving Nairobi for Berlin tomorrow (Thursday) morning for redeployment." Reports indicate that Kikwete's administration was not keen on taking the diplomat, who has just served in a neighbouring country.

On Thursday night, former Prime Minister Raila Odinga hosted the Germany envoy for a dinner to celebrate the end of her four year tour of duty.

During the event, the diplomat said that in Kenya's 50-year history, the promulgation of the Constitution was the most significant event that promised to propel the country to prosperity.

Margit has confirmed to the Standard that her posting has been rejected and saying she will be leaving to Berlin for redeployment.

"In my four-year stay here, I cannot think of anything else the leadership can bequeath the people of Kenya other than the full implementation of the Constitution," she said.

Standard Digital News - Tanzania rejects outgoing German envoy Margit Hellwig-Boette
 
Moja ya sababu za Balozi kukataliwa Tanzania ni kama anajihusisha na masuala ya ushoga. Inawezekana huyo akawa na hiyo sifa.
 
ni sababu za kisiasa zaidi hamna cha ushoga wala u gay hapo.
 
Balozi huyo Amekua na mahusiano ya karibu sana na chama kimoja wapo hapa Tanzania chenye sera na mlengo wa kikristo! Kwa habari za intelijensia balozi huyu ndie alie mleta yule naibu waziri wa maendeleo wa Ujerumani hapa nchini na kukutana na viongozi wa chama hicho hapa Tanzania mkoani kilimanjaro eneo la marangu,pia balozi huyo na naibu waziri wake baada ya kukutana na viongozi wa chama hicho alitaka kuonana na Membe,membe akawakatalia kuonana nao! Alivyo rudi kenya alisema maneno ya hovyo juu ya Tanzania!
 
Balozi huyo Amekua na mahusiano ya karibu sana na chama kimoja wapo hapa Tanzania chenye sera na mlengo wa kikristo! Kwa habari za intelijensia balozi huyu ndie alie mleta yule naibu waziri wa maendeleo wa ujerumani hapa nchini na kukutana na viongozi wa chama hicho hapa tanzania mkoani kilimanjaro eneo la marangu,pia balozi huyo na naibu waziri wake baada ya kukutana na viongozi wa chama hicho alitaka kuonana na Membe,membe akawakatalia kuonana nao! Alivyo rudi kenya alisema maneno ya hovyo juu ya Tanzania!


JF is Where We Dare To Talk Openly.
Haya ni majungu;
Wala sio Umbea.

Bazazi!
 
[h=1]Tanzania rejects outgoing German envoy Margit Hellwig-Boette[/h]NAIROBI, KENYA: Tanzania has rejected the posting of Margit Hellwig-Boette, who has just finished her tour of duty in Kenya as Germany’s ambassador to Dar-es-Salam.

It’s not clear why the government of President JakayaKikwete rejected the envoy, who unlike her predecessors was less controversial, while serving in Nairobi.
Margit has confirmed to the Standard that her posting has been rejected and saying she will be leaving to Berlin for redeployment.
“Yes, Tanzania has rejected my appointment. Under Diplomatic Code, a host country reserves the right to give consent for the posting of an envoy or reject.Tanzania has rejected but is not under any obligation to explain the reasons,” she said.
The envoy added; “I am leaving Nairobi for Berlin tomorrow (Thursday) morning for redeployment.” Reports indicate that Kikwete’s administration was not keen on taking the diplomat, who has just served in a neighbouring country.
On Thursday night, former Prime Minister Raila Odinga hosted the Germany envoy for a dinner to celebrate the end of her four year tour of duty.
During the event, the diplomat said that in Kenya’s 50-year history, the promulgation of the Constitution was the most significant event that promised to propel the country to prosperity.
“In my four-year stay here, I cannot think of anything else the leadership can bequeath the people of Kenya other than the full implementation of the Constitution,” she said.
 
Moja ya sababu za Balozi kukataliwa Tanzania ni kama anajihusisha na masuala ya ushoga. Inawezekana huyo akawa na hiyo sifa.

CCM na serikali ya kikwete hawataki Tanzania ipate katiba inayokubalika na yenye manufaa kwa wengi na ndio maana wanajitahidi kuchakachua mchakato wa katiba; huyu balozi wa kijerumani waliyemkataa aliwasaidia wakenya Katiba yao isichakachuliwe na wakina Kibaki na hiyo ndio sababu ya magamba kumkataa na siyo vinginevyo!!!
 
Balozi huyo Amekua na mahusiano ya karibu sana na chama kimoja wapo hapa Tanzania chenye sera na mlengo wa kikristo! Kwa habari za intelijensia balozi huyu ndie alie mleta yule naibu waziri wa maendeleo wa ujerumani hapa nchini na kukutana na viongozi wa chama hicho hapa tanzania mkoani kilimanjaro eneo la marangu,pia balozi huyo na naibu waziri wake baada ya kukutana na viongozi wa chama hicho alitaka kuonana na Membe,membe akawakatalia kuonana nao! Alivyo rudi kenya alisema maneno ya hovyo juu ya Tanzania!
Basi akatae mabalozi wote isipokuwa yule wa china. Tena ikiwezekana nchi zote zilazimishwe mabalozi wake wawe wachina.
 
Nchi mwenyeji(host country) ina haki ya kumkataa Balozi na haishinikizwi na sheria yoyote ya kimataifa au mkataba wa kidiplomasia wa Vienna wa mwaka 1961 katika kuelezea sababu za kumkataa.

Hii inatoa mwanya kwa watawala kulipiza visasi kidiplomasia kwa watu wasiowapenda kutokana na misimamo yao kisiasa
 
CCM's poor intelligence has discovered that the lady is a good supporter of CHADEMA!!
 
Nimesoma blog ya moja ya Wakenya wakisifia serikali ya JK kwa kukumkataa balozi wa Germany ambaye alikuwa anamaliza muda wake nchini Kenya,Bi Margit Hellwig-Boette.Wakenya hawa ni Wakikuyu to be honest.
Sababu kubwa eti huyu balozi alikuwa instrument wa kuwapeleka Uhuru na Ruto ICC.

Ulapdog wa serikali yetu ulianza pale Werema ,AG wetu eti alipowaandikia ICC kuhusu kesi ya Ruto na Uhuru.Tukumbuke wakati wa ule uchaguzi wa 2008,zaidi ya Wakenya 1500 waliua kwenye fujo wakati wa uchaguzi.
Huyu kilaza anatakiwa atetea serikali ya Tanzania,sio ya Kenya

Wakenya hasa utawala wa Uhuru na Ruto hawakufurahia Obama kutofanya ziara Kenya,na kuja Tanzania.
Angalia walivyotukejeli toka kuanzia hapo,pact ikawepo kati ya Kenya,Uganda na Rwanda kututenga .

How comes now serikali hii yetu ,inawalamba a***s hawa viongozi wa Kenya ,kwa Werema kuandikia ICC na sisi kumkataa balozi wa Germany kwa manufaa ya Kenya?

Hawa Wakenya sio rafiki wetu kabisa,Nyerere aliona hilo.Aliwaita Manyang'au.Tukumbuke wakati sisi tunafight apartheid ,kuhost freedom fighters kutoka Angola,Mozambique,SouthAfrica,Namibia,Zimbabwe and so on Kenya didnt care kabisa.Njojo alikuwa na uhusiano na makaburu.Hasa Wakikuyu ,ambalo ndio dominant tribe chini ya Kenyatta Sr.Kenya ilikuwa favourite ya "Wazungu",mpaka mwisho maana hawakufurahia msimamo wa Nyerere.

Kwa vijana wa sasa ,sisi tulipokuwa JKT ,miaka ya 80 ,tulimwimba Tom Mboya wa Kenya huyo.......!Tom Mboya alikuwa a brilliant Kenyan(Mjaluo) ambaye alikuwa na philosophy ya Nyerere.Kumbuka Toma Mboya ndie alifacilitate baba yake Obama kwenda USA kusoma.

Baba Nyerere rudi ,uone stupidity ya hali ya juu inaendelea nchini kwa sasa.Uliitoa nchi yako kwa hali na mali kukomboa weusi wenzako huko Southern Africa,wakati jirani yako(Kenya) alikuwa hajali kabisa
 
sasa hivi tunamkataa balozi wa China amekiuka mikataba ya Vienna kwenye mahusiano ya kidiplomasia Article 41(1) - (3)
 
Balozi huyo Amekua na mahusiano ya karibu sana na chama kimoja wapo hapa Tanzania chenye sera na mlengo wa kikristo! Kwa habari za intelijensia balozi huyu ndie alie mleta yule naibu waziri wa maendeleo wa Ujerumani hapa nchini na kukutana na viongozi wa chama hicho hapa Tanzania mkoani kilimanjaro eneo la marangu,pia balozi huyo na naibu waziri wake baada ya kukutana na viongozi wa chama hicho alitaka kuonana na Membe,membe akawakatalia kuonana nao! Alivyo rudi kenya alisema maneno ya hovyo juu ya Tanzania!



Kwa hiyo unataka awe na mrengo wa sera za kiislamu? S e r u k a m b a you
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom